"GAZETI LA MASKANI BONGO SASA LINAPATIKANI MTAANI KILA SIKU ZA JUMATANO PATA KOPI YAKO "
TANGAZO MAALUM
TANGAZA NA SISI
Monday, December 30, 2013
WAKULIMA NA WAFUGAJI WACHINJANA KAMA NG'OMBE KITETO, XDEEJAYZ INAOMBA RADHI KWA KUONESHA PICHA HII YA KUTISHA. Kiteto...!
Miongoni mwa waliouawa kinyama Dec 20 kwa kuchinjwa shingo yake ni Juma Mlagwa (49) wa Kitongoji cha Kalikala Kata ya Njoro (Kiteto) ambaye alivamiwa nyumbani kwake usiku na kundi la vijana wa kifugaji masai (makorianga)
Imeelezwa kuwa wakati anavamiwa zilisikika Risasi zikipigwa juu Kitongojini hapo na baada ya watu kuendelea kujificha ndani vijana hao walianza kunyunyizia nyumba zao mafuta aina ya petrol kisha kuwasha moto
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Ally Mussa Mwenyekiti wa Kitongoji hicho alisema siku hiyo haitasahaulika mashani mwake kwa yaliyotokea kutokana na vitendo hivyo akisema ilikuwa mara ya kwanza kuona mtu anachinjwa hadharani
“Nilichomewa Pikipiki zangu mbili pamoja na vitu mbalimbali vya ndani zikiwemo nguo, vyakula, lakini nilichonusuru ni roho yangu ambayo hadi leo nasema najivunia uhai nilio nao”alisema Mwenyekiti huyo
Alisema chanzo cha mauaji hayo ni jamii ya kifugaji wamasai kuingiza mifugo yao kwenye shamba la mmoja wa wakulima Kitongojini hapo na baada ya kukatazwa walimpiga kisha nae kupigwa ndipo wakakusanyana kupanga uvamizi huo
Hata hivyo baada ya kufikishwa taarifa kwa viongozi wa Serikali walidaiwa kulifika Kitongojini lakini walikataa kwenda kuongea nao km chache kwa madai kuwa ni uongo kwamba hakuna watu waliokusanyana
Akielezea hayo Mwenyekiti huyo alisema tatizo ni uongozi dhaifu kuanzia ngazi ya Kitongoji hadi Wilaya ambapo alidai kuwa ukabila umeshamiri kwa viongozi kujiona kuwa wanahaki ya kutfanya utetezi katika upande mmoja
Kwa upande wake Lairumbe Mollel Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya akizungumzia sakata hilo alimzodoa mwenyekiti huyo wa Kitongonji kuwa ni muongo kwani baada ya wao kufika kabla ya tukio alikataa kuwataja wahusika
Hata hivyo kauli hiyo ilionekana kutokuwa na mashiko baada ya mwenyekiti huyo wa Kitongoji kuonyesha udhaifu wa viongozi hao akisema baada tu ya kufika hawakuweza hata kukubali kupelekwa walikoweka kambi vijana hao wa kimasai
“Baada ya kufika walitaka nisema majina ya walioleta fujo na nilipowataka twende eneo la tukio wakakata nakuona kuwa hawakuwa na njia njema kisha wakarejea Kiteto ambapo usiku vijana hao wakatekeleza azima yao ya kuchinja mtu mmoja na kumpiga mwingine risasi kisha kuwajeruhi watu saba”alisema Mwenyekiti huyo wa kitongoji
Waliofariki katika uvamizi huo ni pamoja na Juma Malagwa (49) ambaye alichinjwa shingo, Yohana Ivo (33) ambaye alipigwa sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kifo pamoja na watu wengine saba kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa kujeruhiwa kwa fimbo na mapanga
Waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto ni Hoti Daniel (38) Emanuel matias (21) Juma Bahati (13) Mwajuma Hamisi (20) Habiba Ally (16) Mwajuma Martin pamoja na Musa Juma (16) aliyepelekwa Dodoma kwaajili ya matibabu
Hata hivyo mkuu huyo wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwillo akiwa katika kitongoji hicho aliwapa siku 30 viongozi wa Wilaya ya Kiteto kuweka utaratibu wa kuwatambua wananchi hao ili kuondoa tofauti zao waweze kufanya kazi bila bughdha
“Ninyi wananchi mwende kujisajili Kijijijini ili Serikali iwatambue kwani maisha bora kwa wananchi yatapatikana kwa kufahamika mlipo ili mpatiwe huduma za jamiiambazo kwa sasa hamna hata moja,” alisema Mbwillo.
