Afande Machemba katika ubora wake akiwa kwenye picha ya pozi dakika chache kabla ya kuingia Location kukamua kwenye moja ya filamu alizoshirkishwa hivi karibuni huko Mkoani Arusha mara baada ya kupokea mwaliko toka kwa wasanii wa huko wakimtaka akacheze filamu.
Afande
Machemba
Marehemu Steven Kanumba ambae ni kabila moja na Afande Machemba wote ni Wasukuma.
Na Mwandishi Wetu-Mwanza
Msanii Kinda toka kiwanda cha filamu za Kitanzania Joseph Machemba ameendelea kuwa gumzo nchini na safari hii mashabiki wa filamu toka Kanda ya Ziwa wamejikuta wakibubujikwa na machozi mara wanapoongalia filamu alizocheza msanii huyo toka Shinyanga ambae kwa sasa amehamishia makazi yake Jijini Dar huku wengi wakimfananisha na Marehemu Kanumba.
Mmoja wa wadau wa filamu Mkoani Mwanza aliyejitambulisha kwa jina la Majiha Mankunga alisema' Jamani tunamshukuru Mungu kwa kutupoza machungu tuliyoyapata miaka kadhaa iliyopita kwa kuturudishia mtu mwingine muhimu kwetu, huyu Afande Machemba hakika ni kama Kanumba amezaliwa upy" Alisema mtu huyo ammbae ni msambazaji wa filamu za kitanzania kanda ya ziwa
Msanii Joseph Machemba ambae kwa sasa anatamba kwenye filamu za Bifu la Kitongoji na Filamu ya AKIRI NYINGI ambazo ndani yake msanii huyo ameonesha uwezo wa ajabu kiasi cha kuwashangaza mastaa mbalimbali wa bongo movie kwa kipaji alichokuwa nacho Afande Machemba, Huku watanzania wengi wakimtakia kila raheli msanii huyo kwa juhudi zake
TANGAZO MAALUM
TANGAZA NA SISI
Thursday, January 28, 2016
Saturday, January 23, 2016
WACHUNGAJI, MASHEKH WAWACHARUKIA RAIS MAGUFULI, DC MAKONDA NA LUKUVI, WAFUNGA SIKU 40, WASEMA MUNGU ATAKACHOWAFANYIA ULIMWENGU UTAJUA...!
Mmoja wa wazee wa Kanisa la Hossana akiwa kwenye hisia kali ya maombi kwa Mungu
Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Hosana Mch Mzola
Waziri wa Ardhi Mh Lukuvu kwa sasa yupo chini ya maombi hayo ili afanye maamuzi sahihi.
Mchungaji Amos Mbena Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Holness Mision lililopo Kimara lakini mchungaji huyo amekuwa akiguswa sana na mgogoro huo hivyo nae ameungana kuongeza nguvu ya maombi ili viongozi hao wasikie kilio cha wananchi hao.
Shkhe Sharif Khamis kijana mwenye nguvu ya ajabu kwenye maombi nae ameungana na watumishi hao mbalimbali na wananchi kwenye maombi ya kumaliza mgogoro wa ardhi wa eneo hilo.
Wakina mama na watoto ambao kwa sasa wanaishi mazingira magumu baada ya nyumba zao kubomolewa na polisi kwa shinikizo la mafisadi, wakimlilia Mungu wao.
Na Mwandishi wa Maskanibongo Gazeti
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda, Rais Magufuli na waziri wa Ardhi Mheshimiwa Lukuvu wapo chini ya maombi makali ya siku 40.
