TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, November 29, 2012

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU HUSSEIN RAMADHANI MKIETI-SHARO MILIONEA


HISTORIA FUPI YA MAREHEMU HUSSEIN RAMADHANI MKIETI-SHARO MILIONEA


Marehemu alizaliwa tarehe 20/03/1987. Marehemu walizaliwa mapacha lakini kwa bahati mbaya pacha mwenzake wa kike alifariki  siku ya pili baada ya kuzaliwa.


Marehemu Hussein ramadhani mkieti alisoma elimu ya msingi katika shule ya msingi ya LUSANGA iliyhopo kijiji cha lusanga wilaya ya MUHEZA na kumaliza mwaka 2001. Marehemu alijiunga na elimu ya secondary mwaka 2002 lakini kwa bahati mbaya kutokana na matatizo ya kifamilia hakuweza kumaliza shule na aliiishia kidato cha pili 2003. Mwaka 2004-2007 alijiunga na shuhuli za ujasiliamali na sanaa mwaka 2008 alijiingiza kwenye maswala ya kuimba na kuigiza comed na filamu, hadi umauti unamkuta HUSSEINI RAMADHANI MKIETI alikuwa ameingia mkataba na kampuny ya E MASTERS  kwa ajili ya kumsimamia kazi zake zote za muziki kwa ukaribu kabisa na HEMED KAVU (HK) ndie alikuwa msimamizi mkuu wa kazi zake. MAREHEMU SHARO MILIONEA AMEZIKWA KWENYE MAKABURI YAKIFAMILIA YALIYOPO KIJIJI CHA LUSAGA MKOANI TANGA KATIKA WILAYA YA MUHEZA.YALIYOPO NYUMA YA NYUMBA YAO.

MAREHEMU HUSEIN MKIETI -( SHARO MILIONEA) HAJAOA WALA HANA MTOTO.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU HUSSEIN RAMADHANI MKIETI-SHARO MILIONEA MAHALA PEMA PEPONI AMIN.

No comments:

Post a Comment