TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, December 31, 2012

MAUAJI YA KUTISHA YATIKISA DAR MWAKA MPYA!

Picha za baadhi ya miili ya marehemu ikibebwa na kupakiwa kwenye Land Cruser ya Polisi tayari kupelekwa Hospitali kwa uchunguzi.
Na Livingstone Mkoi
Mauaji ya kutisha yamekikumba kitongoji cha Magomeni Makuti Mtaa wa Somanga kufuatia vijana wawili kupoteza maisha kwa matukio mawili tofauti.
Wakiongea na Xdeejayz wakazi wa eneo hilo walisema kuwa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Santiago aliuliwa na wananchi wenye hasira kwa kuchomwa moto kwa tuhuma za uwizi.

Wananchi hao ambao waligoma kutaja majina yao kwa usalama wao walisema"Huyo kijana alikuwa tishio maeneo haya hivyo siku ya tukio alitaka kumpora mzee mmoja aliyekuwa anatoka Msikitini ndipo alipopiga kelele wananchi wenye hasira wakamtia mikononi kisha kumpiga moto" Alisema dada mmoja mkazi wa maeneo hayo

Aidha katika tukio jingine kijana mmoja ambae inadaiwa ni mwenyeji wa mkoa wa Dodoma aliyefahamika kwa jina moja la Kiduka alikutwa amekufa kwenye gari  yenye namba T585 AFP aina ya Benz maeneo hayo hayo ya Magomeni mataa wa Somanga.

Hata hivyo Xdeejayz ilimtafuta kamanda wa polisi Kanda ya Kinondoni Charles Kenyela ili kuthibitisha tukio hilo hakuweza kupatikana na ilidaiwa baada ya maiti hizo kuchukuliwa na Polisi zilipekwa Hospitali kwa uchunguzi.

MDOGO WAKE KANUMBA AZUSHA BALAA KUBWA!

Diamond apania kuwaliza marembo kwenye USIKU WA WASAFI ndani ya Miasha Club kesho tarehe 1.

Saturday, December 29, 2012

Friday, December 28, 2012

DIAMOND AAPA KUFIA STEJINI NDANI YA MAISHA CLUB MWAKA MPYA!


NITAFANYA BALAA ZAIDI YA DAR LIVE, NEW MAISHA CLUB TAR 1 -I- 2013 - DIAMOND PLATNUMZ












DIAMOND AFUNGUA MWAKA NA USIKU WA WASAFI NEW MAISHA CLUB.

Mkali wa miondoko ya bongo fleva naseeb abdul a.k.a diamond platnumz tar 1 mwenzi wa kwanza atafanya show yakufa new maisha club ambapo atasindikizwa na dully sykes na ben paul.show hii kwa sasa ndio gumzo la jiji la dar es salaam kila mtu anasema lake juu wa kali wote hawa kwenye jukwaa moja.akiongea na x deejayz diamond platnumz amesema kwakawaida huwa hakosei anawaomba wapenzi wake wajitokeze kwa wingi new maisha club tar 1 mwaka mpya waje waone mambo mapya kutoka kwake. alijisifu kuwapa watu show mpya,nyimbo mpya na mambo mabo. kiiingilio ni buku 10 tu.

RATIBA YA BATA LA MWISHO WA MWAKA NEW MAISHA CLUB


UFUSKA WA MWANAMUZIKI MANAIKI SANGA WAANIKWA!



Wednesday, December 19, 2012

SAJUKI HALI TETE!

Msanii Juma Kirowoko "Sajuki" hivi karibuni alidondoka stejini baada ya kuzidiwa alipokuwa Mkoani Arusha.

Saturday, December 15, 2012

SNURA AJA NA VIDEO YA DEBE LA VANGA

 Hapa mzuka umepanda madansa wa snura wakiwa bize na ukamilishwaji wa video ya snura ya debe la vanga.video hiyo inatoka soon jumatatu imesimamiwa na director pabro wa APEX - subiria mzigo huo wakufungia mwaka lazima wakaeeeeee. alisema snura a.k.a snu sex.



 miuno miuno miuono miuno miuno

huyu ndio debe la vanga! una jua maana ya debe la vanga inamaana ya mtu anaepiga kelele lakini hana lolote. anajifanya ana magari kumbe anaazima hana tofauti na mdananda wazee wa slop wakitolaa

MWANAMUZIKI WA FM ACADEMIA B 52 AMEFARIKI DUNIA LEO

 Jopo zima la fm academia usiku wa ijumaa tar 14 ikiwa kwenye stagekwenye tamasha la miaka 15 ya fm academia iliyofanyika msasani club,show hiyo iliudhuliwa na umati mkubwa sana wa watu.