Wakazi wa Kata ya Wazo kwenye Mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa wakishirikiana na mashekh na wachungaji wameanzisha maombi hayo maalum kwa ajiri ya Mungu kuwafungua viongozi hao ili wamalize mgogoro huo ndani yake wenye harufu ya rushwa na ufisadi huku maafisa Ardhi na watu wa Mipango Miji Manspaa ya Kinondoni wakitajwa kuhusika.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wachungaji wa makanisa yaliyopo Mitaa ya Nyakasangwe na Nyakalekwa walisema" Tupo kwenye maombo haya ili Mungu awafungue viongozi wetu kwa vile wao ndiyo wenye mamlaka ya mwisho wamalize hili jambao kwani tunaamini Tanzania kwa sasa imepata rais ambae watanzania walikuwa wakimuhitaji hivyo tumeona ni vyema tukamlilia Mungu azidi kumfungua zaidi na kuona hata mgogoro uliopo kwenye mtaa wetu " Alisema Mchungaji Mzola
Hata hivyo wachungaji hao waliendelea kusema kuwa kazi kubwa aliyoifanya Mheshimiwa Paul Makonda ni kubwa sana na hakika sasa mahara alipofikia anahitaji nguvu ya maamuzi ya Mheshimiwa Waziri Lukuvi na Rais kwa vile mtandao alioukuta mheshimiwa Makonda kwenye mgogoro wetu ni mkubwa na inaelezwa ndani yake kuna baadhi ya vigogo wa Ardhi Manspaa.
Wakazi hao waliendelea kusema Mheshimiwa Makonda amediliki kuhatarisha maisha yake kwa kupigania haki ya wananchi licha ya kwamba amekuwa akikutana na vikwazo kutokana na kuzungukwa na watu ambao hawapo upande wake bali wakiwa upande wa mafisadi hivyo sasa ni zamu ya Waziri kumpa meno ya yenye makali kumaliza mgogoro huo kwa kutoa maamuzi yatakayoondoa kabila mgogoro huo.
Mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa inaongozwa na Mwenyekiti wake Peter Bilebela ambae amekuwa kipenzi cha wakazi hao kutokana na utendaji wake wa hali na kuogpa rushwa kama ukoma, hali hiyo imepelekea kuchukiwa na upande wa pili wa mafisaidi kiasi cha kumtengenezea zengwe kila kukicha kwa kutumia pesa waliyokuwa nayo
Friday, January 22, 2016
HATARI YA NJAA MPWAPWA DODOMA: WANANCHI WASHINDIA MBOGA ZA MAJINI KUNUSURU MAISHA YAO, WAMTOLEA UVIVU MBUNGE WAO MWENYE TABIA YA KUKAA KIMYA BUNGENI, WAMTAKA ASIONE AIBU AOMBE MSAADA ILI KUOKOA MAISHA YAO, PICHA HIZI HAPA....!
Thursday, January 21, 2016
BONGO MOVIE YAWEKWA CHINI YA ULINZI MKALI NA AFANDE MACHEMBA, WATANZANI WASEMA AFANDE HUYO PEKEE NDIYE ANAEWEZA KUVAA VIATU VYA MAREHEMU KANUMBA..!
Afande Machemba akiwa mzigoni ambapo Watanzania wengi wamefurahishwa na kipaji cha msanii huyo toka Kanda ya Ziwa ambae kwa sasa amehamishiwa jeshi lake Jijini Dar ili kuikomboa tasnia hii ya filamu ambayo hadi sasa imebaki na wauza sura tu.
Afande Machemba akiwa kwenye moja ya sinema zake
Afande Machemba akiwa kwenye majukumu yake kikazi
Na Mwandishi Wetu
Matumaini ya watanzania yaliyokuwa yamepotea baada ya msanii aliyekuwa na uchungu na Tanzania pamoja na Tasinia ya Filamu marehemu Steven Kanumba kuondoka Dunia, hatimae sasa yameanza kurejea baada ya msanii Kinda mwenye kipaji cha ajabu kwenye kuigiza Joseph Machemba maarufa kwa jina la "Afande Machemba" kuonesha anaweza
Msanii huyo mwenyeji wa Kanda ya Ziwa akitoka Mkoa wa Shinyanga kwa sasa ndiye amekuwa habari ya mjini kwenye tasnia ya filamu baada ya kuonesha uwezo wa kipekee kwenye moja ya filamu zake alizoshirikishwa ambapo zote zipo mtaani kwa sasa.
