Mwanamuziki Mwana FA akisema chochote kupitia DTV kwenye msiba wa Sharo Milionea.
Waombolezaji wakiwa wamembeba mwanamke ambae alizimia kwenye msiba wa msanii huyo.
Nape akitoa salamu za rambirambi toka Chama Cha Mapinduzi ccm
nyumbani kwa Mwanamuziki huyo Mkoani Tanga Jana.
Na Livingstone Mkoi
Bila shaka kazi ya kumsindikiza kwenye makao ya milele aliyekuwa msanii nyota wa komedi na muziki nchini Sharo Milionea imekwisha lakini sisi tuliobaki tunapashwa kujiuliza tumejifunza nini kutokana na kifo cha ndugu yetu huyu?
Katika maisha ya mwanadamu yana sehemu kuu mbili kuzaliwa na kufa hata hivyo kutokana na usiri wa kutojuwa siku zetu za kufa tatizo ambalo limekuwa likimtatiza kila mmoja.Lakini kubwa zaidi Mungu katupa hali ya kusahau.
Si kama Sharo peke yake bali wengi tumeondokewa na wapendwa wetu kama vile wazazi, watoto wetu na hata wake/Wanaume zetu kila tukifikwa na matukio kama hayo hakika huwa hatuamini kama tutaweza kusahau kamwe lakini kutokana na mipango ya Mungu hali ya kusahau imekuwa ikitufunika sana wanadamu ambapo baada ya kitambo kidogo huwasahau wapendwa wetu waliotutoka.
Hali kadharika kama binadamu tungejuwa siku zetu za kuondoka pengine wengi wetu tungekesha makanisani na misikitini kwa ajili ya kufanya ibada lakini kwa bahati mbaya hakuna afahamue siku yake ya kuondoka duniani zaidi ya Mwenyezi Mungu Muumba Mbingu na vitu vyote vinavyoonekana.
Hata ndugu zetu wazungu.Wanasayansi waliobobea wamepewa ufahamu na maarifa ya hali ya juu wa kugundua mambo mbalimbali lakini kwa kifo wamegonga mwamba.
Sharo ameondoka na amemaliza kazi yake kwani kiimani ilikuwa ahadi siku yake ya kuondoka ilifika na mapenzi ya Mungu yametimia hilo lazima tukubaliane nalo.Lakini kazi kubwa imebaki kwetu sisi tulio hai je tunajipangaje ili na sisi saa yetu ikifika tuwe tayari tumeweka mazingira sawa ya kukutana na mwenyezi Mungu kwani hakuna imani yoyote ambayo inaruhusu binadamu asifanye mema na atakutana na Mungu!
Kila dini inahimiza binadamu kukumbuka ibada kwa vile ndio njia pekee ya kujiweka karibu na muumba ambapo hata vitabu vyote vinahimiza kukumbuka ibada si vinginevyo.Kwani maisha ya mwanadamu ni mafupi sana ambapo kwa mujibu wa vitabu vyote vya dini kila nafsi lazima itaonja mauti na kila mtu ataondoka kwa wakati wake utakapofika.
Ni ukweli usiopingika Sharo tulimpenda sana na ndio maana wengi wetu turishtushwa sana na taarifa za kifo chake tuliamua kusimamisha shughuri zetu na kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kwenda kushiriki mazishi yake,Kwa kweli Sharo katuachia somo kubwa sana kwetu.
Ukitizama Sharo hakuwa Milionea wa mapesa kama alivyojiita labda usema alikuwa anasaidia watu kuwapatia pesa la hasha bali ni upendo aliokuwa anauonesha kwa binadamu wenzake.
Katika maisha yake Sharo alikuwa rafiki wa kila mtu mtoto mdogo kijana hadi wazee na alipenda sana kushrikiana na watu kwenye matatizo licha ya kwamba hakuna binadamu aliyemakamilifu chini ya jua.
Binadamu tukitambua kuwa maisha yetu ni mafupi sana tunakiwa kuishi kwa upendo mkubwa kwa vile thote ni wapitaji kwenye hii dunia hivyo kutokana na vifo vya wapendwa wetu sio kwa Sharo tu au watu maarufu hapana binadamu wote kwani kwa Mungu hakuna staa, wala tajili thote ni kitu kimoja mbele zake na ndio maana hata tunapokufa huondoka kama tulivyokuja hivyo Upendo ni kitu muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku.