Tanzania ni nchi ambayo mfumo wake wa kiuchumi na
kisiasa ,unawafanya watu wengi kuwa na mkanganyiko .Hii ni kutokana na
kutokuwepo kwa viashiria vya moja kwa moja kuwa Tanzania ni nchi ya kijamaa au
kibepari.
Utata huo
umewafanya wasomi na wanafalsafa mashuhuri
nchini kuwa na mawazo tofauti.Hali hiyo imepelekea hata vijana katika
shule kushindwa kujua ukweli yakinifu kuwa Tanzania ipo katika mfumo gani wa
kiuchumi na kisiasa.Tutatumia fursa hii kuonesha mifumo yote miwli ili kuondoa utata unaozidi kuteka nyoyo za
wasomi,wananaharakati na wachambuzi wa masuala ya kisiasa .suala hili limeleta
utata hata katika katiba ya jamhuri ya muunganoi
wa Tanzania ambapo baadhi ya
watanzania wamejaribu kutoa maoni yao kuwa neno ujamaa lisijitokeze tena katika katiba mpya
kwa kigezo kuwa hatuko katika ujamaa tena.Tupo katika mfumo wa
kibepari.Miongoni mwa vifungu vinavyotaja
ujamaa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni
ibara 3(1) “Jamhuri ya Muungano ni nchi
ya kidemokrasia na y a kijamaa, isiyokuwa na dini ,yenye kufuata mfumo wa vyama
vingi vya siasa”
Suala hili
limeleta utata wa hali ya juu kutokana
na hoja kuwa Ujamaa haupo.Kupitia safu hii tunaona ni bora kujadili mifumo hiyo
ili kuondoa utata kitaaluma.Kwa mujibu wa kitabu cha Mwl Nyerere (essay on
socialism) (pg 1) anaelezea ujamma kwa kusema
“Ujamaa ni mtazamo wa kifikra .Katika
mtazamo huo wa wajamaa ni kuwa
mfumo wa kisiasa upo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wananchi wanahudumiwa vyema
katika Nyanja zote za kijamii” lakini wataalam wengine wazamivu katika taaluma
ya falsafa za kijamaa kama Carl Marx yeye ana sema “Katika kitabu chake cha Communist
Manifestal “Ujamma ni mfumo wa kiuchumi
, kisiasa na kijamii wenye lengo la
kutatua matatizo ya wafanyakazi na kuondoa unyonyaji uliokithiri “
Kwa mujibu
wa mitazamo hiyo tunaweza kuona kuwa
Ujamaa ni mfumo wa maisha uliojengwa ili
kukidhi mahitaji ya msingi ya wananchi.Na mfumo huo umejikita kisiasa zaidi
katika kuhakikisha iinatatua matatizo
yote sugu ya kiuchumi na kisiasa.
Mfumo huo wa
kijamaa ulianzishwa mara baada ya kutokea kwa athari ya mapinduzi ya viwanda
(Industrial Revolution) (1750s) Mara baada ya mapinduzi ya viwanda (1750s)
katika nchi ya Uingereza , baadae Ujerumani,Ufaransa na Marekani
yalijitokeza matatizo ya msingi
yaliyowakabili wafanyakazi wa viwandani katika nchi hizo za Ulaya na Amerika
.Matitatizo hayo ndio yalikuwa chachu ya msingi ya wanafalsafa mashuhuri
duniani kukaa na kutafakari njia mbadala itakayotatua matatizo hayo ya
wafanyakazi.
Hapo ndipo
wakina Robert Owen ,Simon Decomte na
Charles Fourier walipoanzisha
Ujamaa (Socialism). Watu hawa walitafuta neno la Socialism ili kupata
wafuasi wengi watakaokuwa na kiu ya kutaka usawa.Hatua hii ya kwanza ilipewa
jina la Utopian Socialism (Ujamaa
ujenzi)1750s-1850s.
