Kamanda wa polisi Kanda ya Dar es Salaam Bwana Suleiman Kova.
Kamanda wa polis kanda ya Kinondoni Charles Kenyela.
Kikao chachukuwa siku nzima
kuweka sawa tofauti zao.
Na Mwandishi Wetu
Kamanda wa polisi kanda maalum Jijini Dar es Salaam Bw Suleiman Kova kushirikiana na maofisa wa ngazi
ya juu toka makao makuu ya polisi wamewaweka kiti moto makamanda wa mikoa ya
kiposi Temeke kamanda Engelbert Kiondo RPC Temeke na Charles Kenyela RPC
Kinondoni kufuatia kutofautiana kuhusiana ishu ya makahaba.
Habari za uhakika
zilizonaswa na Xdeejayz kushirikiana chanzo chetu toka polisi central zilisema
Kamanda kova alifikia uamuzi wa kufanya kikao hicho cha haraka mapema wiki kwa
kuwaita makamanda hao kufika ofisini kwake ili kuzungumzia sakata hilo.
Habari zaidi juu ya
kutofautia kwa makanda hao zilisambaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari
mapema wiki zikimnukuu kamanda wa polisi Temeke kumshutumu kamanda wa polisi
Kinondoni kuwa hajui sheria kwa kuendelesha uparesheni ya kuwakamata
machangudoa na kuwapeleka mahakamani wakati hakuna sheria inataka wanawake hao
wafikishwe mahakamani kwa tuhuma hizo badala yake Kenyela alitakiwa kuwapa
elimu kuacha kufanya hivyo kwani kuna athari nyingi ambazo zinaweza kuwakuta.
Kufuta kauli hiyo Kamanda
Kenyela nayeye kupitia vyombo vya habari alieleza kusikitishwa sana na kauli ya
kamanda Kiondo kuingilia utendaji wake wa kazi na kusema kuwa amedhalilishwa
sana na isitoshe yeye ana simamia mkoa mwingine na labda kama angeona kuna
sehemu kuna mapungufu basi angempigis simu na kumueleza kuliko kuzungumzia ishu
hiyo kwenye vya habari.
Hata hivyo kwa mujibu wa
chanzo chetu haikufahamika hitimisho la kikao hicho kwa utofauti huo.
No comments:
Post a Comment