TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, October 30, 2012

HOMA YA UZINDUZI WA DTV DODOMA YAANZA KUWAUMIZA VICHWA MASHABIKI WA MJI HUO!

Maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma kama wanavyoonekana katika viwanja vya Jamhuri!

Ikiwa siku zinahesabika kabla ya kufanyika lile tamasha kubwa linalosubiriwa kwa hamu na maelfu ya wakazi wa Mji wa Dodoma na vitongoji vyake Tarehe 3/11/2012 wakazi hao wameanza kupandwa na kimuhemuhe huku wakitamani siku zikimbie kama upepo ili lifanyike.
Wakiongea na mapaparazi wetu wakazi hao walisema kuwa wanaona kama siku haziendi vile ili kufikia tarehe tatu"Jamani mbona kama siku zinachelewa? Tunasubiri kwa hamu onesho hilo kwani licha ya wasanii wote wanakuja huju ni wazuri pia DTV ni Channel yetu vijana hivyo tutashiriki pamoja uwanjani" Alisema mwandada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Faudhia.

Hata hivyo wanafunzi mbalimbali toka Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM walisema kuwa" DTV wanatisha jamani tunasubiri Wakati wako Tour na sisi ili tu-"enjoy" Aidha katika hatua nyingine wakazi hao wameapa kufunika nyomi za shoo za zilizofanyika Jijini Dar es Salaam kwa kujitokeza kwa wingi huku.
Aidha meneja wa tamsha hilo lililoandaliwa na kampuni ya Entertainment Masterz Ltd Hemed Kavu 'HK'Aliiambia kona hii kuwa maandalizi yote yamekamilika kinachosubiriwa ni siku ya ishu tu" Kimsingi maandalizi yote yanaenda kama yalivyopangwa vijana wetu wa kujenga steji wameshaondoka tangu jana huku timu ya wanamuziki nao wakiondoka kesho" Alisema HK.

No comments:

Post a Comment