TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Sunday, October 28, 2012

WAHESHIMWA WABUNGE KUTIKISHA KWENYE UZINDUZI WA DTV DODOMA NOV.3 KWENYE UWANJA WA JAMHURI!

 MH. HEMED SHABIBY
 MH. ZITTO KABWE
MH. JOSEPH MBILINYI
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mji wa Dodoma na vitongozi vyake siku ya tarehe 3/11/2012 Waheshimiwa wabunge mbalimbali wanatarajia kuhudhuria uzinduzi wa kituo cha televisheni cha DTV kwenye tamasha kubwa lililopewa jina la "NI WAKATI WAKO TOUR"
Akiongea na Xdeejayz meneja wa tamasha hilo Hemed Kavu "HK" A lisema kuwa" Tunamapango wa kuwaalika waheshimiwa wetu  Wabunge katika uzinduzi huo utakaokuwa wa kihistori ndani ya Dodoma hivyo tunaendelea kufanya michakato hiyo" Alisema HK

Aidha Meneja huyo aliongeza kusema kuwa kwani nini wameamua kuwaalika wabunge hao" Tarehe ambayo tutafanya uzinduzi huo Waheshimiwa Wabunge watakuwa mjini Dodoma kwenye vikao vya Bunge na tarehe hiyo watakuwa wamepunzika hivyo tutakuwa nao kufurahi na wananchi wao" Alisema Meneja huyo.

Uzinduzi huo wa DTV unatarajia kuvunja rekodi ya matamasha yote yaliwahi kufanyka Mkoani humo hiyo inatokana na rundo la wanamuziki walioandaliwa kutoa burudani katika uzinduzi huo utakaofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri na unatarajia kuanza saa sita mchana hadi saa kumi na moja jioni.

No comments:

Post a Comment