TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, April 8, 2014

MASIKINI YA MUNGU WEE, UKATA WA MAISHA WASABABISHA DUDU BAYA AMTOE KAFARA MAMAAKE MZAZI AMKATA SIKIO NA KULIPELEKA SIKIO KWA MGANGA ILI ARUDI KWENYE CHATI..!

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo Flava Godfrey Tumaini Maarufu kwa jina la DUDU BAYA / MAMBA ameingia kwenye List ya wahalifu wanaotafutwa na jeshi la polisi jijini Mwanza, Taarifa hiyo imekuja baada ya kusemekana kuwa eti juzi alidhihirisha kuwa yeye ni DuduBaya baada ya kumvamia mama yake mkubwa na kumkata sikio lake, Akisimulia mkasa huo Mdogo wake Dudu tumbo moja anayeitwa MUETA amesema Juzi majira ya saa nne asubuhi jijini Mwanza DuduBaya alienda kwa mama yake mkubwa ambaye alikua anaumwa sana kutokana na uzee, Dudu alipofika pale alimuita mama yake mkubwa na hakuitikiwa ndipo alipomkokota mama yake mkubwa kutoka kibarazani nje na kumUingiza ndani sebuleni akamlaza kwenye kochi na kuanza kumkata sikio lakini hakufanikiwa kuling'oa lote kwasababu mama mkubwa alipiga kelele kuita majirani ndipo Dudubaya akatoka nje na kutokomea kusikojulikana, lakini wakati Dudu anafanya yote hayo mule ndani alikuwepo mtoto mmoja mdogo ambaye hakuweza kumzuia mjomba wake asifanye ukatili huo, majirani wakafika na kutoa msaada wa kwanza kwa bi Mkubwa na kumwahisha Hospitali ya Sekeu Toure akashonwa sikio, kwani sikio hilo halikukatika kabisa kwa sababu kisu alichokua anatumia Dudubaya kilikua butu, Kwa Mujibu wa Mdogo wa Dudubaya "Mueta" anasema eti Dudu anamtuhumu mama yake mkubwa kuwa ni mchawi na anamroga.
Tukio hili limeripotiwa polisi na DuduBaya anatafutwa na polisi kwa Udi na Uvumba.

No comments:

Post a Comment