Katika hatua
hii ya awali wajamaa wote walijiwekea misingi yao .Misingi hiyo ilikuwa ni
kuhubiri ujamaa kwa njia ya amani bila kuleta vurugu .Pia kudai mabadiliko ya
kisiasa katika katika ubepari kwenda katika ujamaa kwa njia ya amani.Kuanzishwa
kwa mfumo wa Serikali kutoa huduma
muhimu kwa raia, kuondoa matabaka kati ya walionacho na wasionacho na kuweka
rasilimali zote mikononi mwa raia wote si kwa watu wachache, kubinafsishwa
ardhi kubwa na viwanda.
Baada ya
hatua hiyo ya wajamaa ujenzi ilifuata hatua nyingine ya kijamaa iliyojulikana
kama Scientfic Socialism ujamaa wa
kisayansi(1860s-1920s).Ujamaa huo uliongozwa na Carl Marx na Fredrick Engel ambao walikuwa na mtazamo unaofanana.Wao
walikuja na vitabu vyao Das Capital na
Communist Manifestal vitabu ambavyo
vilikuwa vimesheheni nadharia muhimu za ujamaa.Vitabu hivyo vilitapakaa dunia
nzima vikitoa mwelekeo wa watu wa tabaka la chini wafanyakazi kupata nafuu
kiuchumi kupitia siasa nzito zilizokuwa zimejadiliwa na wanafalsafa hao.
Misingi
ifuatayo ndio iliyikuwa imejikita katika hatua hii ya ujamaa .Kuhakikisha chama
cha wafanyakazi kinaundwa na kutatua matatizo yao.Kupiga vita unyanyonyaji
uliokuwa ukifanywa na mabepari.Kupunguza masaa ya kufanya kazi kwa wafanyakazi
wa viwandani kutoka msaa 12 hadi masaa 8.Kuwang’oa mabepari kwa kutumia maandamano na mapinduzi kama njia ya
Diplomasia itashindikana.Kuhakikisha kuwa bara la Afrika na Ulimwengu wote watu
wote wanakuwa huru chini ya mfumo wa Ujamaa.Kupiga vita kodi za uzalishaji.Pia
walitoa changamoto juu ya kutolewa kwa sadaka katika nyumba za ibada ambapo
Carl Marx alitoa wito kwa kusema hakuna haja ya kutoa sadaka kwa ajili ya
Mungu maana kutoa sadaka ni kudhihirisha
kwamba Mungu mnaemwabudu ni dhaifu hawezi kuishi kwa kujitegemea yeye mwenyewe
hadi mtoe rushwa aweze kuishi.Pia Carl Marx alishambulia imani za kidini kwa
kiasi kikubwa ili kudhoofisha ubepari
ambao ulionekana kuwa na uhusiano wa karibu mno na viongozi wa kiimani.
Katika
hatua hii ujamaa ulipiga hatua kubwa mno katika kuhakikisha kuwa unatapakaa kila mahali.Hali hiyo ilisaidia
kwa mapinduzi ya kijamaa nchini Russia
1719 baada ya Lenin kutumia mbinu za waandishi
na wana falsafa mashuhuri katika
kuhakikisha anafanikisha mapinduzi .Pia
chama cha wafanyakazi kilianzishwa International
Labour Organization kikiwa na
madhumuni ya kuhakikisha kuwa
wafanyakazi wote duniani wanapata haki za msingi ikiwa ni pamoja na
kuboreshewa mishahara yao na hali yao ya utendaji kazi pamoja na kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa na bima na
kulipwa pensheni.
Ujamaa
ulienea mataifa kama Argentina, China
,Cuba na Afrika .Kutokana na ukweli kuwa wananchi walikuwa wameathirika kwa
kiasi kikubwa na mfumo wa ubepari.
Nationalism Socialism (1945s-1990s).Huu
ni ujamaa ulianzishwa na kushika hatamu kwa kiasi kikubwa mara baada ya vita
vya pili vya dunia 1945s.Nationalism Socialism
(Ujamaa wa kuleta uhuru ) Nchi nyingi zilizokuwa zinatawaliwa na
mabeberu ziliamua kujiunga na mfumo huo
wa ujamaa ili ziweze kupata msaada kwa nchi kama Urusi na Cuba ili wafanikishe
azma yao ya uhuru nchi hizo ni kama
Kenya ,Ghana na Uganda.Nchi ambazo zilihitaji msaada mkubwa kwa mataifa pingani
kwa wakoloni ili wapate msaada wa kujikomboa.Lakini nchi ya Tanganyika kwa
wakati ule iliamua kujiunga kwa dhati
katika ujamaa kwa kukubali sera na utashi wa ujamaa hususani katika
kipindi cha TANU na Mwl Nyerere akiwa kiongozi .
