TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, May 26, 2014

ANGALIA VITUKO VYA NDOA YA KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN JANA, ILIKUWA BALAA TUPU BEYONCE AWA WA KWANZA KUPOST PICHA HIZI...!


article-2638252-1E26AF4500000578-868_634x565
Kim Kardashian amekuwa Mrs. West rasmi leo baada ya kufunga ndoa na Kanye West.Mastaa hao wamefunga pingu za maisha kwenye harusi private iliyofanyika juu ya mlima Fort di Beleverdre huko Florence, Italia mbele za ndugu na marafiki zaoHata hivyo marafiki wakubwa wa Kanye, Jay Z na mke wake Beyonce hawakuwepo kwenye harusi hiyo.
Awali ilisemekana kuwa Jay Z angekuwa mpambe wa Kanye kwenye harusi hiyo kwakuwa wawili hao ni marafiki wa karibu. article-2638252-1E2BCD2D00000578-859_634x605Beyonce alipost picha hii muda ambao Kanye na Kim walikuwa wakifunga ndoa

WEMA, AUNT EZEKIEL CHUPUCHUPU KUBAKWA ANGALIA TUKIO HILI LA KUSHTUA ILIBAKI KIDOGO TU JAMAA ANANIHII...!


Mastaa wawili wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wakiwa katika Msiba wa Adam Kuambiana.
Mastaa wawili wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel walikipata cha moto walipokuwa kwenye msiba wa Adam Kuambiana, Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar, baada ya kutukanwa na njemba mmoja aliyekuwa amelewa.
Sakata hilo lilijiri usiku mwingi wakati  mastaa hao walipokuwa wameenda kulala kwenya matanga ambayo yalihudhuriwa na mastaa kibao, nyumbani kwa mke wa marehemu
Mwanaume mmoja (jina lake halikupatikana) alianza kumtukana Wema kuwa hana uzuri wowote kama walivyokuwa wakimuona kwenye runinga.
Kitendo cha njemba huyo, kilimkera Wema na kuanza kujibishana naye, Aunt akaununua ugomvi na kujikuta naye akitemewa mbofumbofu.
Hata hivyo, mwisho wa sakata hilo Wema na Aunt waliamua kunyamaza kwani walibaini kuwa walikuwa wakijibishana na mtu ambaye ‘network’ yake ilikuwa bize kwa gambe.

Friday, May 23, 2014

NAY WA MITEGO NA MCHUMBAAKE WAGAWANA KILA KI2 HADI VIJIKO SASA HIVI KILA M2 KIMPANGE MANAIKI AHUSIKA KUVUNJA UCHUMBA WAO..!


picccMiongoni mwa mabalozi wapya kutoka mtandao wa Airtel ni pamoja na Ney wa mitego,stori ambayo imemfikia Soudy Brown ni kwamba mpenzi wake ametaka kugawana vitu na Ney wa Mitego ambavyo amevipata wakiwa pamoja,maongezi ya Ney wa Mitego alipoulizwa na Soudy Brown juu ya tuhuma hizi kama ni za kweli hiki Nay hakuweka bayana ingawa kuna taarifa toka kwa watu wao wa karibu kuwa msanii Manaiki Sanga the don anahusika na kuvunjika kwa uchumba huo.

MZEE ALIYEFUMANIWA ASEMA USIOMBE KUFUMANIWA NA WAANDISHI WA MAGAZETI PENDWA KWANI HAWA HURUMA HATA KIDOGO TIZAMA HAPA...!


Amakweli dunia imekwisha! Watu wa Dar es Salaam wanasema uzee mwisho Chalinze, Dar es Salaam kila mtu baby, kauli hiyo ilitimia usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita baada ya mmiliki wa Gesti ya GLP ya Mabibo Mwisho jijini Dar es Salaam, Amos Makelle kunaswa kitandani usiku wa manane na mfanyakazi wake aitwae Tina.