Filamu alizoonekana Afande Machemba ni pamoja na, Karoge Tena, Night Dress, Akiri Nyingi, Siku Moja na nyinginezo nyingi.
Katika filamu hizo msanii huyo ameonesha kama anakipaji na anataka kuifisha tasnia hiyo kimataifa.
Akiongea na mwandishi wetu msanii huyo mpole na asiye na majivuno alisema " Kaka nawashukuru Watanzania kwa kunipokea kwa kweli kazi za mikono yangu zinapendwa sana ambapo hadi sasa watanzania wamenielewa nini ninachotaka kuwafanyia au kuifanyia nchi hii kimataifa hivyo waniunge mkono tu, lakini pia kwa sasa tayari nimepata mtu wa kunisimamia ambae ni mdau Livingstone Mkoi ambapo hadi sasa tayari ameanza kuniwekea mikakati ya kuwa Afande Machemba mwingine" Alisema
Afande Machemba akiwa kwenye moja ya sinema zake
Afande Machemba akiwa kwenye majukumu yake kikazi
Na Mwandishi Wetu
Matumaini ya watanzania yaliyokuwa yamepotea baada ya msanii aliyekuwa na uchungu na Tanzania pamoja na Tasinia ya Filamu marehemu Steven Kanumba kuondoka Dunia, hatimae sasa yameanza kurejea baada ya msanii Kinda mwenye kipaji cha ajabu kwenye kuigiza Joseph Machemba maarufa kwa jina la "Afande Machemba" kuonesha anaweza
Msanii huyo mwenyeji wa Kanda ya Ziwa akitoka Mkoa wa Shinyanga kwa sasa ndiye amekuwa habari ya mjini kwenye tasnia ya filamu baada ya kuonesha uwezo wa kipekee kwenye moja ya filamu zake alizoshirikishwa ambapo zote zipo mtaani kwa sasa.
Filamu alizoonekana Afande Machemba ni pamoja na, Karoge Tena, Night Dress, Akiri Nyingi, Siku Moja na nyinginezo nyingi.
Katika filamu hizo msanii huyo ameonesha kama anakipaji na anataka kuifisha tasnia hiyo kimataifa.
Akiongea na mwandishi wetu msanii huyo mpole na asiye na majivuno alisema " Kaka nawashukuru Watanzania kwa kunipokea kwa kweli kazi za mikono yangu zinapendwa sana ambapo hadi sasa watanzania wamenielewa nini ninachotaka kuwafanyia au kuifanyia nchi hii kimataifa hivyo waniunge mkono tu, lakini pia kwa sasa tayari nimepata mtu wa kunisimamia ambae ni mdau Livingstone Mkoi ambapo hadi sasa tayari ameanza kuniwekea mikakati ya kuwa Afande Machemba mwingine" Alisema
HALI YA MSANII MANAIKI SANGA KIMAISHA INASIKITISHA, SASA ANAPAKIA MATOFARI JAPO APATE HELA YA KULA, MASKANIBONGOTZ LAMNASA LIVE..!
Msanii wa Filamu na magizo Manaiki Sanga akipatakia matofari huko Wazo kwa ajiri ya kujipatia ridhiki, ambapo imedaiwa kufuria kwa msanii huyo kumetokana na kuwapanga mademu kama ndoo bombani. |
Kajala Masanja ametajwa kwenye kashfa ya kufilisika msanii Manaiki Sanga, huku watu wengi wakisema Kajala anatakiwa kutomtupa Manaiki kwa vile aliwahi kumsaidia vitu vingi kwenye sanaa. |
Wednesday, January 20, 2016
USHIRIKINA: MWANAMKE AKUTWA KWENYE PAA LA JENGO LA WIZARA TA FEDHA AKIWA MAZINGIRA YA KUTATANISHA, WAFANYAKAZI WAGOMA KUINGIA NDANI KWA HOFU YA KULOGWA, PICHA HIZI HAPA...!