Mwl Nyerere
hakusita kubeba dhamana ya ujamaa
kwa kuangalia makusudio yake ya msingi na mifumo yote ya aina tatu ya kiuchumi
ambayo kila taifa ni lazima liifuate
mifumo hiyo ni ;
a)
Commanding economy
(Uchumi Shurutishi) Huu ni mfumo ambao nchi inaongozwa kwa rasilimali
zote za taifa kuwa chini ya Serikali .Na
shughuli za huduma za kijamii zinatolewa
na Serikali mfano huduma za Afya,elimu, ujenzi wa miundo
mbinu .Umoja wa mataifa ,Mashirika na makampuni
kumilikiwa na Serikali na kutokuwepo kwa wawekezaji binafsi .Hakuna
ushindani wa kibiashara
b)
Pure
Capitalism Economy (Uchumi wa Kibepari)Mfumo huu umejikita zaidi katika kutoa uhuru kwa
wawekezaji kuwekeza katika idara zote za
kiuchumi ikiwa pamoja na idara ya Elimu,Afya,na kilimo.Kazi kubwa ya serikali ni
kukusanya kodi kwa wawekezaji.Hapa kuna
ushindani mkubwa wa uzalishaji na uuzaji wa bidhaa,
c)
Mixed
Economy (Uchumi Ingiliani) Huu ni mfumo wa kiuchumi anbao umejikita zaidi katika kutaa 50% wawekezaji kuwekeza katika
shughuli za kiuchumi na 50% Serikali inamiliki mfumo mzima wa mahitaji ya msingi ya raia na kuwatatulia
matatizo.
Mifumo hiyo ya kiuchumi ambayo ni ya aina tatu
inakwenda sambamba na aina tatu muhimu za bajeti (budget) ambazo zinashabihiana
sana kwa tabia .Nchi yeyote duniani ni
lazima iwe na bajeti ya aina hizi.
a)
Deficit
Budget (Bajeti Pungufu) Katika ukusanyaji wa mapato taifa linakusanya fedha kidogo ukilinganisha na mahitaji
yanayotakiwa.Mataifa mengi yenye bajeti ya aina hii urandana sana na mfumo wa commanding economy
(Uchumi shurutishi)
b)
Standard
Budget(Bajeti linganifu) Hii ni aina ya
bajeti ambayo makadirio ya fedha ya
matumizi na fedha iliyokusanywa vina
uhusiano wa karibu sana .Mataifa yenye mfumo huu wa bajeti una randana
sana na mfumo wa kiuchumi wa
mixed economy (Uchumi Linganishi)
c)
Surplus
Budget (Bajeti ya ziada)Huu ni mfumo ambao makadirio ya matumizi ya fedha za Serikali
ambapo fedha za Serikali zilizokusanywa ni nyingi zaidi kuliko matumizi
ya fedha zilizopo.Mfumo huu unajikita zaidi
katika mfumo wa uchumi wa Pure Capitalism economy (Uchumi wa kibepari)
Hivyo Mwl Nyerere kwa kuzingatia mifumo hiyo alikuwa na sababu ya kujiunga na
ujamaa ili kukidhi mahitaji muhimu ya
watanzania.Pia Mwl Nyerere aliona mifano
wa mataifa ambayo yalichukua
mfumo wa ujamaa na kupiga hatua kubwa kimaendeleo kwa wakati ule.Mataifa kama
Russia ,Argentina na Cuba .Mwandishi mashuhuri
wa vitabu vya historia na mwanafalsafa
I,Chekharin (The state and social system in USSR (Pg 5) anasema “Ujamaa
ni mfumo wa kimapinduzi uliopelekea kuondoshwa
kwa mfumo wa ubinafsi katika kumiliki rasilimali za umma,pia ndio umekuwa mwisho wa unyonyaji kwa
watu wa tabaka la chini pia umoja wa
kitaifa umejengwa”
Hali hii ilimpelekea Mwl Nyerere kuunda Azimio la
Arusha mwaka 1967 lilikuwa limebeba
taswira ya ujamaa.Kwa kuzingatia vya kijamaa
Azimio la Arusha liliainisha kwamba binadamu wote ni sawa kwamba kila mtu anastahili heshima bila kujali ana kipato au hana kipato.Kila
raia alitambulika kuwa ni sehemu
na mahali katika Tanzania pia kila mtu alikuwa na haki ya kupata
hifadhi.Katika hatua hii Tanzania ilianzisha vijiji vya ujamaa na kujitegemea lengo na madhumuni ilikuwa ni kuhakikisha kuwa ardhi inatumika kwa maslahi ya
watanzania.
