TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, June 28, 2013

AIBU KUBWA KWA SERIKALI, MWANAMKE AJIFUNGULIA KWENYE BODABODA IKIWA MWENDO KASI, KICHANGA NUSU KIDONDOKE CHINI!

 
Josephine Michael akiwa barabarani baada ya kujifungua.


Wananchi waliofika eneo hilo wakiwa na Josephine (aliyekaa chini).


Hivi ndivyo hali ilivyokuwa baada ya Josephine kujifungua salama mtoto wa kiume

BINTI mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua barabarani wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa bodaboda.
  Tukio hilo lililo
washtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kumshuhudia askari wa kike wa kikosi cha usalama barabarani ‘trafiki’ (jina lake halikupatikana) akiacha kazi ya kuong
oza magari na kugeuka mkunga kwa muda ili kumsaidia binti huyo akiwa sambamba na wanawake wengine na kufanikisha kupatikana kwa mtoto wa kiume ‘dume la nguvu’.
Mmoja wa akina mama waliofika eneo hilo akiwa amembeba mtoto wakati mama yake akihojiwa na mwanahabari.

Awali, wanawake hao walizungusha kanga ili kuweza kuweka usiri wakati wa kumsaidia mwanamke mwenzao alipokuwa akijifungua.

Mara baada ya zoezi hilo kwenda salama, Josephine alisema alipatwa na uchungu alfajiri ya siku hiyo na mume wake aliwapigia simu madereva wa teksi zaidi ya wawili ambao waligoma kufika kijijini kwao kutokana na ubovu wa barabara.

Kulia ni trafiki aliyemsaidi Josephine kujifungua na kushoto mtoto aliyezaliwa akiwa amebebwa.
“Hali ilipozidi kuwa mbaya tuliwasiliana na dereva wa bodaboda ambaye alifika na kunibeba huku mume wangu akitufuatilia nyuma kwa baiskeli yake,” alisema Josephine kwa uchangamfu.


Binti huyo alisema kwamba walipofika eneo la Nanenane hali ilizidi kuwa mbaya akashindwa kujizuia baada ya mtoto kushuka chini, hivyo akamuomba dereva wa bodaboda asimame ndipo alipoanguka chini na hali kuzidi kuwa mbaya.
Baada ya kuliona tukio hilo, trafiki na wanawake wengine waliokuwa jirani wakajitolea kumsaidia hadi alipojifungua salama.
Dereva wa bodaboda aliyembeba Josephine anayejulikana kwa jina la Gitogo Shilagi alikiri barabara iendayo Kijiji cha Kiegea kuwa mbovu.

SHEKH SHARIF WA TANZANIA AZUSHA BALAA KUBWA NCHINI KONGO,WANAJESHI WAMUWEKA MTU KATI!

 Maelfu ya wananchi wa mji wa Bunjumbula wakiwa wamemzunguka Shekh Sharif mwenye bendera ya Tanzania kichwani.

 Maelfu ya wananchi wa mji wa Bunjumbula wakiwa wamemzunguka Shekh Sharif mwenye bendera ya Tanzania kichwani.
 Shekh Sharif mwenye kanzu akiwa mbele ya gari yake nchini Kongo hivi karibuni.
Na Livingstone Mkoi
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua kijana mwenye miujiza ya ajabu nchini Shekh Sharif Khamis hivi karibuni alizusha balaa katika nchini za Kongo, Burundi, Angora na Rwanda kiasi cha kusabaisha maafa  baada ya mihadhara yake kujaza maelfu ya watu hadi kushindwa kupumua.

Habari zaidi toka nchini hizo zilizonaswa na gazeti hili zilisema kijana huyo  amekuwa lulu kila anapotembelea kwenye nchi hizo kiasi cha wakuu wan chi hizo kupigwa na butwaa na kupelekea kumpa Mungu utukufu kwa kumjalia kijana huyo karama za hali ya juu.
 Wakiongea na gazeti hili baadhi ya wakazi wa miji ya Kigari,Bunjumbura na Luanda mji mkuu wa Angora walisema katika mihadhara yote aliyoiifanya kijana huyo watu mbalimbali wameponywa magonjwa yao kuna wakati hata waliokuwa wakiigusa kanzu yake tu walipona.