Manamke ambaye
jina lake halikupatikana mara moja akiwa amekaa juu ya paa la majengo ya
Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam leo.
Mwanamke huyo
akizungumza na watu waliokusanyika lakini alikuwa hasikiki vizuri maneno
aliyokua akiongea kutokana na wananchi waliokusanyika kumuuliza maswali
mengi kwa wakati mmoja.
Polisi akiwa
pembeni ya uzio wa majengo ya wizara ya fedha na mipango mara baada ya
mwanamke huyo kuwa juu ya paa la nyumba hizo. Baada ya muda wafanyakazi
wa wizara hiyo walimwekea ngazi na kumshusha ili kumhoji zaidi nini
kimemfanya apande juu ya paa la majengo hayo.
Tuesday, January 19, 2016
DC MAKONDA, WAZIRI LUKUVI WASHIKWA PABAYA, TAKUKURU KINONDONI YACHAFUKA, NUSRA WASABABISHE MAUAJI, NI BAADA YA AFISA WAKE ASIYYEKUWA MUADILIFU KUMPIGA VIBAYA MWANANCHI NUSU YA……..!
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Simon Sirro
mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyakasangwe Peter Bilebela aliyekaa karibu na Mh Paul Makonda ambae anazungumza na wakazi wa eneo hilo.
Huyu ndiye mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyakasangwe Peter Bilebela akiwa kwenye moja ya majukumu yake na wananchi hivi karibuni
mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyakasangwe Peter Bilebela aliyekaa karibu na Mh Paul Makonda ambae anazungumza na wakazi wa eneo hilo.
Huyu ndiye mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyakasangwe Peter Bilebela akiwa kwenye moja ya majukumu yake na wananchi hivi karibuni
Na Mwandisahi wa Maskanibongo gazeti
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua hali ya utekelezaji wa agizo la Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni na Waziri wa Ardhi Mheshiwa Lukuvi la kutaka maeneo yote
yenye migogoro yapimwe ili kupata ufumbuzi wa mizozo hiyo inayoendelea Jijini ,
lakini kwa Kata ya Wazo hali imekuwa tofauti baada ya zoezi hilo kuonekana kuwa
na dalili zote za kuvurugwa ili likwame.
Habari zaidi zilieleza kuwa mgogoro huo wa Wazo mtaa wa Nyakasangwe
umekuwa na mitihani mingi hasa kwa viongozi wa Serikali ya Mtaa huo unaongozwa
na Mwenyekiti wake Peter Bilebela “Mchungaji”
Kwani mgogoro huo unaohusisha watu wenye fedha nyingi ambao hujiita wenye
mashamba na wananchi ambao wanaoitwa wavamizi huku nyuma yake kukiwa na
masirahi ya baadhi ya vigogo wazito.
Tukio la jana la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Mtaa huo
Peter Bilebela na watu waliofika ofisini kwake huku mwenyekiti huyo akiwa
kwenye majukumu yake ya kikao na wajumbe huku watu hao wakijitambulisha kama
wao ni maafisa TAKUKURU bila kuonesha vitambulisho.
Akiongea kwa masikitiko makubwa Mwenyekiti mbele ya Kamanda Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni wakati
akihojiwa mara baada ya kufikishwa kwenye Ofisi za Takukuru zilizopo Magomeni
Mapipa Jijini Dar es Salaam alisema maafisa hao waliokuwa wametumwa kumkamata
walitumia ubabe mkubwa na nguvu nyingi kuliko hekima na ustaarabu kwa kumpiga
mbele ya watu.
