TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, December 13, 2012

WAKATI WAKO TOUR NA DTV KUILIPUA DAR LIVE JUMAPILI!

NYOMI LA MASHABIKI WALIOFIKA KWENYE VIWANJA VYA JANGWANI NA MWEMBE YANGA KWENYE MATAMSHA YA NI WAKATI WAKO TOUR!
Na Livingstone Mkoi
Maelfu ya mashabiki wa Mbagara na vitongoji vyake wiki hii wanatarajia kufurika kwenye viwanja vya Dar Live vilivyopo Mbagara Zakhem kwa ajili ya kushuhudia onesho kubwa na la kihistoria la muziki wa dance na bongo flava.

Akiongea na Xdeejayz mratibu wa shoo hiyo Hemed Kavu HK toka kampuni ya Entertainment Masterz LTD alisema onesho hilo la Ni wakati wako tour kwa asilimia kubwa limeombwa na mashabiki wa Wilaya hiyo ya Temeke.

"Kweli kabisa tulikuwa tumemaliza shoo zetu za Ni wakati wako tour kwa mkoa wa Dar es Salaam lakini kutokana na maombi mengi ya mashabiki tumekubari kufanya shoo hiyo ili watu .
wetu waendelee kupata mabadailiko ya burudani Tanzania kupita DTV" Alisema HK ambae ni mratibu wa matamasha ndani ya kampuini hiyo.
Aidha HK alieleza kuwa kwenye onesho hilo kutakuwa na burudani nyingi sana ambazo kimsingi hazijawahi kufanyika ndani ya ukumbi huo unatisha kwa burudani Jijini Dar tangu ufunguliwe Januari Mosi mwaka huu na burudani zote hizo zitakuwa na kiingilio kidogo sana cha shilingi elfu tano na elfu mbili kwa watoto na mpango mzima wa shoo inatarajia kuanza saa nane mchana hadi saa sita za usiku.

No comments:

Post a Comment