KING MAJUTO
Asema hata akifa leo hataki wakanyage kwenye mazishi yake.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kuna taarifa kuwa msanii mkongwe wa komed nchini Tanzania Amari Othuman Majuto”King Majuto” amewapa laana kundi la Bongo Muvi na kusema hata ikitokea amekufa leo hataki wakanyage kwenye msiba wake.
Habari za uhakika kuhusiana na tukio hilo toka kwa wasanii wa Komedi nchini ambo walibaki msibani walisema Mzee Majuto alichukizwa sana na uchafu walioufanya wasanii hao wa Bongo muvi bila kujali kama msiba huo ulikuwa wa msanii mwenzao na walipaswa kuuheshimi kwa thati.
Wakiongea na Xdeejayz wasanii hao wa Komedi waliokuwa kwenye kikao chao kilichokuwa na lengo la kujuwa watafanyaje kwenye arobaini ya msanii mwenzao walisema” Kaka huko Tanga kuna makubwa bongo muvi wameikanyaga wenyewe kwa tabia zao mbovu sasa Mzee Majuto amewapa laana na kuwataka wasikanyage kwenye msiba wake” Alisema msanii huyo.
Aidha habari hizo ziliendelea kusema kuwa bongo muvi waliikanyaga wenyewe kwa tabia zao mbovu kwani licha ya kufika msibani pamoja na kushiriki mambo mbalimbali lakini kuna mambo ambayo yaliwaharibia kila kitu ambayo ni pamoja na kukutaa kukalia mkeka na kutaka kukaa kwenye viti ili wasichafuke.
Licha ya tukio la kukataa kukalia mkeka pia kuna baadhi ya wasanii waliingia wakiwa wamelewa chakali, hali iliyoonekana walikuja kuonekana tu na sio kuomboleza msiba huo uliohudhuriwa na maelfu ya watu toka mikoa mbalimbali.
Vyanzo vyetu vilendelea kusema kuwa katika hatua nyingine ambayo huenda ndiyo iliyomkwaza Mzee Majuto ni baada ya kuzika wasanii hao waliingia kwenye magari yao na kuondoka bila hata kuwapa mikono ya pole wafiwa au hata kukaa hadi siku ya tatu kama walivyofanya hata baadhi ya waandishi wa vyombo vya habari.
Aidha kuna tukio la uwizi wa Juisi,Maji pamoja Azam Cola za wafiwa nao zilichangia kumkwaza Mzee Majuto kwani kitendo hicho kilikuwa cha kinyama isitoshe pale msibani palikuwa na wageni wengi ambao walikaa hadi tatu ya msiba na walitegemea vinywaji hivyo vitatumika kwa wageni.
Kufuatia taarifa hiyo Xdeejayz ilimtafuta JB kupitia simu yake ya mkononi ili kuongelea sakata hilo la kuachiwa laana na Mzee Majuto JB hakuweza kupokea simu hadi habari hii inarushwa hewani.
No comments:
Post a Comment