TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, October 30, 2012

NGOMA YA "KAMA NANI" KUMREJESHA KWENYE CHATI LUTEN KARAMA!


Mwanamuziki maarufu aliywahi kutamba kipindi cha nyuma akiwa ndani ya kundi la TMK Famili Karama Beker a.k.a Luten Karama huenda akarudi kwenye kiwango cha juu kwenye muziki baada ya wimbo wake mpya ujilikanao kwa jina la "Kama Nani" kuanza kusumbua kila kona ya Jijini.

Akiongea na paparazi wa Xdeejayz Karama alisema kuwa"Kaka nimerudi kwa nguvu na hii kwa kutokana na kupata mtu wa kuniongoza na kuniwezesha kwa kila jambo kuhusu muziki" Alisema mwanamuziki huyo

Aidha mwanamuziki huyo alielezea marengo yake kwa sasa"Nimeungana na mwanamuziki mwenzangu  Malipo ambapo bila shaka mashabiki wangu wanaujuwa uwezo wa Malipo hivyo tunatarajia kufanya mageuzi makubwa kwenye Indastri ya muziki wa kizazi kipya" Alimaliza kusema Luten

Hata hivyo paparazi wetu alibahatika kuongea na meneja wa Karama pamoja na Malipo aliyejitambulisha kwa jina la Zainabu Mfangavo alisema kuwa" Kwa mara ya kwanza hawa wanamuziki walifika sehemu ya biashara zangu huko maeneo ya Kinyrezi na wakanambia kama naweza kufanya nao kazi ambapo nilikubari kwani kabla  nilikuwa nawafahamu kama wanamuziki wazuri lakini kwa sasa kweli nimewashikiria mimi na natarajia kufany nao mambo makubwa tu kuhusu sanaa" Alisema Meneja huyo 

No comments:

Post a Comment