TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, June 25, 2013

MSANII OMMY DIMPOZ ATETEWA NA MHADHIRI WA CHUO KIKUU: AMTETEA NA KUSEMA KILICHOMPONZA NI KUTOKUJUA KUJIBU MASWALI YA WAANDISHI WA HABARI.. SOMA HAPA




 

Huyu ni mhadhiri wa chuo kikuu cha mzumbe na pia ndio yule mwl wa chuo kikuu anayefanya bongo 

fleva.Ukitaka kumjua vizuri bofya hapa 






Yeye kama Msomi mzuri na mwalimu wa wasomi wa chuo kikuu,ameona kabisa Ommy Dimpoz hana 

makosa kabisa na amewaomba watanzania wamuelewe Ommy Dimpoz na kumsamehe.



Haya ndio maneno ya huyu mhadhiri wa chuo kikuu Issaya Lupogo jina la kisanii Lupojizo.


''Binafsi nasikitishwa sana na mashabiki kumfanyia Ommy Dimpoz mambo haya mabaya. Nilimsikiliza sana Ommy Dimpoz siku ya KTMA, hakumaanisha kama watu suku hizi wanavyotafsiri. Alichikisema Ommy kwa
namna nyingine kinaweza kutafsiriwa kama wadau na serikali zitoe kipaumbele na kuthamini kazi za wasanii wa nyumbani ili wasanii wanufaike zaidi na siku ya mwisho wasife masikini. Huu ni ukweli kabisa kuhusu hali iliyopo kwa wasanii sasa. Wasanii wananyonywa na kudhulumiwa, mwisho wa siku msanii anaishia kupata umaarufu tu usio na kitu chochote.
Kingine nilichokiona ni Ommy D kutotetea hoja yake pindi alivyohojiwa na waandishi wa habari, badala ya kueleza hoja hiyo kiumakini alijikuta aikbabaika na kukumbilia kuomba msamaha.

Jambo alilolisema Ommy D lilisemwa pia na Afande Selle na Mr. Sugu siku
 ya kuaga mwili wa Ngwair uwanja wa Jamhuri morogoro, kama ni hvo basi mbona hao hawakuandamwa kama Ommy D?

Watanzania tuwe waelewa,wasanii wengi wa Tanzania bado ni masikini, kipatao wanachokipata hakiendani na kazi wanayoifanya na umaarufu walionao, hii sio kwa Ngwear tu bali kwa wasanii wengi wa Bongo. Sababu ni unyonyaji na udhulumaji uliopo wa kazi za wasanii, na serikali kutoweka mkazo juu ya kuangalia maslahi ya wasanii nchini.
Nawaomba watanzania tusiendelee kumsakama Ommy D, na Ommy D naomba uwe unajaribu kujenga hoja vizuri kwa kile unachokisema na sio kukimbilia kuomba msamaha bila hata ya kutenda kosa lolote.''

No comments:

Post a Comment