TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Saturday, December 15, 2012

CHRISTMAS YA MWAKA HUU ITAKUWA CHUNGU KWA WATANZANIA WALALAHOI!

 Wakazi wa Jijini Dar  kama walivyofumwa na kamera za Xdeejayz wakiwa kwenye mishemishe katika mitaa ya Kariakoo wakijiandaa na sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya kwa ugumu.
Mti maarufu kwa jina la "Christmas Tree"  Ambo watu wengi huufanya mapambo kwenye nyumba zao au maofisini kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Christmas.Lakini mwaka huu hali imekuwa tofauti kutokana na ugumu wa maisha watu wengi wameonekana kuupotezea  hasa  wale wenye vipato vya chini.
Na Livingstone Mkoi
Uchunguzi wa kina uliofanywa na Xdeejayz kwa kuongea na wanachi mbalimbali hasa wenye vipato vya kawaida umeonesha kuwa sikukuu ya mwaka huu itakuwa ya machungu tu kama zile zilizopita kutokana na ugumu wa maisha pamoja na upandishwaji bei vitu kiholera.

Wakiongea na mwandishi wetu watu hao walianza kusema kuwa sikiwa zimesalia siku tisa kufikia sikukuu ya Chrismasa na siku kumi na sita kufika mwaka mpya mambo yanazidi kuwa taiti kiasi cha kukata tamaa.

Mrs Chaku ambae ni mkazi wa Kimara Jijini Dar es Salaam alisema" Kweli hali ya maisha inazidi kuwa mbaya na kila siku inakuwa ni heri ya jana kwani wafanyabiashara wameanza kupandisha bei vitu sasa hapo unadhani sisi wenye vipato vya chini tutaweza kweli kula sikukuu kwa amani namna hiii bora tuwaachie hao wenye uwezo " Alisema Mama huyo

Aidha uchunguzi wetu umebaini wafanyabiashara  wengi wamenza kupandisha bei hasa mchere na nyama vitu ambavyo havikwepeki kununuliwa, Na wafanyabishara hao wakatoa madai kuwa hata wanakonunua sokoni nako kumepandishwa ndio maana na wao wanapandisha.

Wananchi wengi wametoa maoni yao kwa Serikali kusimamia   suala la wafanyabishara wabinafsi wanaopenda kupandisha bei vitu kwa masrahi yao kwani wanakuwa wanaumiza wanchi wenye vipato vya kawaida ambao hawana uwezo wa kununua kilo ya nyama elfu sita hadi saba.

No comments:

Post a Comment