TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Sunday, October 28, 2012

MAUAJI YA KUTISHA SIKUKUU YA IDD!



Mke amchoma kisu cha kifuani mumewe hadi kufa,Yadaiwa chanzo ni mapenzi kinyume cha maumbile !

Wakazi wa Kinondoni Mkwajuni Jijini Dar Es Salaam wamshitushwa na tukio la kusikitisha na mauaji ya kinyama yaliyotokea maeneo hayo ya kijana wao aliyefahamika kwa jina la Seleman Ramadhan baada ya kuchomwa kisu na mkewe.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea sikuuu ya Idd usiku wa saa saba,Aambapo chanzo kikidaiwa ni wivu wa mapenzi pamoja na  mapenzi kinyume cha maumbile .

Wakiongea na  mapaparazi wa Xdeejayz wakazi wa maeneo hayo walisema kuwa tukio hilo limewashtua sana lakini pamoja na yote kuna uzembe ulitokea wa kuchukuwa tahadhari kabla ya mauji hayo kufanyika.

Wakazi hao waliongeza kusema kabla ya tukio hilo mwanamke huyo alikuwa ametoa taarifa kwa baba wa mumewe anaeishi maeneo ya Magomeni Moroco  aliyefahamika kwa jina la Ramdhani kuwa hamtaki mwanae asimfate fate la sivyo atamchoma kisu" Yani ni kweli kwamba huyo mwanamke alifika nyumbani kwa mkwe na kuwaeleza kuwa hamtaki mtoto wao hivyo siku hiyo asimfatilie la sivyo atafanya mauaji ya kutisha kwa kumchoma moto"  Walisema wakazi hao na kuomba hifadhi ya majina yao

Hata hivyo ipofika saa saba usiku mwanamke huyo ambae hakufahamika jina lake alifika tena nyumbani kwa mkwewe akiwa amelowa damu na kumueleza baba mkwe wake kuwa kazi aliyokuwa amemwambia amemaliza hivyo akachukuwa maiti yake, Kutokana na mwanamke huyo kulowa damu mwili mzima wanafamilia hao walikwenda mbio na kumkuta mtoto wao akiwa ameshapoteza maisha.
Aidha mapaparazi wetu walimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni Charles Kenyela ili aelezee tukio hilo ambapo hakuweza kupatikana hewana hata hivyo Xdeejayz inahidi kufatilia sakata hilo na baadae itawajulisha wasomaji wetu.

No comments:

Post a Comment