 Aidha katika miujiza mingine iliyofanywa na kijana huyo mwenye historia ya kutisha katika mashekh Sharif walipita ndani ya Tanzania ambapo kijana huyo alianza kuzungumza akiwa na umri wa mwaka mmoja baada ya kutoa kauri ya kumtaka babaake aache pombe mara moja na tangu kipindi hicho amekuwa akimtumikia mwenyezi mungu kwa kuwaombea watu dua kisha huwanyooshea kidole cha kati na hupona papo hapo.

 Mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Zaitun Bint Juma mkazi wa Kigari aliliambia gazeti hili kwa njia ya siku kuwa “ Katika historia ya Uislamu haijawahi kutokea kijana mwenye nguvu za kutisha kama Shekh Sharif Khalif kwani maelfu ya watu wamepona kwa dua zake” Alisema Zaitun

 Gazeti hili lilibahatika kuzungumza moja kwa moja na Shekh Sharif toka nchini Burundi muda mfupi akiwa amerejea toka nchini Kongo alisema “ Kwanza namshukuru mwenyezi mungu kwa kuwaponya watu wake kupitia sisi watumishi wake hivyo nimefanya mambo makubwa sana kwenye nchi zote nilizotembelea hakika mungu ni  mwema alinijaza kalama za ajabu ambapo maelfu ya watu wamepona kwenye matatizo yao” Alisema kijana huyo

Hata hivyo kijana huyo aliongeza kusema alipatwa na misukosuko ndani ya mpaka wa        Kongo na Burundi baada ya kuwekwa mtu kati na wanajeshi wan chi hizo na kutaka kujuwa kwa nini gari yake iliwekwa bendera ya Taifa la Tanzania yeye ni nani” Shekh alisema waliwekwa chini ya ulinzi masaa kadhaa kabla ya kuachiwa baada ya kuwaeleza kuwa yeye ni mtanzania na yuko kwa ajili ya kuitumia jamii.

Thursday, June 27, 2013

SASA KAZI IMEANZA UJIO WA OBAMA. HELKOPTA ZA KIJESHI ZAANZA KUINGIA KIMYAKIMYA AIR PORT ZANZIBAR NA DAR!

 Baadhi ya Helkoper za kijeshi toka Marekani ambazo zinadaiwa zimeanza kutua kwenye Air Port ya Zanzibar na Dar kwa ajili ya kuimarisha usalama wa Rais wa nchi hiyo.

 Pia ndege maalum ya kivita itasindikiza Air Force One ya Rais Barak Obama

 
  Askari maalum wa kulinda ndege ya Rais

  Walinzi wa rais Obama kama wanavyoonekana
   Helkoper zitasambaa jiji zima la Dar kuanzi wiki hii hadi tarehe 2 Julai atakapoondoka Rais


 Mabodigadi wa Rais Obama wakiwajibika kama wanavyoonekana.

Na Livingstone Mkoi
Sasa kazi imeaaza ndivyo tunavyoweza kusema kwa sasa. Ambapo ndege na Helkoper za kijeshi toka Jeshi la Marekani zimeanza kuwasili ikiwa ni maandalizi tu ya kuimarisha ulinzi na usalama kwenye ujio wa Rais Obama.

Wakiongea na Xdeejayz baadhi ya maofisa wa Aripot walisema kuwa " Ndege zimeanza kuingia hasa nyakati za usiku ambapo tayari kuna Helkopter kadhaa zimeshuka usiku wa jana hapa Airpot ya Zanzibar na Dar hivyo kweli hali ya usalama ni kubwa sana" Alisema ofisa huyo

Aidha watafiti wa mambo wameiambia Xdeejayz kuwa ulinzi wa Obama umekuwa mkubwa kuliko wa Georg W.Bush ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita.  

OMMY DIMPOZ AKWEPA MAKOPO YA BONGO NA KUKIMBILIA MAREKANI:

 
Omary Fereji Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, amesaini mkataba na kampuni ya DMK Global Promotion leo hii kwa ajili ya tour atakayoifanya Canada na Marekani mwezi wa tisa mwaka huu baada ya kumaliza tour nyingine baran ulaya.

