TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, December 3, 2012

WEMA SEPETU AWATIA AIBU BONGO MUVI KWENYE MSIBA WA SHARO MILIONE!

MSANII NYOTA WA FILAMU NCHINI NA MISS TANZANIA2006/07 WEMA SEPETU.
Watu wengi wapigwa na butwaa na kushindwa kuamini kilichotokea.
Na Livingstone Mkoi
Msanii nyota wa filamu nchini na aliyekuwa Miss Tanzania 2006/07 Wema Isack Sepetu katikati ya wiki iliyopita alilitia aibu kundi la bongo muvi kwa kufanya kitu cha kipekee kwenye msiba wa mwanamuziki na msanii wa komedi aliyefariki kwa ajali Mkoani Tanga Sharo Milionea.
Wema Sepetu ambae siku za hivi karibuni  amepumnzika skendo kwenye vyombo vya habari alipongezwa na watu kwa uungwana aliounonesha baada ya kutoa mchango mwingi kuliko msanii yeyote wa kundi hilo linalosifika kwa kashfa za ngono.
Habari zilizothibitishwa na mmoja wa ndugu wa marehemu ambae aligoma kutaja jina lake kwa madai kuwa yeye si msemaji wa familia alisema kuwa” Ni kweli wasanii mbalimbali walijitolea kwa kuja huku Tanga lakini Wema ndiye aliyetoa mchango mkubwa sana kwa kutoa shilingi laki mbili peke yake 200000/= huku wasanii wengine wakiishia kutia aibu”Alisema mtu.
Aidha ilidaiwa Wema ndiye aliyeonekana kuwa na uchungu wa dhati toka moyoni ambapo licha ya mchango huo pia alionekana kujishughulisha na kazi za kusaidia majukumu msibani hapo bila kujali ustaa wake aliokuwa nao.


No comments:

Post a Comment