mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyakasangwe Peter Bilebela aliyekaa karibu na Mh Paul Makonda ambae anazungumza na wakazi wa eneo hilo.
Huyu ndiye mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyakasangwe Peter Bilebela akiwa kwenye moja ya majukumu yake na wananchi hivi karibuni
Na Mwandisahi wa Maskanibongo gazeti
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua hali ya utekelezaji wa agizo la Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni na Waziri wa Ardhi Mheshiwa Lukuvi la kutaka maeneo yote
yenye migogoro yapimwe ili kupata ufumbuzi wa mizozo hiyo inayoendelea Jijini ,
lakini kwa Kata ya Wazo hali imekuwa tofauti baada ya zoezi hilo kuonekana kuwa
na dalili zote za kuvurugwa ili likwame.
Habari zaidi zilieleza kuwa mgogoro huo wa Wazo mtaa wa Nyakasangwe
umekuwa na mitihani mingi hasa kwa viongozi wa Serikali ya Mtaa huo unaongozwa
na Mwenyekiti wake Peter Bilebela “Mchungaji”
Kwani mgogoro huo unaohusisha watu wenye fedha nyingi ambao hujiita wenye
mashamba na wananchi ambao wanaoitwa wavamizi huku nyuma yake kukiwa na
masirahi ya baadhi ya vigogo wazito.
Tukio la jana la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Mtaa huo
Peter Bilebela na watu waliofika ofisini kwake huku mwenyekiti huyo akiwa
kwenye majukumu yake ya kikao na wajumbe huku watu hao wakijitambulisha kama
wao ni maafisa TAKUKURU bila kuonesha vitambulisho.
Akiongea kwa masikitiko makubwa Mwenyekiti mbele ya Kamanda Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni wakati
akihojiwa mara baada ya kufikishwa kwenye Ofisi za Takukuru zilizopo Magomeni
Mapipa Jijini Dar es Salaam alisema maafisa hao waliokuwa wametumwa kumkamata
walitumia ubabe mkubwa na nguvu nyingi kuliko hekima na ustaarabu kwa kumpiga
mbele ya watu.
Mwenyekiti huyo aliendelea kumueleza Mkuu huyo wa
Takukuru ambapo Maskanibongo ilifanikiwa kunasa mazungumzo hayo ambapo
mwenyekiti huyo alimueleza kamanda huyo kuwa mara baada ya vijana hao kufika
ofisini kwake walianza kumkamata mjumbe wake wa Serikali ya mtaa aliyefahamika
kwa jina la Mohamed Mangundungundu .
Baada ya kumkata mjumbe huyo aliyekuwa amekaa nje ya
ofisi kisha wakamfata Mwenyekiti ambae alikuwa kwenye kikao na kumtaka atoke
nje ili apande kwenye gari, lakini mwenyekiti huyo aliwaambia kwamba kuna nini
na wao ni akina nani lakini mmoja wa maafisa hao ambae hakufahamika jina lake
na ndiye aliyelalamikiwa mwenye matege ya mikono kama baunsa alimjibu
mwenyekiti kuwa yeye hana sababu ya kujitambulisha
wala kutoa kitambulisho anatakiwa kupanda gari watafahamiana huko wanakokwenda.
Hali hiyo ilianza kukusanya umati wa watu ambapo kiukweli
kitendo cha maafisa hao kutotumia maarifa na akili kutimiza majukumu yao
kingeweza kusababisha maafa kwani wananchi wengi walijua ni majambazi wamekuja
kumteka mwenyekiti hao hivyo wananchi walishajipanga kwa mapambano na tayari
vijan waliashaasha kuchukua silaha za jadi ili kuwakabili watu hao .
Hata hivyo wakati wananchi wakitafakari juu ya watu hao walikuwa wamegoma
kujitambulisha wala kuonesha vitambulisho awari afisa huyo mwenye matege
mikononi alimpiga mwenyekiti huyo kibao cha uso hadi miwani kumdondoka huku
akimvutia kwenye gari na kufanikiwa kumingiza ndani hapo ndipo
walipojitambulisha kama wao ni maafisa wa Takukuru lakini hawakuonesha vitambulisho.
Kabla ya gari hiyo kuondoka wananchi mbali mbali
waliokuwa wamefika ofisini pale kupata huduma waliwahoji kwa umakini huku watu
maafisa na kuwabana kwa nini wanampiga mwenyekiti huyo ambae alikuwa anabishana
nao kimaswali ya msingi ya kutaka wajitambulishe tu basi angeweza kutii, ndipo
maafisa hao walipojibu kuwa wao wametumwa kumkamata na kumpiga na mkuu wao
ambae ni Kamanda wa TAKUKURU Kinondoni kisha wakawasha gari na kuondoka kwa
mwendo wa kasi ya ajabu.