"CLUB MAISHA KUWA WA KWANZA KUUONA MWAKA MPYA KESHO USIKOSE MKESHA WA KIHISTORIA NDANI YA CLUBM MAISHA DODOMA MBEYA, MTWARA, MOROGORO NADAR"
RAIS OBAMA, MICHELLE WADAIWA KUTENGANA. MWANAMKE HUYO AFUNGASHA NGUO ZAKE KUTIMKIA KWAO..!!!
Mgogoro baina ya wawili hao ulianza zamani na wameweza kuendelea kuishi pamoja kwa sababu ya watoto wao wawili wa kike Sasha na Malia na kulinda heshima ya urais.
Michelle anadai amechoka na atakutana na mwanasheria wa masuala ya talaka ili aweze kuachana na rais huyo wa 44 nchini Marekani. Michelle ataendela kuishi Ikulu 'White House' kwa muda wote uliobaki katika kipindi cha utawala wa Obama, ila ameweka wazi kuwa watakuwa wakiishi vyumba tofauti.
Anataka kuishi katika chumba kimojawapo cha familia kilichowazi na anajiandaa kuhamisha nguo zake na kila kilicho chake kutoka kwenye jumba lao la kifahari la mamilioni ya dola lililopo Chicago.
Michelle alichanganyikiwa zaidi baada ya Obama kupiga picha za kimahaba akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt, wakati wa mazishi ya marehemu Nelson Mandela nchini Afrika Kusini.
Obama mwenye miaka 52, alikuwa akifurahi, kunong'enezana na kumshika begani mrembo huyo mwenye umri wa miaka 46 ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa Denmark tangu Oktoba 3, 2011.
"GAZETI LA MASKANI BONGO MTAANI KILA JUMATANO USIKOSE KOPI YAKO"
Sunday, December 29, 2013
KUNDI LA KHANGA MOJA LAPIGWA MARUFUKU KUKANYAGA MKOANI BUKOBA, WAAMBIWA WAKITIA PUA ZAO HUKO WATACHOMWA MOTO!
Na Sakina Shabani
Kundi la Khanga Moja la Jijini Dar limepigwa marufuku kukanyaga Mkoani Bukoba kutokana na vitendo vya kifuska walivyovifanya huko.
Kwa mujibu mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina Rubangila aliimbia Xdeejayz kuwa kundi hilo limeacha laana kubwa sana mkoani humo kiasi cha kutia kinyaa hivyo wananchi mbalimbali wamesema kuwa hata siku moja wasithubutu kutia pua zao kwenye ardhi hiyo... Habari zaidi usikose gazeti la Maskani Jumatano tarehe 1.
Friday, December 27, 2013
WEMA NA DIAMOND MAPENZI MOTO MOTO KWA SASA...!!!!
Tukio hilo lilitokea jana pale Leaders club kwenye show ya Diamond ambapo Wema Sepetu alipanda kwenye stage na kuongea na mashabiki waliofika kwenye show hiyo....
Kwenye hiyo show, Diamond aliuliza,”Mnataka kumjua mchumba wangu”? Show ilivyoendelea Diamond alitaka kuimba wimbo wa "ukimwona" akasema:
“Nasikia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani”.
Baada ya kauli hiyo, Wema Sepetu alipanda kwenye stage kisha wakakumbatiana na kucheza wote.
H
WANAMUZIKI MAARAFU WAZIDI KUJIUNGA NA CHADEMA, ROMA MKATOLIKI ACHUKUA KADI YA UNACHAMA KWA MBWEMBWE..!!!
Roma Mkatoliki akiongea na mabest zake Wa Mtaani huko Tanga amesema ana mpango Kuingia Kwenye Uringo wa Kisiasa ili apate nafasi Nzuri ya Kuikosoa Serikali baada ya Muziki wake Kupuuzwa na Viongozi wa Taifa hili.
“Naplan Kuzamia Kwenye Mambo ya Politics hivi sasa, By the Way Wiki Ijayo naweza Kuchukua Kadi ya Chadema Rasmi”… Pia amesema Atahakikisha Wasanii Wenzake wanaoimba Muziki wa HipHop akina Kala Jeremiah nao Wanaunda timu ya Maangamizi Kuing’oa CCM Madarakani, ila aliwasihi sana Viongozi wa Chadema Kuwa Karibu nao pale Wanapozushiwa Shutuma za ajabu ajabu Kisa Wamejiunga na Chadema.
