TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, October 12, 2015

ZANZIBAR KWALIPUKA MOTO, WATU WAHAHA KILA KONA, WENGI WASHINDWA KUAMINI MACHO YAO, JESHI LA POLISI LAENDELEA NA MSAKO MKALI ILI KUBAINI WANAOHUSIKA, ANGALIA TUKIO HILI..!


 Msanii Manaika Sanga akiwa na mashabiki wake walimuomba wapige picha nao huko Zanzibar ambako yupo kuangalia mwenendo wa  mauzo ya filamu yake Iitwayo Wake Up  pamoja na kuwasaka wezi wa kazi za wasanii kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoani humo
Mmoja wa mashabiki wa Manaiki akiwa kwenye picha ya pozi
 Msanii Manaika Sanga akiwa na shabiki wake

 Msanii Manaika Sanga akiwa na mashabiki wake ambao ni wapemba wakifurahia baada ya kumuona msanii huyo live, Manaiki Sanga amejichukulia umaarufu mkubwa na heshima baada ya kutoka kwa filamu ya Wake Up




Msanii Manaika Sanga wiki iliyopita alizikonga nyoyo za mashabiki wake huko Zanzibar baada ya kufanya ziara ya kushtukiza huku umati mkubwa wa watu ukimsonga japo kumshika mkono pamoja na kupiga nae picha za ukumbusho.
Manaiki Sanga ambae toka kwenye mtandao wake wa kijamii anasema kuwa bado anaendelea na msako kwa wezi wa kazi za wasanii ambapo amekuwa akifanya kimya kimya ili kubaini kama kuna watu au mtu atakuwa anahujumu mauzo ya kazi yake mpya ya Wake Up filamu ambayo hadi sasa imevunja rekodi baada ya kuuza nakala nyingi kuliko filamu yoyote.
Aidha msanii huyo aliendelea kutoa angalizo kwa wezi wa kazi za wasanii na kusema msako mkali bado unaendelea kushirikiana na maofisa wa Jeshi la Polisi ambao amekuwa akizunguka nao kila mahara na kama watafanikiwa kumkamata mtu basi huyo jela ina mwita

Sunday, October 4, 2015

KUELEKEA UCHAGUZI MKUUU KINONDONI YAWAKA MOTO, AFANDE HUYU AKINUKISHA KILA KONA VIBAKA, WEZI WATAFUTA PA KUTOKEA WENGINE WAAMUA KUWA WAJASIRIAMALI, WANANCHI WAMPONGEZA..!

Mkuu wa kitengo cha Oparesheni ya kupambana na uharifu Kinondoni Swai Jakob Swai akiwa kazini
 Waharifu mbalimbali waliokamatwa wakiwa chini ya ulinzi mkali, pongezi kubwa kwa Swai ya kujitoa kwa ajiri ya kuwasaidia wananchi.
 Swai Jakob Swai akiwa mbele ya Kito cha Polisi Oysterbay Polisi hivi karibuni.
Na Livingstone Mkoi
Wakazi wa Kinondoni meneo tofauti tofauti wamejitokeza na kumpongeza Askari shupavu mwenye nyota mbili aliyefahamika kwa jina la Swai Jakobu kwa kazi nzuri anayoifanya ya kupambana na uhairifu wa vibaka pamoja na uharifu mwingine kiasi cha kuwafanya kwa sasa wananishi kwa amani.
Wakiongea na gazeti hili watu hao walisema" Jamani kiukweli ni lazima tushukuru huyu Afande Swai amekuwa msaada mkubwa sana kwetu hizi patro anazozifanya mara kwa mara zimekuwa msaada mkubwa sana kwetu" Alisema mmoja wa wakazi wa Kinondoni Mkwajuni aliyefahamika kwa jina la Mama Zai ambae ana miliki Salooni
Aidha wananchi wengine  waliongeza kusema kuwa Afande huyo ambae ni kipenzi cha watu ila ni adui wa mkubwa wa waharifu " Huyu Afande anaijua kazi yake vizuri na huwa hataki masihara awapo kazini ndiyo maana unaona hata vibaka wengi wameamua kuacha kuiba au kuvuta unga kwani huyo jamaa akikukamata hana msalie mtume ni moja kwa moja mahakamani kisha jela, hivyo uadilifu wake umesaidia sana kuondoa uharifu kwa kweli" Alisema Mwita ambae ni askari Jeshi Mstaafu mkazi wa Msasani

