Wananchi wa Jiji la Dar watoto kwa wakubwa wakiwa wamekusanyika barabarani!
Hapa wananchi mbalimbali wakiangalia vichwa vya habari vilivyoandikwa kwenye magazeti mbalimbali kuhusiana na kifo cha mwanamuziki Sharo Milionea.
WANANCHI WENGI WALIOMBA AZIKWE DAR ILI WASHIRIKI MAZIKO YAKE!
.Lakini ilishindikana Watoto wa shule washindwa kujizuia na kujikuta wakiimba nyimbo zake madarasani.Na Mwandishi Wetu
Jiji la Dar es Salaam jana na leo limepooza kufuatia kifo cha aliyekuwa msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Sharo Milionea huku wengi wao wakitamani masanii huyo angezikwa Dar ili nao waweze kushiriki.
Wakiongea na Xdeejayz wakazi hao walisema kuwa kweli kifo hicho kimewasikitisha sana" Kweli tumeumia sana kwa taarifa za msiba huo kwani Sharo alikuwa kipenzi cha watu wote hivyo tumepokea kwa uchungu taarifa hizo" Alisema mkazi wa Magomeni aliyejitambulisha kwa jina la Mama Amina ambae alisema ana mfahamu siku nyingi Sharo
Wananchi waliendelea kusema kuwa kama wangekuwa na uwezo wa kuishawishi familia ya Sharo ili wakubari matakwa yao ni bora wangemzika huku huku Dar ambako ilikuwa maskani yake kubwa.
Kufuatia kifo cha Sharo ambae alizoeleka sana na wa lika zote kutokana na staili yake ya utembeaji,uigizaji,usemaji pamoja na uimbaji hivyo baada ya kifo hicho watoto wengi walishikwa na simanzi ambapo hadi watoto wa shule kushindwa kusoma wakimkumbuka msanii huyo.
"MUNGU AMETOA NA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE DAIWA AMENI"
No comments:
Post a Comment