TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Tuesday, October 23, 2012

ARUSHA,MWANZA WALILIA SHOO ZA WAKATI WAKO TOUR KUFIKA HUKO!
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua mashabiki mbalimbali toka mikoani wamejitokeza na kutaka shoo za NI WAKATI WAKO TOUR zilizofanyika Jijini Dar katika viwanja vya PT Sinza na Temeke Mwembe Yanga pia ziende kufanyika katika mikoa yao ili wapate burudani.
 
Wakitoa maoni yao kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii mashabiki hao walisema wanavutiwa sana na maonesho ya tamasha hilo linaloandaliwa na kituo cha televisheni cha DTV chini ya kampuni ya Entertainment Masters Limited "EML" hivyo wanaomba waandaji hao kuwafikiria juu ya hilo.
 
Aidha mashabiki wa Mkoa wa Mwanza ambao wanaitizama DTV kupitia Startimes walisema kuwa" Ni ukweli usiopingika DTV wanatisha tunashuhudia maonesho ya huko Dar hivyo tunaomba waratibu watuletee na sisi burudani hiyo huku Mwanza kwani DTV ndo tv ya wananchi wa huku si majumbani, kwenye mabaa, Saloon, Madukani maofisini kote watu wanatizama televisheni hiyo ya ukweli" Alisema mmoja wa wakazi wa Konabwilu Jijini Mwanza aliyejitambulisha kwa jina la Masanja Machichi.
 
Hata hivyo si Mwanza pekee bali mikoa mingi imeomba shoo hizo ikiwemo Arusha, Mbeya, Zanzibar na Singida ambako kote huko wanaitizama DTV kupitia king'amuzi cha Startimes.
Akiongea na mapaparazi wa Xdeejeyz Meneja Mkuu wa kampuni ya Entertainment Masters Limited "EML" Geofrey Ndaula alisema" Ni kweli mashabiki mikoani  wanahitaji kufikiwa na shoo zetu na sisi kama kampuni tunajipanga  ili kuwafikia lakini nadhani hilo halina shida tutahakikisha kote huko mapinduzi haya yanayoendelea kufanyika Jijini Dar  huko nako yatafika kwani ndo malengo yetu kuleta mabadiriko kama haya ya burudani katika ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati" Alisema meneja huyo. 
 


No comments:

Post a Comment