"yaah nimesaini mkataba na nitaondoka kwenda kwenye tour hiyo mwanzoni mwa mwezi wa tisa, imekuwa hivyo kwasababu tunasubiri mwezi mtukufu upite si unajua tena, kampuni niliyosaini nayo inaitwa DMK global promotion ambayo ni ya mtanzania ambae anaishi marekani." amesema Dimpoz

nilipomuuliza kuhusu mkwanja alioingiza kwa mkataba huo, Dimpoz aligoma kutaja kiasi na kusema 

"aaaah unajua tena kwa matatizo yaliyotokea nikitaja tena na mkwanja nilioingiza si ndio itakuwa matatizo kabisa?

Wednesday, June 26, 2013

NATASHA AFUNDWA: MASTAA WAKATA MAUNO MBAYA:



Baadhi ya waalikwa wakijiachia pamoja na Natasha (kushoto) wakati wa sherehe hiyo.
Na Imelda Mtema
HUKU siku za kufunga ndoa zikihesabika, mkongwe kwenye filamu za Kibongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ amefanyiwa sherehe ya kufundwa kabla ya kwenda kwa mumewe ambayo huko mitaani inajulikana zaidi kwa jina la singo.Shughuli hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Tandika Maghorofani, Dar ambapo iliandaliwa na shostito wa Natasha aliyejulikana kwa jina moja la Nuru.

APEWA SOMO
Natasha aliwekwa ndani kwa muda wa saa moja akipewa somo la ndoa na watu maalumu walioandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo kabla ya kutoka nje kuungana na wageni waalikwa.

Alipotoka nje, alikutana na waalikwa ambapo kati yao ni mastaa mbalimbali Bongo kisha wakaungana kwenye zoezi zima la kucheza ngoma.
KIASILI ZAIDI
Waalikwa walipata nafasi ya kupakwa urembo mbalimbali wa kiasili usoni na kuifanya hafla hiyo iwe ya kipekee kutokana na vivutio hivyo.
Baada ya yote hayo kukamilika, msafara wa kuelekea nyumbani kwa Natasha, Yombo ulianza huku ngoma zikiendelea kupigwa na mastaa mbalimbali wakikata mauno ndani ya gari.

Akizungumzia shughuli hiyo, Natasha alisema: “Nashukuru sana jamani kwa kupita hatua hii ya kwanza kuelekea kwenye ndoa yangu. Siwezi kuacha kumshukuru zaidi rafiki yangu Nuru kwa kunifanikishia.”

KAJALA AFUNGUKA KUHUSU BEEF LAKE NA WEMA SEPETU

 
Baada ya siku chache za magazeti ya udaku nchini kuripoti kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa karibu sana kati ya mwanadada Wema sepetu na Muigizaji mwenzake Kajala masanja, tuliamua kufanya uchunguzi wa kina ili kupata ukweli wa suala hili ili tusije kuipotosha jamii kwa habari za zisizo na ushahidi wowote.
Katika habari iliyoripotiwa na blogs na magazeti kadhaa ya udaku kuhusu kuvunjika kwa uhusiano huo zilisema kuwa chanzo ni vitendo vya mwanadada wema Sepetu “kumbania” Kajala kwenye dili anzopata za kucheza filamu na hasahasa kumkosesha dili ya kwenda china kufanya filamu aliyoalikwa na watanzania waishio nchini humo.
Bongomovies.com tuliamua kuwatafuta hewani wasanii hawa ili tuweze kupata ukweli wa jambo hili na mwanadada Kajala alikuwa wa kwanza kupokea simu na alikanusha vikali habari hizo na kuwashangaa wanaoziandika wanazipata wapi.
“Unajua mi nashangaa sana watu wanatoa wapi maneno wanayoandika, mimi sina tatizo na Wema, wala siwezi kuwa na tatizo naye, wema amekuwa msaada mkubwa kwangu, sa sijui nitagombana nini na wema, huo ni uzushi tuu jamani, muwe mnatuuliza kabla ya kuandika” Alisema kajala
Alipoulizwa kuhusu ukaribu wake mpya na wolper alisema
“Wolper nimekutana naye kwenye party ndo tukaamua kupiga picha, au siku hizi sitakiwi kupiga picha na mtu mwingine zaidi ya wema? Wolper ni rafiki yangu” Alisisitiza Kajala
Tulipojaribu kumtafuta wema simu yake ilikuwa haipokelewi na baadaye ilipokelewa na alisema yuko location anatengeneza filamu na mwigizaji Rado hivyo tumtafute baadaye

