TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Wednesday, December 4, 2013

MZIMU WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA WAWATAFUNA MASTAA WA KIUME BONGO MOVIE, RAY NA JB WAATHIRIKA VIBAYA, WASHAURIWA KUSTAAFA SANAA ILI KULINDA HESHIMA ZAO!








Na Mtu Msitu

Hakika kamwe huwezi kusafiria nyota ya mwenzako hata siku moja hiyo ndiyo kauri ya wanunuzi wa kazi za wasanii wa filamu Tanzania kufutia hali halisi iliyopo sasa kwenye tasnia ya uigizaji kwa ujumla ambapo viwango vya wasanii vimeshuka sana imebaki kusafiria  nyota zao za zamani.

XDEEJAYZ LIVE inakupa mtiririko mzima wa maoni ya wananchi ambao ndiyo nguzo pekee ya wasanii wote tanzani kwani ndio wanaowafanya wasanii hao kuonekana mastaa na wenye mafanikio, imeelezwa kuwa tangu taifa hili lilipompoteza msanii marehemu Stevan Charles Kanumba hapa mwaka jana ambapo ni mwaka mmoja na miezi hakuna msanii yeyote aliyethubutu kufata nyayo zake.

XDEEJAYZ iliamua kuingia mitaani kukusanya maoni ya mashabiki ambao kwa kweli wametoa yao mazito ya moyoni na kusema wasanii karibia wote ambao wanajiita mastaa wameisha kisanaa tangu alipofariki dunia Kanumba hakuna msanii hata mmoja aliyeonesha nia ya kuendeleza yale aliyokuwa anayafanya Kanumba kwa ajili ya kuifikisha kimataifa sana hii ya Bongo Movies.

Mashabiki hao waliieleza XDEEJAYZ walikuwa na matumaini makiubwa kwa msanii Vicent Kigosi “ Ray” kuwa huenda angeendeleza kazi za rafiki yake kipenzi Kanumba hata kabla ya umauti wa Kanumba Ray alionekana mpinzani mkubwa wa Kanumba huku wakichuana vikali kwenye sanaa kiasi cha wote kuon ekana bora. Lakini sasa baada ya Kanumba kufariki Ray kwa sasa anapumulia mashine hakuna lolote la maana alilolifanya kwenye sanaa.

Kanumba alikuwa chachu kwa sanaa ya Bongo na alikuwa na malengo makubwa sana pamoja na mikakati ya kuifikisha sanaa ya bongo mbali na kipindi chake wasanii wengi walionekana kuwa na upinzani mkali kila mmoja alitamani kufikia hatua aliyokuwa amefikia Kanumba, lakini cha kujiuliza ni kwamba ziko wapi hizo harakati tena kwani wasanii wote wa Bongo movie hasa wa kiume wamepotea vibaya baada ya kifo chake hali inayoelewza huenda mzimu wa Kanumba unawatafuna.

Wasanii wengi tu walionekana kuwa wapinzani na hawa ni baadhi tu kama vile JB, Mtitu, Dk Chen, Eliya Mjata, Mtunisi,Benny, Swebe,Richie, Ray, Stev Nyerere, Slim Omar, Kaprado, Patcho, nk. Hawa waliotajwa naweza kusema ni wale wakongwe sana ambao wako walioanza sanaa na marehemu Kanumba na wengine walikutana kwenye fani ukubwani.

Lakini hata hivyo Ray na Jb ndio watu waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kuvaa viatu vya Kanumba lakini imekuwa patupu Jb hajaonesha nia ya kuifikisha sanaa hii ya kimaifa kama ilivyokuwa kwa Kanumba “ Jb alikuwa mmoja wa wasanii waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kuifiksha sanaa ya bongo kimataifa lakini sasa hivi hakuna lolote analolifanya zaidi ya kuwa hapa hapa na hata kazi zake anazozitoa hazina ubora zimekosa vionjo vya kimataifa hali hiyo inadhihilisha kweli wote hao walikuwa wanasafiria nyota za Kanumba” Alisema Mama Ismail mshabiki wa Bongo Movie

Aidha mtu mwingine aliyekuwa anapewa nafasi ni Ray kutokana na upinzani mkubwa aliokuwa anauonesha kipindi cha Kanumba akiwa hai lakini kwa sasa mmh ni Majanga matupu, Ray amekwisha kabisa kisanaa  kiasi cha baadhi ya mashabiki wenye mionyo miepesi wanadiriki bora msanii huyo angechukua maamuzi magumu ya kustaaf sanaa na angezalisha wasanii wachanga huenda hapo angejitengenezea sifa kubwa sana.

Tangu kuondoka kwa maarehemu Kanumba Ray ametengeneza kazi nyingi sana lakini hadi sasa hakuna hata kazi moja iliyofanya vizuri tofauti na zile alizokuwa akishindana na Kanumba ambapo alikuwa anapata pesa kutokana na nyota ya Kanumba lakini kwa sasa kazi zake hazilipi na amebaki kusafarilia nyota ya zamani.

XDEEJAYZ ilitenda haki  na kuwatafuta RAY na JB ili kuzungumzia suala hili la mshabiki wao kuwalalamikia kushuka kisanaa, lakini kwa bahati mbaya simu ya Ray iliita bila kupokelewa huku simu ya JB ilikatwa kila ilipopigwa hali iliyoonesha huenda alikuwa Location akiwajibika. 
"GAZETI LA MASKANI BONGO MTAANI WIKI IJAYO USIKOSE KUKAMATA KOPI YAKO KWA HABARI NA MATUKIO YA PICHA HAPO UTAKATA KIU YAKO"

1 comment:

  1. Kanumba alikua juu zaidi,na hawa wajamaa hawawezi kitu.

    ReplyDelete