Huyu ndio mwanamuziki wa fm academia aliefariki dunia leo tar 15 saa 10 jioni ambapo marehemu alikuwa anaumwa kwa muda mrefu sana mpaka umauti kumkuta leo jioni. kwa mujibu wa kiongozi wa band ya fm academia nyoshi elisadat "amesema marehemu atazikwa jumatatu saa 9 katika makaburi ya kinondoni". mungu ailaze roho ya marehemu B 52 mahala pema peponi amin.

MOJA YA MAONESHO YA BURUDANI YALIYOVUNJA REKODI 2012 NI SHOO YA DTV KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI!

Shoo iliyovunja rekodi  kwa mwaka 2012 kwenye viwanja vya Jangwani kwa kuhudhuria na maelfu ya mashabiki!

CHRISTMAS YA MWAKA HUU ITAKUWA CHUNGU KWA WATANZANIA WALALAHOI!

 Wakazi wa Jijini Dar  kama walivyofumwa na kamera za Xdeejayz wakiwa kwenye mishemishe katika mitaa ya Kariakoo wakijiandaa na sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya kwa ugumu.
Mti maarufu kwa jina la "Christmas Tree"  Ambo watu wengi huufanya mapambo kwenye nyumba zao au maofisini kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Christmas.Lakini mwaka huu hali imekuwa tofauti kutokana na ugumu wa maisha watu wengi wameonekana kuupotezea  hasa  wale wenye vipato vya chini.
Na Livingstone Mkoi
Uchunguzi wa kina uliofanywa na Xdeejayz kwa kuongea na wanachi mbalimbali hasa wenye vipato vya kawaida umeonesha kuwa sikukuu ya mwaka huu itakuwa ya machungu tu kama zile zilizopita kutokana na ugumu wa maisha pamoja na upandishwaji bei vitu kiholera.

Wakiongea na mwandishi wetu watu hao walianza kusema kuwa sikiwa zimesalia siku tisa kufikia sikukuu ya Chrismasa na siku kumi na sita kufika mwaka mpya mambo yanazidi kuwa taiti kiasi cha kukata tamaa.

Mrs Chaku ambae ni mkazi wa Kimara Jijini Dar es Salaam alisema" Kweli hali ya maisha inazidi kuwa mbaya na kila siku inakuwa ni heri ya jana kwani wafanyabiashara wameanza kupandisha bei vitu sasa hapo unadhani sisi wenye vipato vya chini tutaweza kweli kula sikukuu kwa amani namna hiii bora tuwaachie hao wenye uwezo " Alisema Mama huyo

Aidha uchunguzi wetu umebaini wafanyabiashara  wengi wamenza kupandisha bei hasa mchere na nyama vitu ambavyo havikwepeki kununuliwa, Na wafanyabishara hao wakatoa madai kuwa hata wanakonunua sokoni nako kumepandishwa ndio maana na wao wanapandisha.

Wananchi wengi wametoa maoni yao kwa Serikali kusimamia   suala la wafanyabishara wabinafsi wanaopenda kupandisha bei vitu kwa masrahi yao kwani wanakuwa wanaumiza wanchi wenye vipato vya kawaida ambao hawana uwezo wa kununua kilo ya nyama elfu sita hadi saba.

WAKATI WAKO TOUR NI ZAIDI YA BURUDANI:JOE MAKINI

 Mwanamuziki Joe Makini
                                                Joe Makini
Na Mwandishi Wetu
Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa tamasha ambalo kwa siku chache tu limfenikiwa kujizolea umaarufu mkubwa  kiasi cha kutia "presure" matamasha mengi yaliyokuwepo siku nyingi si  "Ni Wakati wako Tour" limekuwa gumzo kila kona ya nchi huku mikoa mbalimbali ikiomba tamasha hilo kuwafikia kwa udi na uvumba.

