TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, December 31, 2012

MAUAJI YA KUTISHA YATIKISA DAR MWAKA MPYA!

Picha za baadhi ya miili ya marehemu ikibebwa na kupakiwa kwenye Land Cruser ya Polisi tayari kupelekwa Hospitali kwa uchunguzi.
Na Livingstone Mkoi
Mauaji ya kutisha yamekikumba kitongoji cha Magomeni Makuti Mtaa wa Somanga kufuatia vijana wawili kupoteza maisha kwa matukio mawili tofauti.
Wakiongea na Xdeejayz wakazi wa eneo hilo walisema kuwa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Santiago aliuliwa na wananchi wenye hasira kwa kuchomwa moto kwa tuhuma za uwizi.

Wananchi hao ambao waligoma kutaja majina yao kwa usalama wao walisema"Huyo kijana alikuwa tishio maeneo haya hivyo siku ya tukio alitaka kumpora mzee mmoja aliyekuwa anatoka Msikitini ndipo alipopiga kelele wananchi wenye hasira wakamtia mikononi kisha kumpiga moto" Alisema dada mmoja mkazi wa maeneo hayo

Aidha katika tukio jingine kijana mmoja ambae inadaiwa ni mwenyeji wa mkoa wa Dodoma aliyefahamika kwa jina moja la Kiduka alikutwa amekufa kwenye gari  yenye namba T585 AFP aina ya Benz maeneo hayo hayo ya Magomeni mataa wa Somanga.

Hata hivyo Xdeejayz ilimtafuta kamanda wa polisi Kanda ya Kinondoni Charles Kenyela ili kuthibitisha tukio hilo hakuweza kupatikana na ilidaiwa baada ya maiti hizo kuchukuliwa na Polisi zilipekwa Hospitali kwa uchunguzi.

No comments:

Post a Comment