TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Wednesday, November 28, 2012

MAZISHI YA SHARO MILIONEA KUFURU!


 Umati mkubwa wa watu wakiwemo maandishi mbalimbali wa vyombo vya habari wakiwa nyumbani kwao Sharo Milione Mkoani Tanga muda mfupi kabla ya kuelekea Makaburini kwa ajili ya kuupumnzisha mwili wa mwanamuziki huyo.

 Mama Mkubwa wa Sharo ambae hakufahamika jina lake  akilia kwa chungu huku akishindwa kuamini kuhusu kifo cha mwanae huyo

 Kijana aliyedaiwa kuwa mjomba wa Sharo Milionea alishindwa kujizuia kwa simanzi kufuatia kuushuhudia mwili wa Sharo Mochare!

 Rafiki kipenzi wa Sharo Milionea,Kitare akiwa mwenye majonzi makubwa kufuatia kifo hicho.
Muigizaji nyota ambae alikuwa rafiki kipenzi cha marehemu, King Majuto akiel
kea Makaburini kwa ajili ya mazishi ya marehemu Sharo Milionea.


Boti ya abiria ambayo tangu juzi imekuwa ikifanya kazi ya kuwachukuwa waombolezaji toka Kenya hadi Tanga,Ambapo ilidaiwa watu hao ni mashabiki wa mwanamuziki huyo ambae  amezikwa  jioni hii ya leo Mkoani Tanga.
Na Mwandishi Wetu
Mazishi ya aliyekuwa na msanii mahili wa Komedi Tanzania na mwanamuziki wa kizazi kipya Sharo Milionea yameweka historia mpya nchini kufutia umati maelfu ya watu kijitokeza na kumzika.

Habari toka Mkoani Tanga zinasema kazi mbalimbali za kijamii zimesimama leo kwa ajili ya kushiriki kwenye mazishi ya mwanamuziki huyo aliyekuwa kipenzi cha watu nchini ambayo yamefanyika  jioni hii.

Katika hatua nyingie watu toka mikoa mbalimbali tangu jana wamekuwa wakimiminika kwa ajili ya msiba huo ambao umewashtu wengi,waandishi wetu waliopo huko wamesema kuwa msiba huo umehudhuriwa na maelfu ya watu wakiwemo wasanii ambao wameonesha ushirikiano mkubwa  sana kwenye msiba wa msanii mwenzao

Hata hivyo katika hali nyingine Boti za usafiri toka Kenya zimekuwa zikishusha watu zaidi ya mara tatu ambao wote walikuwa wamefika kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho.
Aidha ndugu wa marehemu wa mwanamuziki huyo waliwapongeza wananchi wote kwa kushiriki pamoja kwenye kipindi hiki kigumu cha kumsindikiza msanii huyo.

Viongozi mbali mbali wa Serikali toka Mkoani humo nao wameshiriki  vyema kwenye mazishi hayo pamoja na kutoa rambirambi zao kwa familia ya marehemu.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA AMENI

No comments:

Post a Comment