TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, October 19, 2012

TUMEDHIBITI MAANDAMANO:KAMANDA KOVA
Wengi watiwa mbaroni!
Jeshi la Polisi Kanda Maalum  Dar Es Salaam limesema kuwa limeweza kudhibi maandamano ya Waislamu yaliyokuwa yafanyike Ijumaa ya leo kushinikiza kuachiwa huru kwa wenzao wanaoshikiriwa na Jeshi hilo kwa tuhuma mbalimbali za uvunjifu wa amani.

Akionge na waandishi wa blog hii Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam Bw. Suleiman Kova alisema” Jeshi letu limefanya kazi kubwa na nzuri kwa kuzuia maandamano hayo ambayo yangeweza kuleta uvunjifu wa amani kwa wananchi wasio kuwa na hatia” Alisema Kamanda Kova

Aidha Kamanda Kova aliongeza kusema kuwa watu kadhaa wanashikiriwa na Jeshi hilo kwa kukiuka agizo la Serikali kupitia Jeshi hilo.Hata hivyo timu wanahabari wetu waliokuwa mitaani kwa ajili ya kukusanya matukio walishuhudia katikati ya mji maduka yakiwa yamefungwa na hakuna kilichokuwa kinaendelea.

Mmoja wa wanafabiashara wa mitumba maeneo ya Mtaa wa Kongo alisema kuwa” Jamani tuliamua kusimama baishara zetu kwa kuhofia usalama wetu na mali lakini tunashukuru Mungu amesaidia hivyo hivyo” Alisema kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Ibarahim.

No comments:

Post a Comment