Mpaka sasa baadhi ya wanamuziki wa Bongo Fleva waliojiunga na ambao wanampango wa kujiunga na Chama Cha kuwakomboa wanyonge CHADEMA ni Afande Sele wa Morogoro, Joseph Haule ambaye anajulikana kama Prof J, Soggy Doggy na Wengineo wengi.
"SASA CLUB MAISHA ZINAPATIKANA DODOMA, MTWARA, IRINGA, MBEYA, MOROGORO NA DAR KAZI NI KWAKO"
Thursday, December 26, 2013
MAN WOLTER: STUDIO MPYA ZA COMBINATION MOBILE KUTUMIA MILION 200!
Na Jemsi Luhunga
Prodyuza maarufu
nchin John Vomo Shariza “ Man
Wolter” ambae ni mmilki wa Studio
maarufu ya Combination amesema anaenda kufunga mwaka kwa kufanya mabadiliko
makubwa kwa kutengeneza studio kubwa ya kisasa pamoja na kununua magari maalum
ya Mobile Studio ambayo yote yatatumika kwenye kazi hiyo ya muziki.
KWA HABARI ZAIDI NDANI YA GAZETI LA MASKANI BONGO USIKOSE LIPO MTAANI..!!!
AY ASIMAMISHA SHUGHURI ZA MUZIKI KWANZA ILI KUJIPANGA UPYA 2014..!!!
Na Hawamu Juma
Mwanamuziki wa
kimataifa Ambene Yesaya “AY” amesema kuwa kwa sasa amesimamisha masuala yoyote
yanayohusiana na muziki na kugeukia
mambo mengine.
Akionge na
Maskani Bongo AY alisema” Kaka kwa sasa nimesimama sitaki kufanya chochote
kunachohusiana na muziki badala yake nafanya mambo yangu binafsi ambayo
nisingeweza kuyaweka wazi itakuwa sio poa” Alisema AY
HABARI ZAIDI ZINAPATIKANA KWENYE GAZETI LA MASKANI BONGO
MIMI SINA UNDUGU NA KIKUNDI KINACHOITWA BONGO MOVIE-BARAFU...!!
Na Sakina Shabani
Muigizaji mahali
kwenye nchini Sulemain Barafu ameibuka na kusema kamwe hana uhusiano wowote na
kundi la Bongo Movie zaidi ya kujuana na wasanii wenzake ikiwa ni pamoja na
kushirikiana kikazi na kipindi cha matatizo lakini si kwenye mambo mengine yanayoangaliwa
kwa jicho la tatu na jamii.GAZETI LA MASKANI BONGO LIKO MTAANI PATA KOPI YAKO SASA
MAGOLI YA HAMISI TAMBWE KWA YANGA YAMKIMBIZA RAY UWANJANI!
Na Shumba Msitu
Katika hali
isiyokuwa ya kawaida Magoli yaliyofungwa na mchezaji wa kimataifa anaeichezea
timu ya Simba Hamis Tambwe dhidi ya timu ya Yanga yalimkimbiza mapema uwanjani
msanii nyota wa maigizo Vicent Kigosi “Ray” ambae ni shabiki mkubwa wa Yanga.
Ray ambae
alikuwepo uwanjani pamoja na wasanii wengine kama Steve Nyerere huku akiwa
amevalia kofia ya kijana pamoja na traksuti ya njano, alishuhudia timu yake
ikifungwa magoli 3-1 na magoli ya simba 2 yakifungwa na Hamis Tambe moja
akifunga kwa penaiti na jingine akishinda kawaida.
Paparazi wetu
aliyekuwepo uwanjani alishuhudia mastaa wengi hasa wa Bongo Movie kama Michael
Sangu, Kupa, Shamsa Ford,Barafu wakiongozwa na Ray ambae baada ya Magoli hayo yaliyofungwa Ray alikimbia
uwanjani mapema kabla ya mechi kumalizika .HABARI ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO ZINAPATIKANA KWENYE GAZETI LA MASKANI BONGO..!!!