UJIO WA OBAMA DAR:ULINZI MKALI AIRPORT MADEGE YA JESHI YAANZA KUSHUKA

 

Dar es Salaam. Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini.
Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea.
Ulinzi haujawahi kutokea
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo.
Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa.
“Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa Rais huyo,” alisema Malaki.
Pia alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa kwa mwezi mmoja sasa na tangu wakati huo, maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa wakifika kwa nyakati mbalimbali.
“Sijawahi kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja marais wengi hapa nchini lakini ulinzi huu ni wa kutisha, sijui kwa sababu gani?” alisema Malaki.
Alisema awali, wakati maofisa hao walipoanza kuwasili nchini hawakutambua ni mgeni gani anayetarajia kufika lakini baadaye walipelekewa taarifa kuwa ni Rais Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa angetua saa 8.40 mchana, Julai Mosi.
Mkurugenzi huyo alisema Rais Obama atakuja na ndege nne, moja itakayombeba, ya pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi wa habari na maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura ambayo itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Malaki alisema maofisa wa Marekani wanaowasili nchini wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kuhakikisha kuwa hali ya usalama inaimarishwa na kuwaacha wazawa wakifanya shughuli za kawaida.
TOA MAONI YAKO HAPA

KAMANDA KOVA AONYA KUHUSU ULINZI WAKATI WA UJIO WA RAIS OBAMA!

 Kamanda Kova ameonya vikali kwa mtu au kikundi chochote kitakachothubutu kuvunja amani wakati huu wa ujio wa Rais Obama wa Marekani.
Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar imetoa angalizo kwa mtu yeyote atakaejaribu kuvuruga amani kuanzia wiki hii hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DAR LAKAMATA SHEHENA ZA PESA BANDIA, ZILIKUWA ZINAENDA KUWALIZA WAKULIMA MIKOANI!

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalu ya Dar es Salaam Bw. Sulemain Kova akionesha baadhi ya pesa bandia za noti zilizokamatwa na Jeshi hilo kwenye msako maalum wa kukata uharifu Jijini Dar unaendelea sasa.
 Kamanda  Kova akionesha bastora iliyokuwa inamikiwa na mwanamke aliyemtaja kwa jina la Grace huko Sinza na baadae ikaibiwa na watu wasiofahamika ndani ya gari yake baada ya kuvunjwa kioo. Hata hivyo silaha hiyo imekamtwa na Polisi ikiwa mikononi mwa majambazi 29 walionaswa na jeshi hilo. 
 

Picha zote na Livingstone Mkoi

POLISI JIJINI DAR WAKAMATA WATU WAWILI WAKIWA NA BASTOLA KATIKA PIKIPIKI..!!

 

Asklari kanzu akiwa na bastola alikamatwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer.

 Askari kanzu (kulia) akiwa ameshika bastola aliyokutwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usaji T 961 CJW katika mtaa wa Makunganya jirani kabisa na benki ya Posta jijini Dar es Salaam jana mchana . Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ujambazi wa kutumia pikipiki Polisi wameimarisha ulinzi na hasa katika maeneo ya mabenki.
 Watu waliokamatwa wakijaribu kuwasiliana na ndugu zao.
 Neno kwenye Pikipiki waliyokuwa wakitumia hao. 
 Ofisa wa Polisi akijaribu bastola waliyokutwa nayo watu wawiliwaliokuwa katika Pikipiki Posta Mpya jirani na Benki ya Posta leo.
 Heee ina risasi!
 Mtu aliyekutwa  na bastola hiyo, ambaye alijitambulisha kama mfanyabiashara.
 Polisi wakifanya mawasiliano na wenzao wa doria kuomba msaada wa gari.
 Mtuhumiwa aliyekutwa na bastola akihojiwa na kuchukuliwa maelezo.
 Dereva wa Pikipiki naye akichukuliwa maelezo yake.
Add caption
 Unaitwa nani, unaishi wapi, unafanya kazi gani, kabili gani, Ofisa wa Polisi akimuhoji mtuhumiwa.