Kimsingi tukio hilo liliwashtua watu wengi ambapo kama si
rehema za mungu huwenda lingeweza kuleta maafa kitendo cha maafisa hao
kushindwa kutoa vitambulisho mapema na kushindwa kujitambulisha halikuwa jema
kwani katika eneo hilo kuna vita inaendelea kati mgogoro wa ardhi kati ya
matajiri na wananchi hivyo wananchi wengi walidhani kuwa watu hao ni watekaji
kwa jinsi pia walivyokuwa wanatumia ubabe na nguvu nyingi bila hakiri.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambae pia ni mtoto wa Waziri
Mkuu mstaafu aliyejitambusha kwa jina la
Liberty Msuya alisema “ Ndugu mwandisahi naweza kusema Mungu kasaidia unauona umati huu
watu zaidi ya 800 wamekusanyika nusu saa tu na walikuja hapa kwa baada ya
kusikia mwenyekiti wao katekwa na watu wasiofahamika sasa je unadhani
wangewakuta hapa nini kingetoa unadhani wangetoka salama wangewezaje kupambana
na nguvu hii ya uma? “ Alisema mtoto huyo wa waziri na kushauri kuna haja ya
watumishi wa namna hiyo kupewa elimu sahihi jinsi ya kukamata watuhumiwa wao
kutoa kitambulisha ni usalama wa kwanza kwao.
Hata hivyo baada ya wananchi kusikia mwenyekiti wao ameshaondoka
umati huo uliekea kituo cha polisi Wazo na kuzajana pale kwa ajiri ya
kumuulizia kiongozi wao ambapo maafisa wa ngazi za jauu wa kituo hicho
walifanyakazi ya ziada kuwaeleza kama kiongozi wao hayupo na wala hawana
taarifa za kukamatwa kwao, licha maafisa wa Polisi kuwauliza kama waliokuja
kuwamata walitoa vitambulisho? Lakini ilionekana hawakutoa huku Polisi nao
wakiingia hofu huenda mwenyekiti huyo alikuwa ametekwa na wahuni na kuwataka
waende kituo cha Polisi Oysterbay.
Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mtaa ambao hawakuwepo
eneo la tukio ambapo walimpigia RPC Kinondoni simu na kumueleza tukio hilo
ambapo alisema kama watu hao walikuwa wametaja kama wao ni Takukuru labda waende ofisi zao ndipo walipokwenda na
kumkuta akiwa chumbani akihojiwa na maafisa wa ngazi za juu wa Takukuru
Kinondoni.
Hata hivyo wananchi mbalimbali wakazi wa kata hiyo ya
Wazo wamelani vikali tukio la kudhalilishwa kwa kupigwa mwenyekiti wao mbele ya
watu kuhusu suala ya kukamatwa wanasema hawaingilii kwa kama kiongozi wao
alikamtwa kwa ajiri ya uchunguzi wa hilo hawapingi kwa vile chombo hicho kina
haki na mamlaka ya kufanya hivyo, ila tu kitendo cha kushindwa kuonesha
vitambulisho vyao na kumpiga ndicho kimepelekea wao kushikwa na tahamaki kwani
awali walijua ametekwa na watu huenda waliokuwa wametumwa na wenye mashamba ili
wakamdhuru.
Hali hiyo kiukweli ingeweza kuleta maafa makubwa kwa
jinsi staili waliyoitumia kumkamata kibabe mwenyekiti huyo kama kundi lile la
watu wangekuwepo tungeweza kuwakosa
maafisa wetu hao wa Takukuru ambao ni muhimu kwa taifa letu hasa kipindi hichi
cha kutumbua majibu, hivyo ni heri maafisa hao
baadhi wa Takukuru Kinondoni wakaendelea kupewa elimu au kurudi kwenye
mafunzo upya kwa ajiri ya kupata maadili ya kufanya kazi kwa kuzingatia maadili
ili kuepuka mdhara kwani hasira waliyokuwa nayo wananchi wa Wazo hakika
wangeweza hata kuwachoma moto maafisa hao
kwani wasingeweza kuona mwenyekiti wao akipigwa mbele yao.
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda Mkuu
wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni ili azungumzie sababu za kumatwa kwa Mwenyekiti
huyo ambae alikamatwa akiwa kwenye kikao ofisini jana tarehe 18 saa kumi jioni na kufikisha
makao makuu ya Takukuru ziligonga mwamba mara baada ya simu yake kuita bila
kupokelewa hadi habari hii inakwenda mitamboni.
Hata hivyo kitendo cha afisa takukuru huyo kushindwa
kutumia akili na maarifa kwenye utendaji
wa kazi yake watu huku akisema katumwa na kamanda mkuu wa Takukuru Mkoa wa
Kinondoni ampige mwenyekiti huyo kimetafriwa kama ni kukichafua chombo hicho
Mkoa wa Kinondoni kwani haiaminiki kama kweli Kamanda huyo anaweza kumtuma
afisa wake ampige mtu asiyekuwa na ubishi, bali itakuwa ni utovu wake wa
nidhamu.
No comments:
Post a Comment