Katika kipindi hiki cha Nationalism Socialism (Ujamaa uliojikita
katika Uhuru) kazi kubwa kwa nchi zote zilizosadiki ujamaa ilikuwa ni kuhakikisha mataifa yote ya Afrika
yanapata Uhuru.Tanzania ikiwa ni nchi mwanachama.Zama hizo zilianza 1945s-1990s
kipindi hiki kilikuwa cha ujamaa uliojikita katika kuleta uhuru barani Afrika.
Zama za Modern Socialism (Ujamaa wa kisasa ) 1990s-2015s Hiki ni
kipindi cha ujamaa uliopevuka au ujamaa wa kisasa ambao umeboresha maeneo yote
ambayo yalionekana kuwa pingamizi katika kuleta maendeleo mfano ni kuondoshwa
kwa vijiji vya ujamaa na kujitegemea ambavyo havina tija kwa sasa lakini mizizi ya
misingi ya ujamaa bado inaonekana ikiwa ni pamoja na kuwa na mfumo wa Serikali kutoa huduma kwa wananchi wake moja kwa
moja pia bado watu wanashirikiana kwenye
misiba na sherehe hata kama hawajaalikwa.Serikali
inatoa huduma zote muhimu katika nyanja
zote muhimu mfano ni Idara ya elimu na afya
kwa kuwa na shule za Serikali na Hospitali za Serikali..Mala baada ya kuangalia
mifumo na hatua muhimu za ujamaa ni vyema pia kuutazama mfumo wa kibepari ili
tuweze kujadili kwa kina Tanzania itakuwa katika mfumo upi wa kati ya ujamaa au
ubepari?.pia ni vyema kujua ubepari ni nini.
Ubepari
umetokana na neno Capitalism ambalo
mzizi wake ni neno Capital (mtaji) na
mfumo huo umeanza kushika hatamu Ulaya tangu karne ya 15th C Mfumo huu ulijikita zaidi
kwenye biashara .Pia muundo wake wa kijamii na kisiasa umejikita katika ubaguzi wa hali ya juu kati ya waliokuwa nacho ambao ndio wenye
maamuzi katika nchi,na wasiokuwa nacho ambao kazi yao ni kutekeleza majukumu kutoka kwa walionacho.Katika nchi
zinazoendeshwa kwa mfumo wa kibepari,mabepari wanalipa kodi kwa kiasi
kikubwa hali inayopelekea Serikali kuwa
na fedha za kutosha kuliko mahitaji
(surplus budget).Katika nfumo wa kjbepari hakuna mwingiliano wa kijamii kila
mtu ataishi kwa uwezo wake mwenyewe .Uwekezaji kwa watu binafsi katika nchi ni
asilmia 100% Serikali ni kukusanya kodi tu.Ubepari umejikita katika utabaka kwa
dhati mwanafalsafa wa kibepari Rugner Nurks anatoa falsafa iliyoungwa mkono
sana na mataifa ya kibepari inayosema
“Mtu tajiri ni lazima apewe elimu ya utajiri ili aulinde utajiri wake na
mtu maskini apewe elimu ya umaskini ili
ajue vema umaskini wake” na huo ndio utofauti mkubwa kati ya ubepari na ujamaa.
No comments:
Post a Comment