Tuesday, June 25, 2013

MAULID WA KITENGE ATANGAZA NIA YAKE YA KUGOMBEA UBUNGE 2015 JIMBO LA UBUNGO


 
 
KILA LA HERI MAULIDI WA KITENGE TOKA ITV NA RADIO ONE KWA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UBUNGO 2015
KUPITIA CCM
SASA KUPITIA CCM KUNA;
- LYIMO
- PAUL MAKONDA

MSANII OMMY DIMPOZ ATETEWA NA MHADHIRI WA CHUO KIKUU: AMTETEA NA KUSEMA KILICHOMPONZA NI KUTOKUJUA KUJIBU MASWALI YA WAANDISHI WA HABARI.. SOMA HAPA




 

Huyu ni mhadhiri wa chuo kikuu cha mzumbe na pia ndio yule mwl wa chuo kikuu anayefanya bongo 

fleva.Ukitaka kumjua vizuri bofya hapa 






Yeye kama Msomi mzuri na mwalimu wa wasomi wa chuo kikuu,ameona kabisa Ommy Dimpoz hana 

makosa kabisa na amewaomba watanzania wamuelewe Ommy Dimpoz na kumsamehe.



Haya ndio maneno ya huyu mhadhiri wa chuo kikuu Issaya Lupogo jina la kisanii Lupojizo.


''Binafsi nasikitishwa sana na mashabiki kumfanyia Ommy Dimpoz mambo haya mabaya. Nilimsikiliza sana Ommy Dimpoz siku ya KTMA, hakumaanisha kama watu suku hizi wanavyotafsiri. Alichikisema Ommy kwa
namna nyingine kinaweza kutafsiriwa kama wadau na serikali zitoe kipaumbele na kuthamini kazi za wasanii wa nyumbani ili wasanii wanufaike zaidi na siku ya mwisho wasife masikini. Huu ni ukweli kabisa kuhusu hali iliyopo kwa wasanii sasa. Wasanii wananyonywa na kudhulumiwa, mwisho wa siku msanii anaishia kupata umaarufu tu usio na kitu chochote.
Kingine nilichokiona ni Ommy D kutotetea hoja yake pindi alivyohojiwa na waandishi wa habari, badala ya kueleza hoja hiyo kiumakini alijikuta aikbabaika na kukumbilia kuomba msamaha.

Jambo alilolisema Ommy D lilisemwa pia na Afande Selle na Mr. Sugu siku
 ya kuaga mwili wa Ngwair uwanja wa Jamhuri morogoro, kama ni hvo basi mbona hao hawakuandamwa kama Ommy D?

Watanzania tuwe waelewa,wasanii wengi wa Tanzania bado ni masikini, kipatao wanachokipata hakiendani na kazi wanayoifanya na umaarufu walionao, hii sio kwa Ngwear tu bali kwa wasanii wengi wa Bongo. Sababu ni unyonyaji na udhulumaji uliopo wa kazi za wasanii, na serikali kutoweka mkazo juu ya kuangalia maslahi ya wasanii nchini.
Nawaomba watanzania tusiendelee kumsakama Ommy D, na Ommy D naomba uwe unajaribu kujenga hoja vizuri kwa kile unachokisema na sio kukimbilia kuomba msamaha bila hata ya kutenda kosa lolote.''

MASIKINI MTOTO HUYU!!! AMEPOTEZA MAISHA KIKATILI SANA.

Hatua ya mwisho kabisa ya mateso ya Mtoto huyu

RIP Mtoto Mzuri.
Umeenda mahali ambapo watoto HUPENDWA na Kuheshimiwa.
Mama yake alimruhusu baba yake wa Kambo KUMBAKA
...
na kumpiga mpaka kufa. Alikuwa na miaka Minne (4)
tu. Aibakwa na kulawitiwa.
Please andika RIP' na Share' kusaidiana nami
kukemea uovu huu Ulimenguni mwote.
Kama haijakugusa Achana nayo (Ignore).

 


  •