TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Wednesday, December 4, 2013

BIFU ZITO: MASHABIKI WA AUNT LULU WAMVUA NGUO BOND WA WASTARA, WAMWAMBIA BILA LULU KUMTEMBEZA MJINI HAKUNA MTU ANGEMJUA!




Na Sakina Shabani
Prodyuza chipukizi kwenye tasnia hiyo Bond Bin Sinnon amechanwa ile mbaya na mshabiki wa mtangazaji mwenye rekodi  ya kuanza fani hiyo akiwa na umri mdogo “ 13” Lulu Hemagongo huku wakimtaka Prodyuza huyo kuacha kuongea kitu mbele ya Aunt Lulu kutokana na msaada mkubwa alioupata toka mtangazaji huyo hadi leo hii anaonekana mtu flani kwenye jamii.
Wakiongea na XDEEJAYZ ambayo ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuripo taarifa mahusiano ya Bond na Wastara kabla ya habari hiyo kusambaa kwenye mitandao mingine, mashabiki hao walisema kuwa Bond amekosea sana kusema kuwa Lulu anatafuta umaarufu kupitia kwake wakati yeye ndiye aliyepata jina kupitia Lulu kwani ndiye aliyempatia nafasi ya kupewa kipindi Channel Ten huku akimuhangaikia mambo mengi tu hadi leo hii anaonekan Bond.
Mashabiki hao waliongeza kuieleza XDEEJAYZ  na kusema kuwa Bond hakuwa na nyuma wala mbele lakini Lulu alikuwa msaada mkubwa kwake ambapo alianza kumtambulisha kwa wadau hapa mjini pamoja na kumpeleka kwa mguu wake hadi Channel Ten pamoja kampuni ya Beknet Production ambako ndiko alikoajiliwa hadi sasa huko kote huko Lulu ndiye aliyekuwa akimshika mkono kumuonesha mji unavyoenda.
Aidha nao watu wa karibu na Bond walioneshwa kushangazwa na kauri ya Bond ya kuwa Lulu anataka umaarufu kupitia yeye jambo ambalo sio kweli Bond” Kwanza Lulu alishamuacha Bond muda mrefu sana zaidi ya miaka miwili sasa huku kila mmoja anafanya yake sasa haingii akilini kwamba kwanza Lulu ni msomi kuliko Bond na hata leo hii Wastara kamuona yeye kupitia Lulu sasa iweje aseme kuwa Lulu anamuonea wivu huu ni ukosefu wa fikra” Alisema Alfan Mohamed ambae ni rafiki wa karibu.
Hata hivyo Lulu alipotafutwa kupitia simu yake mkononi alipatikana na kusema kuwa hataki kuzungumzia chochote kuhusu hilo kwani Mungu mwenyewe ndiye anaejua
"GAZETI LA MASKANI BONGO LITAKUWA MTAANI WIKI IJAYO USIKOSE KOPI YAKO KWA HABARI NA MATUKIO YA PICHA" 

No comments:

Post a Comment