ULOKOLE WAMSATAAFISHA SANAA MZEE MAGALI, KUTIMKIA MAREKANI FEB 2014
Na Sakina Shabani
Msanii nyota
kwenye tasinia ya filamu nchini Charles Thobias Magali " Mzee Magali"
amsema kuwa huenda mwaka huu 2013 ukawa mwisho wake wa kuigiza kwani anahitaji
kuachana na sanaa na anataka kwenda Marekani kula maisha na mchumbaake wake wa
muda mrefu ambae ni mzungu muhudumu wa Kanisa.
Akiongea na
Maskani Bongo Mzee Magali ambaye yuko Mkoani Morogoro akimalizia kazi za watu
alizochukua hela kwa ajili ya kuigiza lakini baada ya hapo atafunga kuigiza
tena kwani mwakani miezi anasafari hiyo ndefu angani.
HABARI ZAIDI UTAZIPATA NDANI YA GAZETI LA MASKANI BONGO LIPO MTAANI KILA KUMATANO
NITAENDELEA KUWATETEA MASHOGA HADI MWISHO WA UHAI WANG-AUNT LULU
Na Shumba Msitu
Mtangazaji nyota
nchini Lulu Semagongo ameibuka na kusema kuwa ataendelea kuwatetea wanaume ambao si ridhiki "Mashoga"
ili wasinyanyasikie kwenye jamii hadi mwisho wa uhai wake.
Akiongea kwa njia
ya simu na mwandishi wetu Lulu alisema amekuwa akiumia sana kuona watu wq
jinsia hiyo wakiteswa na wengine kuuawa kisa tu ni mashoga hiyo siyo haki ni
ukiumwaji wa hali za binadamu kwani mashoga ni binadamu kama alivyo binadamu
mwingine.HABARI ZAIDI NDANI YA MASKANI BONGO LIKO MTAANI KILA JUMATANO
WEMA, DIAMOND WAKIMBIZANA VIBAYA KWENYE NAMBA MOJA SOMA HII..!!!
Na
waandishi wetu
WAKATI
mwaka 2013 ukielekea ukingoni na kuukaribisha 2014, mastaa wawili Wema Sepetu
na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’ wameonekana kuwa bado wako juu kwa kupendwa
sana na mashabiki kuliko nyota wengine wote.
Wema
Sepetu, muigizaji nyota wa filamu Tanzania na Diamond, kinara wa muziki wa
kizazi kipya ndiyo wasanii waliokimbiza sana kwa kazi na hovyo kuendelea
kujipatia mashabiki kila kukicha.
Wema
Isack Sepetu mwaka huu ameendelea kuwa kinara kwa kuwafunika mastaa wote wa
kike kwenye kila idara kuanzia fedha,
kupendwa pamoja na kung’ara karibu kwenye kila jambo analofanya.
Habari zadi zinapatikana ndani ya gazeti la Maskani Bongo lipo mtaani Kila Jumatano
Tuesday, December 24, 2013
HII NDIYO RATIBA NZIMA YA BURUDANI CLUB MAISHA DODOMA, MTWARA, MBEYA, MOROGORO NA DAR MSIMU HUU WA SIKUKUU..!!
Kampuni ya
Entertainment Masters LTD inayomiliki Club Maisha zote Tanzania, Dodoma, Mbeya,
Ntara,Morogoro na Dar imetangaza ratiba nzima ya burudani kwenye Club Maisha
zake zote.
Akiongea na
Xdeejayz Meneja wa kampuni hiyo Mr Ndawula alisema “ Ni wiki mbili za
kukumbukwa nchini Tanzania hasa kwa wapenda burudani wa mikoa yote
kunakopatikana Miasha Club hivyo watu wafike kwa wingi kujionea burudani
tofauti” Alisema Mr Ndawula
Aidha
Meneja huyo alitoa pongezi kwa wakazi wa mji wa Mogorogo wale wote waliofika
kwenye uzinduzi wa Club Maisha kwani ulikuwa uzinduzi wa aina yake maelfu ya
watu walifika kujionea uzinduzi huo huku wengi wakionekana kudatishwa na kikosi
kazi cha Xtreme Dejeeyz Drummer Live Dj .
Meneja huyo
alisema burudani zimeanza mapema wiki siku Jumanne na zitaendelea hadi Jumapili
huku baada ya Jumatatu ijayo Jumanne
tena mshike mshike hadi mwakani.
"GAZETI LA MASKANI BONGO MTAANI KESHO USIKOSE KOPI YAKO"
Subscribe to:
Posts (Atom)