TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Saturday, December 15, 2012

TWANGA PEPETA WAPANIA KUWAFUNIKA BONGO FLAVA KWENYE WAKATI WAKO SHOO DAR LIVE KESHO!

 Wanamuziki Luiza Mbutu na Amigo wakiwajibika stejini!

Wanenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta .
Na Livingstone Mkoi
Bendi ya muziki wa dance nchini The African Stars "Twanga Pepeta" wameapa kufanya shoo ya kihistoria itakayowafunika wanamuziki wa bongo wa Flava siku ya tarehe 16 kesho kwenye ukumbi namba moja kwa burudani bongo Dar Live.
Wakiongea na Xdeejayz wanamuziki wa bendi hiyo Amigo na Luiza Mbutu walisema kwa mara ya kwanza kufanya shoo kwenye tamasha la Ni wakati wako Tour hivyo wanataka kuwaonesha waandaji wa tamsha hilo kuwa walikuwa wanakosea kuwapa nafasi kwenye matamasha yaliyopita.

Luiza mbae ni kiongozi wa bendi hiyo alisema"Jamani tulikuwa tunatamani sana kufanya shoo kwenye tamasha hili la Ni wakati wako Tour lakini sasa tumepata nafasi sasa wasubiri kuona balaa lake kesho" Alisema dada Luiza

Aidha katika tamasha hilo linalotarajia kuacha historia katika ukumbi huo pia kutakuwa na wanamuziki wengi wa bongo flava watakaoshusha gharika ya burudani na shoo zote hizo zitaanza saa nane hadi saa sita usiku huku kiingilio kikiwa shilingi elfu 2000 kwa watoto na shilingi 5000, kwa wakubwa.

No comments:

Post a Comment