Pamoja na kupiga shoo kazaa katika miji ya Dodoma na Dar es Salaam kuna wasanii kutokana na majukumu mengi hawakuweza kupiga mzigo hata siku moja mwanamuziki Joe Makini ni mmoja wa wasanii ambao hawakuwahi kufanya shoo ya Ni Wakati wako Tour lakini sasa ni zamu yake siku ya kesho kwenye ukumbi unaoongoza kusambaza virusi vya burudani Bongo wa Dar Live.

Joe amepania kufunika vilivyo kutokana na mara ya kwanza kufanya shoo kwenye tamasha hilo ambapo akiongea na Xdeejayz Joe alisema" Kaka namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi hii adimu najuwa wako wasanii wengi wanatamani kufanya shoo kwenye Wakati wako Tour  ni tamasha lenye zaidi ya burudani"  Alisema mwanamuziki huyo anaetokea Arusha

TWANGA PEPETA WAPANIA KUWAFUNIKA BONGO FLAVA KWENYE WAKATI WAKO SHOO DAR LIVE KESHO!

 Wanamuziki Luiza Mbutu na Amigo wakiwajibika stejini!

Wanenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta .
Na Livingstone Mkoi
Bendi ya muziki wa dance nchini The African Stars "Twanga Pepeta" wameapa kufanya shoo ya kihistoria itakayowafunika wanamuziki wa bongo wa Flava siku ya tarehe 16 kesho kwenye ukumbi namba moja kwa burudani bongo Dar Live.
Wakiongea na Xdeejayz wanamuziki wa bendi hiyo Amigo na Luiza Mbutu walisema kwa mara ya kwanza kufanya shoo kwenye tamasha la Ni wakati wako Tour hivyo wanataka kuwaonesha waandaji wa tamsha hilo kuwa walikuwa wanakosea kuwapa nafasi kwenye matamasha yaliyopita.

Luiza mbae ni kiongozi wa bendi hiyo alisema"Jamani tulikuwa tunatamani sana kufanya shoo kwenye tamasha hili la Ni wakati wako Tour lakini sasa tumepata nafasi sasa wasubiri kuona balaa lake kesho" Alisema dada Luiza

Aidha katika tamasha hilo linalotarajia kuacha historia katika ukumbi huo pia kutakuwa na wanamuziki wengi wa bongo flava watakaoshusha gharika ya burudani na shoo zote hizo zitaanza saa nane hadi saa sita usiku huku kiingilio kikiwa shilingi elfu 2000 kwa watoto na shilingi 5000, kwa wakubwa.

Friday, December 14, 2012

SAM WA UKWELI ADAIWA KUSHINDWA MAISHA,ARUDI KUISHI KWA WAKWEZE!

Mwanamuziki Samu wa Ukweli 
akiwa kwenye picha ya pozi.
Na Mwandishi Wetu
Kuna taarifa kuwa msanii aliyewahi kutamba sana kwenye muziki wa kizazi kipya nchini Samu wa Ukweli ameshindwa kuishi maisha ya kupanga hadi kwenda kuishi kwa wakwe zake maeneo ya Kiwalani Jijini Dar.

Habari za uhakika toka kwa mtu wa karibu na mwanamuziki huyo aliwika sana nyimbo zake kali kama Sina Raha na Hata Kwetu Wapo miezi ya hivi karibuni ametimuliwa na kwenye nyumba aliyokuwa anaishi maeneo ya Hananasifu kwa kile kilichodaiwa kushindwa kulipa kodi ya pango.

Hata hivyo baada ya Xdeejayz kupata umbea huo ilinyanyua mkonga wa simu yake na kumcheki hewani ili kuthibitha tuhuma hizo ambapo simu ya Samu iliita muda mrefu  bila hata ya  kupokelewa.

AFYA YA MZEE MAJUTO YAIMARIKA!

MSANII KING MAJUTO
Na Livingstone Mkoi
Afya ya Mzee Majuto aliyekuwa anaumwa sasa imerejea kwenye hali ya kawaida kufuatia kuanza kupata matibabu ya uhakika baada ya kuletwa Dar akitokea Tanga alikokuwa anajiuguza.

Habari za uhakika zilizofika mezani kwa Xdeejayz zinasema kuwa Mzee Majuto alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kuvimba miguu na shingo lakini hadi sasa hali yake inatia moyo kwani ameanza kufanyua majukumu yake mepesi mepesi tofauti na awali ambapo alikuwa anashindwa hata kutembea.

Kwa mujibu wa mtoto wake mzee Majuto alisema waliamua kumleta Dar baba yao ili kupata matibabu yenye uhakika zaidi.

