TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, November 12, 2012

MZEE MAGALI KUOA MSICHANA WA KIMAREKANI!

Vikao vya harusi vitaanza siku yoyote kuanzia sasa.Ndoa kufungwa Marekani sherehe kufanyika Tanzania,Mastaa kibao wa filamu Afrika kuhudhuria!
Msanii nyota wa filamu Tanzania Charles Thobias Magali ametangaza ndoa yake na msichana wa Kimarekani ambae hakupenda kumtaja jina lake kwa madai kuwa bado mapema sana kumuweka wazi.

Akiongea na Xdeejayz Mzee Magali anaeongoza kucheza filamu nyingi za kushirikishwa nchini alisema kuwa" Ndugu mwandishi nimekuwa kimya muda mrefu sana kutokuwa na mchumba hali iliyoleta minong'ono kwa mashabiki wangu lakini sasa time imefika kuweka wazi kila kitu kuhusu maisha yangu ya kimapenzi" Alisema msanii huyo

Hata hivyo mzee Magali aliongeza kusema maandalizi ya harusi yake yameanza kidogo kidogo ambapo muda wowote vikao vitaanza kukaliwa hapa nchini na kule nchini Marekani nako pia vikao vitaendelea kama kawaida kwa upande wa ukweni.

Aidha msanii huyo alimalizia kusema msichana huyo hajawahi kukutana nae hata siku moja lakini amekuwa na ukaribu nae mwaka wa nne sasa wanachati huku wakiwa kwenye mapenzi mazito kiasi cha kila mmoja kuchanganyikiwa na mwenzake.

No comments:

Post a Comment