Friday, October 2, 2015

MWANAMKE ALIYEBAKWA : WATANZANIA JAMANI MSAIDIENI MAMA HUYU NA MUNGU WOTE WA MBINGUNI ATAWABARIKI NA KUWAONGEZEA NA KUBARIKI KAZI ZA MIKONO YENU, MSANII MANAIKI SANGA AFUNGUA NJIA..!

 Mama huyu ambae kwa sasa anaishi kwenye jumba bovu la Tanganyika Packers  huku akiwa na mtoto mchanga mwenye siku 50 huku mwanae mwingine akiwa na mwaka mmoja.
  Mkuu wa kitengo maalum cha habari za uchunguzi katika kituo cha E-fm Radio Bw Livingstone Mkoi akiwa kwenye kajichumba anakolala mama huyo na kichanga chake baada ya kubakwa
 Hapa msanii na mkurugenzi wa kampuni ya Manaiki Production Manaiki Sanga akimkabidhi mama huyo kiasi cha fedha laki mbili kama msaada wake baada ya kuguswa na tukio hilo


Msanii Manaiki Sanga akiwa amemshika mtoto mkubwa wa dada huyo huku kichanga kikiwa kimelala chini ambapo watoto wote wapo chini ya umri wa mwaka mmoja.
Mwananchi mwingine ambae aliguswa na tukio hilo akitoa chochote kitu kwa mama huyo japo siku ipite.
Na Mwandishi Wetu.
Watanzania mbalimbali Duniani na Jiji la Dar wameombwa kuendelea kumtolea kitu chohcote dada anaishi kwenye jengo la Tanganyika Packers baada ya kukosa mahara pa kuishi huku akiwa na kichanga cha umri wa siku 5.
Mama huyo ambae aliibuliwa na kituo cha E-fm Radio kupitia kipindi cha Ubaoni kwenye Ripoti ya leo ambae alitokea jijini Mwanza alikokuwa anaishi na mumewe baada ya kulazimishwa na dadaake kuolewa hivyo hivyo baada ya maisha kuwa magumu.
Akiwa amejifungua mtoto wa kwanza kwa mumewe huyo akiwa na mwezi mmoja tu mwanaume huyo alianza kumuingilia kinguvu dada huyo bila kujari mtoto akiwa bado mdogo mwanaume huyo amabae ilidaiwa ni mlevi  alikuwa anambaka  hadi mwanamk huyo alipoamua kukimbia mwanza na kuja Dar na kufikia kwenye jengo hilo la Tanganyika Packers  japo ajihifahi kwa muda wakati akisubiri hatma yake ya maisha.
Dada huyo anasema baada ya kuka kwa kipindi flani alihisi ni mjamzito kumbe kule kubakwa na mumewe tayari alikuwa ameshanasa mimba bila yeye kujua kama nadipo hadi juzi alipojifungua bila msaada wowote huku kichanga hicho na mwanae wa kwanza ambae pia ni mdogo wakiwa mazingira sio salama huku waking'atwa na mbu usiku kucha kwa kukosa neti ya kuzuia mbu.
Kama umeguswa kwa mkasa huu wa mtanzania mwenzetu popote ulipo unaweza kumsaidia kupitia namba hii ya simu ya 0713-575718 na Mungu atakubariki. Namba hii ni ya kituo cha E-fm Radio

UKAWA WATIKISA JIJI LA DAR, WAPIGA MIKUTANI MITANO KWA SIKU MOJA, MAELFU YA WANANCHI WAPAGAWA NA SERA ZAKE, BODABODA WAPATA NAFUU YA MAISHA..!


