Taarifa tulizozipata zinaarifu kuwa Balozi Isaac Abraham Sepetu ambaye ni baba mzazi wa Wema Sepetu ameaga dunia.
Balozi Sepetu alikuwa amelazwa kwa miezi kadhaa hospitalini jijini Dar es Salaam kwa maradhi ya kiharusi na kisukari na mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.
Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarag Nyerere.
Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere. Machi 27, mwaka huu, Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein, kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega uchumi ya Zanzibar (ZIPA).
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amina.
No comments:
Post a Comment