Mmoja wa wazee wa Kanisa la Hossana akiwa kwenye hisia kali ya maombi kwa Mungu
Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Hosana Mch Mzola
Waziri wa Ardhi Mh Lukuvu kwa sasa yupo chini ya maombi hayo ili afanye maamuzi sahihi.
Mchungaji Amos Mbena Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Holness Mision lililopo Kimara lakini mchungaji huyo amekuwa akiguswa sana na mgogoro huo hivyo nae ameungana kuongeza nguvu ya maombi ili viongozi hao wasikie kilio cha wananchi hao.
Shkhe Sharif Khamis kijana mwenye nguvu ya ajabu kwenye maombi nae ameungana na watumishi hao mbalimbali na wananchi kwenye maombi ya kumaliza mgogoro wa ardhi wa eneo hilo.
Wakina mama na watoto ambao kwa sasa wanaishi mazingira magumu baada ya nyumba zao kubomolewa na polisi kwa shinikizo la mafisadi, wakimlilia Mungu wao.
Na Mwandishi wa Maskanibongo Gazeti
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda, Rais Magufuli na waziri wa Ardhi Mheshimiwa Lukuvu wapo chini ya maombi makali ya siku 40.
Wakazi wa Kata ya Wazo kwenye Mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa wakishirikiana na mashekh na wachungaji wameanzisha maombi hayo maalum kwa ajiri ya Mungu kuwafungua viongozi hao ili wamalize mgogoro huo ndani yake wenye harufu ya rushwa na ufisadi huku maafisa Ardhi na watu wa Mipango Miji Manspaa ya Kinondoni wakitajwa kuhusika.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wachungaji wa makanisa yaliyopo Mitaa ya Nyakasangwe na Nyakalekwa walisema" Tupo kwenye maombo haya ili Mungu awafungue viongozi wetu kwa vile wao ndiyo wenye mamlaka ya mwisho wamalize hili jambao kwani tunaamini Tanzania kwa sasa imepata rais ambae watanzania walikuwa wakimuhitaji hivyo tumeona ni vyema tukamlilia Mungu azidi kumfungua zaidi na kuona hata mgogoro uliopo kwenye mtaa wetu " Alisema Mchungaji Mzola
Hata hivyo wachungaji hao waliendelea kusema kuwa kazi kubwa aliyoifanya Mheshimiwa Paul Makonda ni kubwa sana na hakika sasa mahara alipofikia anahitaji nguvu ya maamuzi ya Mheshimiwa Waziri Lukuvi na Rais kwa vile mtandao alioukuta mheshimiwa Makonda kwenye mgogoro wetu ni mkubwa na inaelezwa ndani yake kuna baadhi ya vigogo wa Ardhi Manspaa.
Wakazi hao waliendelea kusema Mheshimiwa Makonda amediliki kuhatarisha maisha yake kwa kupigania haki ya wananchi licha ya kwamba amekuwa akikutana na vikwazo kutokana na kuzungukwa na watu ambao hawapo upande wake bali wakiwa upande wa mafisadi hivyo sasa ni zamu ya Waziri kumpa meno ya yenye makali kumaliza mgogoro huo kwa kutoa maamuzi yatakayoondoa kabila mgogoro huo.
Mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa inaongozwa na Mwenyekiti wake Peter Bilebela ambae amekuwa kipenzi cha wakazi hao kutokana na utendaji wake wa hali na kuogpa rushwa kama ukoma, hali hiyo imepelekea kuchukiwa na upande wa pili wa mafisaidi kiasi cha kumtengenezea zengwe kila kukicha kwa kutumia pesa waliyokuwa nayo
No comments:
Post a Comment