TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, November 12, 2012

MSANII NISHA WA BONGO MUVI ANUSURIKA KIFO KWA AJALI!


 Msanii  wa tasnia ya filamu bongo NISHA 
akiwa katika picha ya pozi.
 GARI ya msanii huyo kama inavyoonekana ikiwa nzima kabla ya kupata ajali mbaya  maeneo ya Masaki Jijini Dar es Salaam iliyopelekea msanii huyo kuumia vibaya!
 Hapa gari ya Nisha ikiwa haitamaniki baada ya ajali hiyo.
 Msanii NISHA akiwa amelazwa Hospitali baada ya kupata ajali mbaya na kuumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake!
 Mguu wa Nisha kama unavyoonekana ukiwa umejeruhiwa vibaya kutokana na ajali hiyo.
 Mguu wa Nisha kama unavyoonekana ukiwa umejeumia vibaya!


Msanii nyota wa filamu Tanzania Nisha weekend iliyopita alipata ajali mbaya iliyosababisha kunusurika kifo huku ikimuachia majeraha makubwa sehemu kadhaa za mwilini mwake.
Akiongea na Xdeejayz kwa taabu sana msanii huyo alisema kuwa ilikuwa mwishoni mwa juma alikuwa anatokea Location akiwa ba gari yake ndogo kama inavyoonekana hapo juu kwenye picha ndani yake alikuwa na wadogo zake wawili saa saba za usiku alipofika eneo moja maneo ya Masaki gafra akiwa anaendesha alihisi kiga kubwa mbele yake liliambatana na upepo wa ajabu ndipo gari ilipoacha njia na kudondoka.
Nisha aliongeza kusema alishangazwa sana na ile hali ambapo hakuwa amelewa labda angesingizia pombe lakini cha ajabu alikuwa mzima na hiyo hali ilikuwa ya kushangaza,Hata hivyo aliongeza kusema kuwa katika eneo hilohilo alilopata ajali masaa kadhaa mwanamuziki Diamond alikuwa amenusurika ajali kwa hali kama iliyokuwa imemtokea Nisha.
Msanii huyo amemshukuru Mungu kwa kumuokoa na kifo kwani kiukweli katika ajali hiyo asingepona mtu lakini anashukuru amepata majeraha ya kawaida tu ambayo anaamini yatapona haraka na kurejea kwenye hali yake ya siku zote na kuendelea na majukumu.

No comments:

Post a Comment