.
.
Toka tarehe 29 August ulipofanyika uzinduzi wa kampeni Ukawa bado wameendelea kusogea sehemu mbali mbali za kuwafikia wananchi na leo Octoba 1, 2015 ilikuwa ni zamu ya wakazi wa jimbo la Kawe Dar es Salaam  katika uwanja wa Tanganyika Peakers Dar es Salaam.
Ni wajibu wangu kukusogezea kila kinachonifikia na hapa nimekuwekea picha za mkutano mtu wangu.
.
Mgombea Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa akiongea na wananchi wa jimbo la Kawe Dar es Salaam.
.
.
.
.
.
.
.
Mwanasheria Tundu Lissu akizungumza na wananchi leo Octoba 1, 2015.
.
.
.
Mbunge John Mnyika akizungumza na Wananchi.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Mwenyekiti wa NCCR, James Mbatia akizungumza na wananchi.
3X6A0041

.
Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), Freeman Mbowe.
.
.
.
.
.
.
.
.
Unaweza uka bonyeza play kusikiliza kile kilichozunguzwa kwenye mkutano wa UKAWA jimbo la Kawe Octoba 1, 2015

Wednesday, September 23, 2015

MWANAMUZIKI MUDY KIBERITY AMFANYIA UMAFIA WA KUTISHA DIAMOND PLATNUM, SIASA ZAMPONZA MASHABIKI WASAMBARATIKA WENGINE WAAPA KUTOKUWA SHABIKI WAKE TENA..!

Mwanamuziki Muddy Kiberity  wa bongo flava

Wimbo wa  Muddy Kiberity uitwao Kwanza Pesa MAPENZI BAADAE.

Mwanamuziki Diamond ambae kwa sasa amewagawa mashabiki wake baada ya kuonekana kuegemea upande mmoja wa chama flani na kupiga nae kampeni.
Na Mwndishi Wetu  
Mwanamuziki wa Bongo Flava aliyefahamika kwa jina la Muddy Kiberity amefanikiwa kuwanyakua mashabiki wote wa mwanamuziki Diamond baada ya kujiingiza kwenye ushabiki wa kisiasa.
Wakionge na kwa nyakato tofauti mashabiki hao wamsema kuwa mwanamuziki Muddy anakipaji zaidi ya Diamond kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao wa kuimba huku sauti yake ikiwa balaa kwa mvuto.
Hata hivyo mwanamuziki huyo mwenyewe alisema kuwa amefurahishwa na mashabiki hao kukubari kwa vile ameweza kutoa wimbo uliokubarika huku akitamba mziki wake ni mzito kwa sasa Diamond asitie maguu ataumia.
Wimbo wa mpya wa mwanamuzki huyo Uitwao Kwanza Pesa Mapenzi Baadae umeanza kuchezwa kwa fujo kwenye vituo vyote vya radio kiasi cha kushika kwenye chati mbalimbali huku mashabiki wengi wakiuomba upigwe mara kwa mara kutokana na ubora wake 

Friday, September 18, 2015

FILAMU YA GOING BONGO YAZIDI KUTISA DUNIA, WAINGEREZA WAPONGEZA MTANZANIA ERNEST NAPOLEON WASEMA TANZANIA INATAKIWA KUJIVUNIA KWA KIPAJI CHAKE..!-

 Staa wa filamu ya Going Bongo Ernest Napoleon akiwa pamoja na wasanii wengine..!
  Staa wa filamu ya Going Bongo Ernest Napoleon akifafanua jambo  kwenye mkutano na waandishi wa habari hwapo pichani..!
 Ernest Napoleon akiwa pamoja na wasanii wengine wa bongo movie










Filamu ya Going Bongo imeendelea kuwa gumzo duniani kote kutokana na kuigizwa kwa kiwango cha juu huku nchi ya Tanzania ikipata sifa kede kede kutokana na sinema hiyo kuigizwa na raia wa Tanzania aishie nchini,
Sinema hiyo wiki mbili zilizopita ilionshwa tena kwa mara ya pili nchini Uingereza katika mji mwingine na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu huku mabalozi toka nchi mbalimbali wakihudhuria kuishuhudia sinema hiyo matata ambayo kwa sasa inapatikana nchini.