Mama na mwanae wameuawa kikatili baada ya kukatwa mapanga na baadhi ya viungo vyao kuchomwa moto katika tukio linalohusishwa na imani za kishirikina lililotokea mkoani Shinyanga.
Wanawake hao vikongwe mtu na mtoto wake
ni Jadi Temi (90) na mwanae Samara Mathias (70) wakazi wa kijiji cha
Ikonda wilayani Shinyanga.
Wawili hao walishambuliwa na kuuawa juzi
na watu wasiojulikana wakiwa wamekaa nje ya nyumba yao wakiota moto na
kufurahi chakula cha usiku.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinha Kihenya
Kihenya, alisema vikongwe walishambuliwa na mapanga sehemu mbalimbali
za miili yao na kufa papo hapo huku baadhi ya viungo vya Samara
vikitupwa kwenye moto uliokuwa jirani.
Kihenya alisema tukio hilo lilitokea
Ijumaa saa 2:00 usiku katika kijiji cha Ikonda wilayani Shinyanga,
wakati wawili hao wanaoishi peke yao wakila chakula na kuota moto.
Kihenya alifafanua kuwa mara baada ya
kushambulia na kuua wauaji hao wakikata kichwa cha Samara, kiganja cha
mkono wa kushoto na mguu wa kulia na kuvitupa kwenye moto uliokuwa
jirani .
Alisema wauaji hawakuiba chochote na kuna wasiwasi kuwa mauaji hayo yamefanywa kutokana na ushirikina .
No comments:
Post a Comment