MBWA MWENYE KICHWA CHA JOGOO ATIA HOFU YA KUMALIZIKA DUNIA!

Mnyama aina ya mbwa mwenye kichwa cha jogoo akiwa kwenye pozi!
Na Mwandishi Wetu
Ama kweli dalili za mwisho wa dunia dhahili zinaonekana kufuatia mambo ya ajabu ajabu kuibuka kila kona ya dunia.
Mbwa mmoja wa ajabu amezaliwa nchini Botswana akiwa na kichwa cha kuku dume jogoo na kusababisha mtafaruku mkubwa nyumbani kwa mfugaji huyo.
Habari zaidi zilisema kuwa mfugaji huyo aliyefahamika kwa jina la Jonsein Mutezo ambae anaishi nje ya mji alisema mama wa mbwa huyo yuko kawaida tu lakini baada ya kuzaa mbwa huyo alizaa kitoto hicho chenye kichwa cha jogoo.

NYOKA WA AJABU ALIVYOUAWA NA KUWEKA REKODI 2012 DUNIANI!

 Nyoka wa ajabu akiwa amepakizwa kwenye gari la kubebea kontena baada ya kuuliwa na wanajeshi nchini Misri.
Nyoka wa ajabu akipambana na zana za kijeshi bila mafanikio.Hata hivyo baada ya vita hiyo kudumu kwa siku tatu usiku na mchana hatimae nyoka aliuliwa kwa kupigwa  bomu kichwani.Tukio la nyoka huyo limeelezwa kuwa ni tukio lililovunja rekodi ya mwaka 2012.
Na Mwandishi Wetu
Katikati ya mwaka huu dunia ilikubwa na mshtuko mkubwa kufuatia kuonekana kwa nyoka wa ajabu nchini Misri na kusababisha watu kukumbwa na hofu kuu.

Tukio hilo lilitokea nchini Misri kwenye bahari ijulikanayo kwa jina la Bahari Nyekundu ambapo nyuko huyo anadaiwa alikuwa anaishi ndani ya kina kirefu cha maji lakini siku moja alionekana mkia wake ndipo vyombo vya wanausalama vikaingia kazini kumsaka.

Hata hivyo haikuwa kazi rahisi kumkamata au kumua nyoka huyo kutokana na ukubwa wake ambapo mapambano makali yalitokea kati ya nyoka huyo askari jeshi waliokuwa na zana zote za kivita lakini palichimbika sana.

Vita hivyo iliendelea karibu siku tatu nzima usiku na mchana ambapo nyoka huyo aliweza kuharibu vifaru zaaidi ya ishirini vilivyokuwa vikapambana nae hadi walipotumia helkopta maalum ya kivita ambayo inadaiwa ilifanikiwa kumlipua kichwa bomu na kufa papo hapo.

Aidha baada ya kufanikiwa kumuua nyoka huyo wananchi wengi wa mji huo walikosa amani kwa imani kuwa nyoka huyo hakuwa peke yake lazima atakuwa na watoto wake pamoja na mumewe kwani alikuwa jike na balaa likawa namna ya kumbeba hadi kumpeleka uwanja wa mako makuu ya jeshi la inchi hiyo kutokana na ukubwa wake.

MAAJABU YA MUNGU,MTI WENYE UMBO NA SURA KAMA YA BINADAMU!

Mti wa ajabu kama unavyoonekana ukiwa na sura kama ya binadamu pamoja viungo vinavyofanana  na mwanamke!
Na Mwandishi Wetu
Watafiti wa mambo Kaskazini mwa Misri wameshikwa na butwaa baada ya kuugundua mti mmoja mkubwa wenye umbo kama la binadamu tena mwanamke wa kike na kusababisha taharuki kubwan nchini humo

Habari juu ya maajabu hayo zilirushwa kwenye televisheni moja ya nchini humo na kusababisha wananchi nchini humo kuogopa huku wengine wakisema sasa huu ni mwisho wa dunia.

Hata hivyo maajabu mengine ya mti huo kama unavyoonekana kwenye picha huwa hauoti matawi lakini ni mbichi na ukiusogerea karibu unatoa unakutana na baridi kari zaidi ya ile ya kipupwe"AC" hali inayofanya kuwa kivutio kwa watalii wanaomiminika kuustaajabu.

