TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, December 26, 2013

MAGOLI YA HAMISI TAMBWE KWA YANGA YAMKIMBIZA RAY UWANJANI!



Na Shumba Msitu
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Magoli yaliyofungwa na mchezaji wa kimataifa anaeichezea timu ya Simba Hamis Tambwe dhidi ya timu ya Yanga yalimkimbiza mapema uwanjani msanii nyota wa maigizo Vicent Kigosi “Ray” ambae ni shabiki mkubwa wa Yanga.
Ray ambae alikuwepo uwanjani pamoja na wasanii wengine kama Steve Nyerere huku akiwa amevalia kofia ya kijana pamoja na traksuti ya njano, alishuhudia timu yake ikifungwa magoli 3-1 na magoli ya simba 2 yakifungwa na Hamis Tambe moja akifunga kwa penaiti na jingine akishinda kawaida.
Paparazi wetu aliyekuwepo uwanjani alishuhudia mastaa wengi hasa wa Bongo Movie kama Michael Sangu, Kupa, Shamsa Ford,Barafu wakiongozwa na Ray ambae  baada ya Magoli hayo yaliyofungwa Ray alikimbia uwanjani mapema kabla ya mechi kumalizika .
HABARI ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO ZINAPATIKANA KWENYE GAZETI LA MASKANI BONGO..!!!

No comments:

Post a Comment