TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, November 16, 2015

HILI BALAA: WAKAZI JIJINI DAR WAMUOMBEA UKUU WA MKOA DC PAUL MAKONDA, WASEMA WANAIMANI NAE ATAENDANA NA KASI YA HAPA KAZI TU, NDUGU WA BAUNSA WALIOUAWA WASEMA KAMA MAKONDA ANGEKUWEPO VIJANA HAO WASINGEUAWA..!

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Makonda ambae tangu ateuliwe na Mh Rais Mstaafu JK amekuwa mfano wa kuigwa kwa wakuu wengi wa Wilaya hapa nchini kutokana na utendaji wa kazi mzuri anaoufanya wa kutatua Migogogro ya Ardhi pamoja na kero za vijana kuhusu Ajira na maendeleo makubwa. visit maskanibongotz

 Wananchi mbali mbali wakimtazama Baunsa, Amiri Abdallah(47), maarufu kwa jina la Chura Mchimba Makaburi ya Kinondoni, aliyejeruhiwa Dar es Salaam, akidaiwa kubomoa nyumba Wazo Hill Madale, akiwa na wenzake 26. mwaka juzi ambapo baunsa huyu ambae kwa sasa ni marehemu. Mgogoro huo wa Ardhi ulisababishwa na utendaji mbovu wa viongozi wa Manispaa ya Kinondoni huku ukihisiwa kuwa na harufu ya Rushwa.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli ambae wakazi wa Jiji la Dar wengi wamemuomba kumpandisha cheo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda na kuwa Mkuu wa Mkoa kijana ambae ataendana na sirogani yake ya hapa Kazi kwa vile ni mchapakazi mzuri.
Wakiongea na mtandao huu wa maskanibongotz wakazi hao toka maeneo mbaimbali walisema kuwa Makonda kwa kipindi kifupi amefanya makubwa sana kwenye maendeleo hasa kwenye Wilaya yake ya Kinondoni ambapo hadi sasa migogoro ya Ardhi ipo ukingoni kumalizika kumalizika hali iliyopelekea hata wilaya zingine za Jijini Dar kumtaka kuongoza Wilaya hizo
Makonda hivi karibuni alikuwa kwenye Kata ya Wazo maeneo ya Nakasangwe na Nakarekwa ambako kulikuwa na mgogoro wa miaka mingi na kufanikiwa kutuliza hali ya amani kiasi cha kuwafanya wakazi hao kuhisi kama nao ni watanzania kwani kabl yake hali ilikuwa mbayo ambapo ilidaiwa Mkuu wa Wailaya aliyemtangulia alikuwa anawaburuza wakazi hao kwa kutumiwa na wawekezaji na kutaka kuwahamisha wakazi hao wapatao 2700 ambao wengi wao ni wanachama wa CCM.
Hata hivyo Paul Makonda kwa kauri yake baada ya kusikiliza pande zote mbili za hao wawekezaji na wananchi aligundua kuwa kuna harufu kubwa ya rushwa iliyokuwepo, na wakazi hao walimweleza wazi wazi mkuu huyo kuwa ndani ya ofisi yake kuna watu ambao bado wanashirikiana na wawekezaji hao kuwakandamiza licha ya Mkuu wa Wilaya aliyeondoka
Jordan Rugimbana kumtuhumu ndiye alikuwe kinara wa kuwakandamiza wao.

Wakazi wote hao wamemuomba Mh Magufuli kutomuhamisha Paul Makonda Wilaya badala yake amuongezee cheo na kuwa mkuu wa Mkoa kwa vile Mkuu wa Mkoa aliyepo sasa kiumri anatakiwa kupumnzika.
Credit:maskanibongotz

No comments:

Post a Comment