TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, October 31, 2013

MATUKIO YA KUSHANGAZA YA MAZISHI YA BABA NA WEMA SEPETU, AZIKWA KWA HESHIMA ZOTE LICHA KUWA ALIHANGAIKA BILA MSAADA WOWOTE!!

SIKU 1 NA MASAA KADHAA ZIMEBAKI ILI KUFIKIA ILE SHOW ILIYOKUWA INASUBIRIWA KWA HAMU NA MAELFU YA WAKAZI WA MJI WA DODOMA NA VITONGOJI VYAKE, NI LIVE DJ DRUMMER NDANI YA CLUB MAISHA JUMAMOSI HII YA TEREHE 2/11/2013 NI BALAA KUBWA WABUNGE WA VYAMA VYOTE WAUNGANA KUPISHA SHOW HIYO!!!
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiuaga Mwili wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani, Mnazi mmoja Mjini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimpa pole Mjane wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu,Mama Miriam Sepetu,alipofika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja, kuuaga mwili wa Marehemu.
Ibada ya Kuuombea Mwili wa Marehemu Sepetu  ikiendelea kwenye Kanisa la Minara Miwili Zanzibar
Baadhi ya watoto wa marehemu Balozi Sepetu wakisikiliza neno la mungu
Wema Sepetu(Aliyesimama Kushoto) akiwa kanisani kwenye maombezi ya baba yake mzazi 



Baadhi ya Wananchi mbali mbali wakiwa katika sehemu maalum nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani, Mnazi mmoja Mjini Unguja,wakisubiri kuuaga mwili wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu, ambapo utazikwa Kijiji kwao Mbuzini Wilaya Magharibi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. akisalimiana na Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Mjini Zanzibar, Cosmas Amani Shayo,  alipowasili katika eneo la Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu, yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa na viongozi wengine akiwemo Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Mohamed Gharib Bilali,katika Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja jana
Jeneza la Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,likiwa limebebwa na Askari Polisi na kulifikisha katika kaburi lake yalipofanyika mazishi kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja jana.
 Padri wa Kanisa Katoliki la  Minara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo, akiuombea mwili wa marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja jana.
 
---------------------
Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohammed Shein, jana aliwaongoza mamia ya waombolezaji katika maziko ya mwanasiasa na mwanadiplomasia mkongwe Marehemu

Balozi Issack Abraham Sepetu (71),aliyezikwa katika Kijiji cha Mbuzini,Mkoa wa Kusini Unguja jana Alasiri.
 

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
 

Mapema mwili wa Balozi Sepetu uliagwa na waombolezaji wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi na viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya siasa shughuli ambayo ilifanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo eneo la Kikwajuni katika Manispaa ya Zanzibar kabla ya misa maalumu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph katika Mtaa wa Shangani.
 

Watoto wa marehemu, Amani,Mkusa, Wema na wengineo walikuwapo katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na Balozi mstaafu, Ali Abeid Karume, ambaye alisema marehemu ameacha pengo kubwa katika jamii kwani alikuwa kiongozi makini na mzalendo aliyelipenda taifa lake.
 

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Vuai Ali Vuai,alimwelezea marehemu kama mwasisi wa mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa kisiasa Zanzibar wakati juhudi hizo zilipoanza mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi visiwani mwaka 1995 kupitia kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Chifu Emeka Anyaoku.

HAYA NDIYO MAAJABU YA XTREME DEEJAYZ NDANI CLUB MAISHA DODOMA JUMAMOSI HII USINGOJE KUFIMULIA FIKA UONE LIVE DJ DRUMMER KWA MARA YA KWANZA MKOANI HUMO!!!

No comments:

Post a Comment