Mwenyekiti huyo aliendelea kumueleza Mkuu huyo wa
Takukuru ambapo Maskanibongo ilifanikiwa kunasa mazungumzo hayo ambapo
mwenyekiti huyo alimueleza kamanda huyo kuwa mara baada ya vijana hao kufika
ofisini kwake walianza kumkamata mjumbe wake wa Serikali ya mtaa aliyefahamika
kwa jina la Mohamed Mangundungundu .
Baada ya kumkata mjumbe huyo aliyekuwa amekaa nje ya
ofisi kisha wakamfata Mwenyekiti ambae alikuwa kwenye kikao na kumtaka atoke
nje ili apande kwenye gari, lakini mwenyekiti huyo aliwaambia kwamba kuna nini
na wao ni akina nani lakini mmoja wa maafisa hao ambae hakufahamika jina lake
na ndiye aliyelalamikiwa mwenye matege ya mikono kama baunsa alimjibu
mwenyekiti kuwa yeye hana sababu ya kujitambulisha
wala kutoa kitambulisho anatakiwa kupanda gari watafahamiana huko wanakokwenda.
Hali hiyo ilianza kukusanya umati wa watu ambapo kiukweli
kitendo cha maafisa hao kutotumia maarifa na akili kutimiza majukumu yao
kingeweza kusababisha maafa kwani wananchi wengi walijua ni majambazi wamekuja
kumteka mwenyekiti hao hivyo wananchi walishajipanga kwa mapambano na tayari
vijan waliashaasha kuchukua silaha za jadi ili kuwakabili watu hao .
Hata hivyo wakati wananchi wakitafakari juu ya watu hao walikuwa wamegoma
kujitambulisha wala kuonesha vitambulisho awari afisa huyo mwenye matege
mikononi alimpiga mwenyekiti huyo kibao cha uso hadi miwani kumdondoka huku
akimvutia kwenye gari na kufanikiwa kumingiza ndani hapo ndipo
walipojitambulisha kama wao ni maafisa wa Takukuru lakini hawakuonesha vitambulisho.
Kabla ya gari hiyo kuondoka wananchi mbali mbali
waliokuwa wamefika ofisini pale kupata huduma waliwahoji kwa umakini huku watu
maafisa na kuwabana kwa nini wanampiga mwenyekiti huyo ambae alikuwa anabishana
nao kimaswali ya msingi ya kutaka wajitambulishe tu basi angeweza kutii, ndipo
maafisa hao walipojibu kuwa wao wametumwa kumkamata na kumpiga na mkuu wao
ambae ni Kamanda wa TAKUKURU Kinondoni kisha wakawasha gari na kuondoka kwa
mwendo wa kasi ya ajabu.
Kimsingi tukio hilo liliwashtua watu wengi ambapo kama si
rehema za mungu huwenda lingeweza kuleta maafa kitendo cha maafisa hao
kushindwa kutoa vitambulisho mapema na kushindwa kujitambulisha halikuwa jema
kwani katika eneo hilo kuna vita inaendelea kati mgogoro wa ardhi kati ya
matajiri na wananchi hivyo wananchi wengi walidhani kuwa watu hao ni watekaji
kwa jinsi pia walivyokuwa wanatumia ubabe na nguvu nyingi bila hakiri.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambae pia ni mtoto wa Waziri
Mkuu mstaafu aliyejitambusha kwa jina la
Liberty Msuya alisema “ Ndugu mwandisahi naweza kusema Mungu kasaidia unauona umati huu
watu zaidi ya 800 wamekusanyika nusu saa tu na walikuja hapa kwa baada ya
kusikia mwenyekiti wao katekwa na watu wasiofahamika sasa je unadhani
wangewakuta hapa nini kingetoa unadhani wangetoka salama wangewezaje kupambana
na nguvu hii ya uma? “ Alisema mtoto huyo wa waziri na kushauri kuna haja ya
watumishi wa namna hiyo kupewa elimu sahihi jinsi ya kukamata watuhumiwa wao
kutoa kitambulisha ni usalama wa kwanza kwao.
