Mama huyu ambae kwa sasa anaishi kwenye jumba bovu la Tanganyika Packers huku akiwa na mtoto mchanga mwenye siku 50 huku mwanae mwingine akiwa na mwaka mmoja.
Mkuu wa kitengo maalum cha habari za uchunguzi katika kituo cha E-fm Radio Bw Livingstone Mkoi akiwa kwenye kajichumba anakolala mama huyo na kichanga chake baada ya kubakwa
Hapa msanii na mkurugenzi wa kampuni ya Manaiki Production Manaiki Sanga akimkabidhi mama huyo kiasi cha fedha laki mbili kama msaada wake baada ya kuguswa na tukio hilo
Msanii Manaiki Sanga akiwa amemshika mtoto mkubwa wa dada huyo huku kichanga kikiwa kimelala chini ambapo watoto wote wapo chini ya umri wa mwaka mmoja.
Mwananchi mwingine ambae aliguswa na tukio hilo akitoa chochote kitu kwa mama huyo japo siku ipite.
Na Mwandishi Wetu.
Watanzania mbalimbali Duniani na Jiji la Dar wameombwa kuendelea kumtolea kitu chohcote dada anaishi kwenye jengo la Tanganyika Packers baada ya kukosa mahara pa kuishi huku akiwa na kichanga cha umri wa siku 5.
Mama huyo ambae aliibuliwa na kituo cha E-fm Radio kupitia kipindi cha Ubaoni kwenye Ripoti ya leo ambae alitokea jijini Mwanza alikokuwa anaishi na mumewe baada ya kulazimishwa na dadaake kuolewa hivyo hivyo baada ya maisha kuwa magumu.
Akiwa amejifungua mtoto wa kwanza kwa mumewe huyo akiwa na mwezi mmoja tu mwanaume huyo alianza kumuingilia kinguvu dada huyo bila kujari mtoto akiwa bado mdogo mwanaume huyo amabae ilidaiwa ni mlevi alikuwa anambaka hadi mwanamk huyo alipoamua kukimbia mwanza na kuja Dar na kufikia kwenye jengo hilo la Tanganyika Packers japo ajihifahi kwa muda wakati akisubiri hatma yake ya maisha.
Dada huyo anasema baada ya kuka kwa kipindi flani alihisi ni mjamzito kumbe kule kubakwa na mumewe tayari alikuwa ameshanasa mimba bila yeye kujua kama nadipo hadi juzi alipojifungua bila msaada wowote huku kichanga hicho na mwanae wa kwanza ambae pia ni mdogo wakiwa mazingira sio salama huku waking'atwa na mbu usiku kucha kwa kukosa neti ya kuzuia mbu.
Kama umeguswa kwa mkasa huu wa mtanzania mwenzetu popote ulipo unaweza kumsaidia kupitia namba hii ya simu ya 0713-575718 na Mungu atakubariki. Namba hii ni ya kituo cha E-fm Radio
No comments:
Post a Comment