Thursday, December 13, 2012

MUNGU AKINIJALIA HADI MWAKANI NATAKA NIWAINUE UNDERGROUND KUMI WAWE MASTAA!

Staa wa filamu za Kitanzania Nisha 
akiwa kwenye picha za pozi.
Na Livingstone Mkoi
Msanii nyota wa filamu Tanzania Nisha amesema kuwa ana mpango maalum wa kuwainua wasanii kumi wachanga na kuwa mastaa kabisa kwa vile wamekuwa wakisahaulika sana na kukumbwa na mitihani mizito.

Nisha akiongea na Xdeejayz msanii huyo alisema kuwa"Wasanii wachanga wanateseka sana wengi wao hasa wakike wanakumbwa na mitihani ya rushwa ya ngono bila msaada wowote nitawasaidia kadri nitakavyojaliwa kwani wako wengi wana vipaji" Alisema Nisha

Msanii huyo aliongeza kusema kuwa kama Mungu amemjalia yeye kupiga hatua kadhaa mbele lazima na yeye awavute wengine na sio kuwa wachoyo kwani hata kanuni za vitatu vya mungu vinasema ukitaka kufanikiwa kwa jambo lolote usiwe mchoyo.

WAKATI WAKO TOUR NA DTV KUILIPUA DAR LIVE JUMAPILI!

NYOMI LA MASHABIKI WALIOFIKA KWENYE VIWANJA VYA JANGWANI NA MWEMBE YANGA KWENYE MATAMSHA YA NI WAKATI WAKO TOUR!
Na Livingstone Mkoi
Maelfu ya mashabiki wa Mbagara na vitongoji vyake wiki hii wanatarajia kufurika kwenye viwanja vya Dar Live vilivyopo Mbagara Zakhem kwa ajili ya kushuhudia onesho kubwa na la kihistoria la muziki wa dance na bongo flava.

Akiongea na Xdeejayz mratibu wa shoo hiyo Hemed Kavu HK toka kampuni ya Entertainment Masterz LTD alisema onesho hilo la Ni wakati wako tour kwa asilimia kubwa limeombwa na mashabiki wa Wilaya hiyo ya Temeke.

"Kweli kabisa tulikuwa tumemaliza shoo zetu za Ni wakati wako tour kwa mkoa wa Dar es Salaam lakini kutokana na maombi mengi ya mashabiki tumekubari kufanya shoo hiyo ili watu .
wetu waendelee kupata mabadailiko ya burudani Tanzania kupita DTV" Alisema HK ambae ni mratibu wa matamasha ndani ya kampuini hiyo.
Aidha HK alieleza kuwa kwenye onesho hilo kutakuwa na burudani nyingi sana ambazo kimsingi hazijawahi kufanyika ndani ya ukumbi huo unatisha kwa burudani Jijini Dar tangu ufunguliwe Januari Mosi mwaka huu na burudani zote hizo zitakuwa na kiingilio kidogo sana cha shilingi elfu tano na elfu mbili kwa watoto na mpango mzima wa shoo inatarajia kuanza saa nane mchana hadi saa sita za usiku.

MAANDALIZI YA 40 YA SHARO MILIONEA JOHN MNYIKA AFUNGUA NJIA ATOA LAKI MOJA MCHANGO WAKE!

 Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupita CHADEMA John Mnyika.
Mbunge wa Ubumgo John Mnyika.
Na Livingstone Mkoi
Mbunge kipenzi cha watu katika Jimbo la Ubungo John Mnyika ametoa mchango wake wa shilingi laki moja kwa ajili ya maandalizi ya arobaini ya marehemu Sharo Milionea itakayofanyika hivi karubini nyumbani kwao Mkoani Tanga.

Habari za uhakika toka kwa wasanii wa Komedi ambao wamepanga kamati maalum ya kuchangisha mchango ili wafanikishe shughuri hiyo inayotarajia kuwa kubwa.

"Mheshimiwa  Mnyika ametoa laki moja kama sehemu ya mchango wake ambapo pia tunaendelea na zoezi la ukusanyaji michango ili tuweze kufanikisha zoezi hilo" Alisema mmoja wa wasanii wa Komedi Sheri Magali.
Arobaini hiyo inayotarajia kufanyika hivi karibuni Mkoani Tangu na tayari wasanii mbalimbali wameanza kujipanga kwa ajili ya kufanikisha 4