TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, June 28, 2013

SHEKH SHARIF WA TANZANIA AZUSHA BALAA KUBWA NCHINI KONGO,WANAJESHI WAMUWEKA MTU KATI!

 Maelfu ya wananchi wa mji wa Bunjumbula wakiwa wamemzunguka Shekh Sharif mwenye bendera ya Tanzania kichwani.

 Maelfu ya wananchi wa mji wa Bunjumbula wakiwa wamemzunguka Shekh Sharif mwenye bendera ya Tanzania kichwani.
 Shekh Sharif mwenye kanzu akiwa mbele ya gari yake nchini Kongo hivi karibuni.
Na Livingstone Mkoi
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua kijana mwenye miujiza ya ajabu nchini Shekh Sharif Khamis hivi karibuni alizusha balaa katika nchini za Kongo, Burundi, Angora na Rwanda kiasi cha kusabaisha maafa  baada ya mihadhara yake kujaza maelfu ya watu hadi kushindwa kupumua.

Habari zaidi toka nchini hizo zilizonaswa na gazeti hili zilisema kijana huyo  amekuwa lulu kila anapotembelea kwenye nchi hizo kiasi cha wakuu wan chi hizo kupigwa na butwaa na kupelekea kumpa Mungu utukufu kwa kumjalia kijana huyo karama za hali ya juu.
 Wakiongea na gazeti hili baadhi ya wakazi wa miji ya Kigari,Bunjumbura na Luanda mji mkuu wa Angora walisema katika mihadhara yote aliyoiifanya kijana huyo watu mbalimbali wameponywa magonjwa yao kuna wakati hata waliokuwa wakiigusa kanzu yake tu walipona.

 Aidha katika miujiza mingine iliyofanywa na kijana huyo mwenye historia ya kutisha katika mashekh Sharif walipita ndani ya Tanzania ambapo kijana huyo alianza kuzungumza akiwa na umri wa mwaka mmoja baada ya kutoa kauri ya kumtaka babaake aache pombe mara moja na tangu kipindi hicho amekuwa akimtumikia mwenyezi mungu kwa kuwaombea watu dua kisha huwanyooshea kidole cha kati na hupona papo hapo.

 Mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Zaitun Bint Juma mkazi wa Kigari aliliambia gazeti hili kwa njia ya siku kuwa “ Katika historia ya Uislamu haijawahi kutokea kijana mwenye nguvu za kutisha kama Shekh Sharif Khalif kwani maelfu ya watu wamepona kwa dua zake” Alisema Zaitun

 Gazeti hili lilibahatika kuzungumza moja kwa moja na Shekh Sharif toka nchini Burundi muda mfupi akiwa amerejea toka nchini Kongo alisema “ Kwanza namshukuru mwenyezi mungu kwa kuwaponya watu wake kupitia sisi watumishi wake hivyo nimefanya mambo makubwa sana kwenye nchi zote nilizotembelea hakika mungu ni  mwema alinijaza kalama za ajabu ambapo maelfu ya watu wamepona kwenye matatizo yao” Alisema kijana huyo

Hata hivyo kijana huyo aliongeza kusema alipatwa na misukosuko ndani ya mpaka wa        Kongo na Burundi baada ya kuwekwa mtu kati na wanajeshi wan chi hizo na kutaka kujuwa kwa nini gari yake iliwekwa bendera ya Taifa la Tanzania yeye ni nani” Shekh alisema waliwekwa chini ya ulinzi masaa kadhaa kabla ya kuachiwa baada ya kuwaeleza kuwa yeye ni mtanzania na yuko kwa ajili ya kuitumia jamii.

No comments:

Post a Comment