Na Mtu Msitu
Hakika kamwe
huwezi kusafiria nyota ya mwenzako hata siku moja hiyo ndiyo kauri ya wanunuzi
wa kazi za wasanii wa filamu Tanzania kufutia hali halisi iliyopo sasa kwenye
tasnia ya uigizaji kwa ujumla ambapo viwango vya wasanii vimeshuka sana imebaki
kusafiria nyota zao za zamani.
XDEEJAYZ
LIVE inakupa mtiririko mzima wa maoni ya wananchi ambao ndiyo nguzo pekee ya
wasanii wote tanzani kwani ndio wanaowafanya wasanii hao kuonekana mastaa na
wenye mafanikio, imeelezwa kuwa tangu taifa hili lilipompoteza msanii marehemu
Stevan Charles Kanumba hapa mwaka jana ambapo ni mwaka mmoja na miezi hakuna
msanii yeyote aliyethubutu kufata nyayo zake.
XDEEJAYZ
iliamua kuingia mitaani kukusanya maoni ya mashabiki ambao kwa kweli wametoa
yao mazito ya moyoni na kusema wasanii karibia wote ambao wanajiita mastaa
wameisha kisanaa tangu alipofariki dunia Kanumba hakuna msanii hata mmoja
aliyeonesha nia ya kuendeleza yale aliyokuwa anayafanya Kanumba kwa ajili ya
kuifikisha kimataifa sana hii ya Bongo Movies.
Mashabiki
hao waliieleza XDEEJAYZ walikuwa na matumaini makiubwa kwa msanii Vicent Kigosi
“ Ray” kuwa huenda angeendeleza kazi za rafiki yake kipenzi Kanumba hata kabla
ya umauti wa Kanumba Ray alionekana mpinzani mkubwa wa Kanumba huku wakichuana
vikali kwenye sanaa kiasi cha wote kuon ekana bora. Lakini sasa baada ya
Kanumba kufariki Ray kwa sasa anapumulia mashine hakuna lolote la maana
alilolifanya kwenye sanaa.
Kanumba
alikuwa chachu kwa sanaa ya Bongo na alikuwa na malengo makubwa sana pamoja na
mikakati ya kuifikisha sanaa ya bongo mbali na kipindi chake wasanii wengi
walionekana kuwa na upinzani mkali kila mmoja alitamani kufikia hatua aliyokuwa
amefikia Kanumba, lakini cha kujiuliza ni kwamba ziko wapi hizo harakati tena
kwani wasanii wote wa Bongo movie hasa wa kiume wamepotea vibaya baada ya kifo
chake hali inayoelewza huenda mzimu wa Kanumba unawatafuna.
Wasanii
wengi tu walionekana kuwa wapinzani na hawa ni baadhi tu kama vile JB, Mtitu,
Dk Chen, Eliya Mjata, Mtunisi,Benny, Swebe,Richie, Ray, Stev Nyerere, Slim
Omar, Kaprado, Patcho, nk. Hawa waliotajwa naweza kusema ni wale wakongwe sana
ambao wako walioanza sanaa na marehemu Kanumba na wengine walikutana kwenye
fani ukubwani.
Lakini hata
hivyo Ray na Jb ndio watu waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kuvaa viatu vya
Kanumba lakini imekuwa patupu Jb hajaonesha nia ya kuifikisha sanaa hii ya
kimaifa kama ilivyokuwa kwa Kanumba “ Jb alikuwa mmoja wa wasanii waliokuwa
wanapewa nafasi kubwa ya kuifiksha sanaa ya bongo kimataifa lakini sasa hivi
hakuna lolote analolifanya zaidi ya kuwa hapa hapa na hata kazi zake anazozitoa
hazina ubora zimekosa vionjo vya kimataifa hali hiyo inadhihilisha kweli wote
hao walikuwa wanasafiria nyota za Kanumba” Alisema Mama Ismail mshabiki wa
Bongo Movie
Aidha mtu
mwingine aliyekuwa anapewa nafasi ni Ray kutokana na upinzani mkubwa aliokuwa
anauonesha kipindi cha Kanumba akiwa hai lakini kwa sasa mmh ni Majanga matupu,
Ray amekwisha kabisa kisanaa kiasi cha
baadhi ya mashabiki wenye mionyo miepesi wanadiriki bora msanii huyo angechukua
maamuzi magumu ya kustaaf sanaa na angezalisha wasanii wachanga huenda hapo
angejitengenezea sifa kubwa sana.
Tangu
kuondoka kwa maarehemu Kanumba Ray ametengeneza kazi nyingi sana lakini hadi
sasa hakuna hata kazi moja iliyofanya vizuri tofauti na zile alizokuwa
akishindana na Kanumba ambapo alikuwa anapata pesa kutokana na nyota ya Kanumba
lakini kwa sasa kazi zake hazilipi na amebaki kusafarilia nyota ya zamani.
XDEEJAYZ
ilitenda haki na kuwatafuta RAY na JB ili kuzungumzia suala hili la mshabiki wao
kuwalalamikia kushuka kisanaa, lakini kwa bahati mbaya simu ya Ray iliita bila
kupokelewa huku simu ya JB ilikatwa kila ilipopigwa hali iliyoonesha huenda
alikuwa Location akiwajibika.
"GAZETI LA MASKANI BONGO MTAANI WIKI IJAYO USIKOSE KUKAMATA KOPI YAKO KWA HABARI NA MATUKIO YA PICHA HAPO UTAKATA KIU YAKO"
Kanumba alikua juu zaidi,na hawa wajamaa hawawezi kitu.
ReplyDelete