Hata hivyo baada ya wananchi kusikia mwenyekiti wao ameshaondoka
umati huo uliekea kituo cha polisi Wazo na kuzajana pale kwa ajiri ya
kumuulizia kiongozi wao ambapo maafisa wa ngazi za jauu wa kituo hicho
walifanyakazi ya ziada kuwaeleza kama kiongozi wao hayupo na wala hawana
taarifa za kukamatwa kwao, licha maafisa wa Polisi kuwauliza kama waliokuja
kuwamata walitoa vitambulisho? Lakini ilionekana hawakutoa huku Polisi nao
wakiingia hofu huenda mwenyekiti huyo alikuwa ametekwa na wahuni na kuwataka
waende kituo cha Polisi Oysterbay.
Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mtaa ambao hawakuwepo
eneo la tukio ambapo walimpigia RPC Kinondoni simu na kumueleza tukio hilo
ambapo alisema kama watu hao walikuwa wametaja kama wao ni Takukuru labda waende ofisi zao ndipo walipokwenda na
kumkuta akiwa chumbani akihojiwa na maafisa wa ngazi za juu wa Takukuru
Kinondoni.
Hata hivyo wananchi mbalimbali wakazi wa kata hiyo ya
Wazo wamelani vikali tukio la kudhalilishwa kwa kupigwa mwenyekiti wao mbele ya
watu kuhusu suala ya kukamatwa wanasema hawaingilii kwa kama kiongozi wao
alikamtwa kwa ajiri ya uchunguzi wa hilo hawapingi kwa vile chombo hicho kina
haki na mamlaka ya kufanya hivyo, ila tu kitendo cha kushindwa kuonesha
vitambulisho vyao na kumpiga ndicho kimepelekea wao kushikwa na tahamaki kwani
awali walijua ametekwa na watu huenda waliokuwa wametumwa na wenye mashamba ili
wakamdhuru.
Hali hiyo kiukweli ingeweza kuleta maafa makubwa kwa
jinsi staili waliyoitumia kumkamata kibabe mwenyekiti huyo kama kundi lile la
watu wangekuwepo tungeweza kuwakosa
maafisa wetu hao wa Takukuru ambao ni muhimu kwa taifa letu hasa kipindi hichi
cha kutumbua majibu, hivyo ni heri maafisa hao
baadhi wa Takukuru Kinondoni wakaendelea kupewa elimu au kurudi kwenye
mafunzo upya kwa ajiri ya kupata maadili ya kufanya kazi kwa kuzingatia maadili
ili kuepuka mdhara kwani hasira waliyokuwa nayo wananchi wa Wazo hakika
wangeweza hata kuwachoma moto maafisa hao
kwani wasingeweza kuona mwenyekiti wao akipigwa mbele yao.
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda Mkuu
wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni ili azungumzie sababu za kumatwa kwa Mwenyekiti
huyo ambae alikamatwa akiwa kwenye kikao ofisini jana tarehe 18 saa kumi jioni na kufikisha
makao makuu ya Takukuru ziligonga mwamba mara baada ya simu yake kuita bila
kupokelewa hadi habari hii inakwenda mitamboni.
Hata hivyo kitendo cha afisa takukuru huyo kushindwa
kutumia akili na maarifa kwenye utendaji
wa kazi yake watu huku akisema katumwa na kamanda mkuu wa Takukuru Mkoa wa
Kinondoni ampige mwenyekiti huyo kimetafriwa kama ni kukichafua chombo hicho
Mkoa wa Kinondoni kwani haiaminiki kama kweli Kamanda huyo anaweza kumtuma
afisa wake ampige mtu asiyekuwa na ubishi, bali itakuwa ni utovu wake wa
nidhamu.
Subscribe to:
Posts (Atom)