TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Wednesday, January 16, 2013

MADENT WALIOPIGA PICHA ZA UCHI MBARONI!

Msichana aliyeitwa Elizabeth Patrick (Eliza) Ambae amekamatwa na jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni kwa tuhuma za kumtishia maisha mwandishi wa blog hii.
Msichana Lukia Laus ambae bado anatafutwa na jeshi hilo kwa kosa kama hilo la Eliza.

OCD Mtafungwa atoa tamko.

Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni linamshikilia mmoja wa wakina dada waliopiga picha za uchi kwa tuhuma za kumdhalilisha mwandishi wa habari wa blog hii pamoja DTV bwana Livingstone Mkoi kwa kumtolea lugha za matusi kwa njia ya mtandao ya simu.
Habari za uhakika zilizothibitishwa na mwandishi huyo zilisema kuwa”Ni kweli jeshi la polisi limemkamata mmoja wa wasichana walipoiga picha za uchi ambazo zililipotiwa na blog hii hivi karibuni kwa tuhuma za kunitukana na kunitishia Maisha” Alisema Mkoi
Aidha akizungumzia zaidi tukio hilo mwandishi huyo alisema kuwa baada ya kupatikana picha hizo za aibu ambazo hazifai hata kuziona alimpigia simu mmoja wa wasichana hao aliyefahamika kwa jina la Editha      Adolf a.k.a Eliza kwa lengo la kubalansi stori na baada ya kumshushia tuhuma hizo aliambulia matusi makali pamoja na vitisho vya kutekwa harafu afanyiwe kitu mbaya ndipo alipojisalimisha polisi na kupewa taarifa OB/903/2013 KUTOA LUGHA YA MATUSI KUPITIA MTANDAO.
Hata hivyo katika tukio hilo watuhumiwa ni wote waliopiga picha hizo chafu kwa vile pia namba za simu zilizotumika kututisha maisha ya mwandishi huyo kwa sasa ziko chini ya uchunguzi wa kina na wana usalama ili itakapofia hatua wahusikia wafikishwe mahakamani.
Katika tukio hilo  Editha      Adolf a.k.a Eliza ndiye aliyekuwa wa kwanza kukamtwa ambapo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Summit iliyopo Kinondoni Mkwajuni ambapo mtuhumiwa namba mbili aliyefahamika kwa jina la Lukia Laus bado anatafutwa na jeshi hilo ambapo atakapokamatwa ataunganishwa kwenye kesi hiyo.
Aidha akizungumza na mwandishi wetu Mkuu wa Kituo cha Polisi Kinondoni OCD.Mtafungwa alisema kisheria ni kosa kumtishia mtu maisha pamoja na kutukana hayo yote ni makosa hivyo ni lazima sheria ichukuwe mkondo wake.
Hata hivyo katika hatua nyingine wasichana hao wamekuwa na tabia ya kujifanya wanafunzi ili wajipatie wanaume wa kishua ambao mara nyingi hupenda wanafunzi, Lakini uchunguzi wa kina uliofanywa na Xdeejayz umebaini wasichana hao hawasomi popote isipokuwa wanajishughulisha na biashara ya kuuza miili yao.
Wakiongea na Xdeejayz kwa nyakati tofauti wananchi waishio maeneo ya Kinondoni Mkwajuni walisema”Jamani hao mabinti hawasomi popote waache kujipakazia hawa wanaishi nyumba ya wageni iliyopo hapa hapa Mkwajuni inaitwa Summit au Kirumo pamoja na Kipepeo, hata hivyo tunaliomba jeshi la polis kuja kuwakama wakina dada hawa kwani watoto wetu wako hatarini kujifunza tabia mbaya wanayoifanya maeneo haya ya kuuza miili yao” Alisema mkazi wa maeneo hayo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Ismail.
Aidha katika hatua nyingine wanawake hao ambao inadaiwa wamebadisha majina yao halisi ili kuwaibia wanaume.

No comments:

Post a Comment