Na Livingstone Mkoi
Kwa kawaida ya binadamu
thote tulivyo iwe sehemu yoyote ya kazi kwenye uongozi nk.Huwa tunashindwa kutambua
umuhimu wa mtu huyo hadi anapoondoka katika mazingira hayo ndipo umuhimu wake
huonekana.
Najaribu kuweka hilo
wazi na kimsingi halina ubishi kwani ndio mazoea yetu binadamu na hapa
namuelezea kijana mwenzetu ambae ametuacha kwenye ulimwengu huu huku tukiwa
tuhahitaji mawazo yake mchango wake nk.
Sharo milionea amefariki
kwa sasa huku maelfu ya mashabiki wake wakiwa hawaamini pamoja na mimi mwenyewe
kwani mara ya mwisho wiki moja iliyopita nikiwa ofisini kwangu maeneo ya
Komakoma EML nilikutana na Sharo na tulizungumza mambo mengi kuhusu gemu ya
muziki wa kizazi kipya huku akiniambia kuwa anajiandaa kufanya video ya wimbo
wake mpya hivyo atanishtua tushirikiane.
Mimi nilimjibu powa huku
tukiachana kwa kupeana mikono lakini wakati naondoka kuelekea Kinondoni Mkwajuni
toka Maeneo ya Koma Koma Sharo aliniuliza naelekea wapi ili anape lifti ya gari
yake ambapo nilipomjibu ninako elekea aliniambia tuondoke wote na tukaiingia
kwenye gari hadi maeneo ya kwangu na kunishusha.
NILIANZA KUMJUWA SHARO
TOKA ALIPOIGIZA KOMEDY YA ‘MWEMBWE”
Sharo akiwa chini ya
kampuni ya Beknet Production miaka mitano iliyopita huku akiwa na rafiki zake wakubwa
Kitale.Kipemba,Kishoka na wengineo
ambapo katika komedy hiyo Sharo alimudu vyema kuigiza hadi kuonekana kuwafunika
wenzake hasa kutokana na nafasi aliyokuwa anaigiza pamoja uongeaji mzuri na wa
kuvutia kwa mashabiki wake.
Katika maisha yake Sharo
alipenda sana masihara kwa kila mtu na aliheshimu kila mtu pamoja na rafiki
zake wakubwa watoto wadogo ambapo hali hiyo ya kujali binadamu wenzake ilimpa
umaarufu na kumjengea heshima kubwa nchini.
ANAVYOKUMBUKWA NA MASTAA
WENZAKE!
Ni dhahili kuwa kuwa
Sharo alikubalika hata na mastaa wenzake hapa MKURUGENZI WA CLUB MAISHA CLAUD CIZA
anaelezea namna alivyomjuwa na kumchukulia kama msanii anaetarajia kuja kuwa
tishio kimafanikio nchini” Kifo cha Sharo kwa kweli ni kimenigusa sana kama
ambavyo kimewagusa wengine nilimjuwa Sharo miaka miwili iliyopita kwa kuangalia
kazi zake za sanaa hasa komedy na nikaanza kuwa na ukaribu nae baada ya kuingia
kwenye muziki ambapo tulishirikiana mambo mengi sana kwenye muziki” Alisemna
Claud
Hata hivyo
MKURUGENZI huyo aliongeza kusema”Sharo
alikuwa anatumia juhudi binafsi ili kumletea mafanikio na alikuwa amefanikiwa
lakini kwa bahati mbaya ameondoka ghafra na nyota yake kuzimika lakini hata
hivyo Mungu apewe utukufu kwa vile yeye ndiye muamuzi wa yote”Alimaza
kumuelezea
NISHA MSANII WA BONGO
MUVI NAE AMUELEKEZE NAMNA ALIVYOMJUWA SHARO!
Msanii nyota wa bongo
muvi Nisha alimuelezea Sharo namna alivyomjuwa”Nilimjuwa Sharo kama kwa mambo
mengi kwanza nilimkubari kwenye kazi zake ubunifu kwenye sanaa ulimfanya kila
msanii avutiwe nae hivyo sitoweza kumsahau kwa hayo” Alisema Nisha.
MUNGU AMETOA NA AMETWAA JINA LAKE
LIHIMIDIWE DAIMA AMEN
No comments:
Post a Comment