Babu Amos Makelle baada ya kunaswa akiwa kitandani  na mfanyakazi wake aitwae Tina wakiwa tayari kuchepuka.
Bosi huyo na mfanyakazi wake walinaswa na mchumba wa Tina aitwae Salum Mbonde ambaye alipenyezewa umbeya huyo na mteja mmoja aliyekodi chumba kwenye gesti hiyo kwa ajili ya kufuatilia nyendo za wawili hao.
Baada ya mchumba wa Tina kupewa umbeya huo kuwa wawili hao walikuwa katika harakati za kuchepuka aliwawekea mtego na kuwashirikisha waandishi wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na askari wa doria.
BOSI ATOA SHINGO KUCHUNGULIA NOMA
OFM na mchumba wa Tina wakiwa wamelizingira eneo la gesti hiyo mishale ya Saa 8:17 usiku kukiwa kumetulia tuliii... mtonyaji aliyekodi chumba kwa ajili ya kazi maalum aliwatumia ujumbe mapaparazi wa OFM kuwa mzee Makelle aliyekuwa kwenye chumba chake alitoa shingo kama mara tatu na kuangalia kulia na kushoto kama kulikuwa na mtu aliyemuona.

Babu Amos Makelle bada ya kufumwa akiwa na mfanyakazi wake gesti.
APIGA HATUA ZA KUNYATA
Ilipotimu saa 8:31, Mzee Makelle akiwa tumbo wazi na kipensi chake aliangalia tena kama hakukuwa na noma, akachomoka chumbani kwake fastafasta kwa hatua za minyato na kuzama chumba namba 104 alimokuwa Tina.

SHAAABASH... WANASWA KITANDANI
Shaaabash... baada ya dakika chache OFM na mchumba wa Tina walizama kwenye chumba hicho na kuwakuta wawili hao wakiwa kitandani huku Tina akiwa na nguo za ndani.

Walipohojiwa na OFM Tina alikuwa akilia na kumuomba radhi mchumba wake na kusema bosi wake huyo ndiye alimshawishi kuchepuka naye aliona kitendo cha kumnyima kingesababisha apoteze ajira yake ambayo anaitegemea.
Mzee Makelle alipohojiwa, katika hali ya kustaajabisha baada ya kujitetea alianza kumchongea Tina kwa mchumbaake akidai si mwaminifu.


Chondechonde: Babu akiomba msamaha kutoka kwa makachero wa OFM.
“Wewe kama huyu ni mchumba wako hilo mimi nilikuwa silijui, lakini huyu mwanamke juzi tu kalala na mwanaume mwingine palepale gesti na kama unabisha twendeni nikawaoneshwe kitabu cha wageni muone jina lake na la huyo bwana,” alisema mzee huyo.
Waungwana waliokuwa wakimsikiliza mzee Makelle walimtafadhalisha kutozungumza maneno ya kichochezi na kumtaka ajitete mwenyewe.
Baada ya sakata hilo kijana huyo alimchukua mchumba wake na kuondoka naye ambapo OFM ilifuatilia na kubaini kuwa bado msichana huyo anaendelea kufanya kazi kwenye gesti hiyo.
Endapo mfanyakazi huyo atafukuzwa kazi na bosi wake baada ya kufumaniwa OFM inaiomba serikali kuingilia kati ili mwanamke huyo apate haki zake kwani bosi huyo awali alikuwa akisema huenda katika mchongo wa kumnasa Tina anahusika.
CDT:GPL

AIBU KUBWA, MSANII JB NA STEVE NYERERE WAZICHPA JB APIGWA NGUMI TISA ZA TUMBO NA KUSHINDWA KUPUMUA KISHA AKAPIGWA TEKE LA KOLODANI NA KUDONDOKA CHINI TUKIO LATOKE BAA, XDEEJAYZ LIVE..!

 Msanii Jb
Msanii Steve Nyerere
Na Livingstone Mkoi
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua wasanii Jakob Steven Jb na Steve Magele Nyerere wamepiga nguvu kavukavu karibu na eneo la msiba wa marehemu Adam Kuambiana huko Bunju huku kisa kikiwa kugeukana kwenye dili la matangazo.
Habari za uhakika zilizotua mezani kwa Maskanibongotz zilisema kuwa msanii steve nyerere ndiye aliyeanza kumchokoza msanii Jb kwa kumchana baada ya kumgeuka kwenye mchongo wa matangazo ya kampuni moja ya simu iliyopo maeneo ya Moroco  Jijini Dar.
Habari zaidi zilisema wakati wasanii hao wakiwa baa wanakula kijala siku moja kabla ya mazishi ya msanii mwenzao Steve alimvamia Jb na kuanza kumchana na kumueleza jinsi alivyokuwa na roho mbaya kwa kumgeuka kwenye mchongo wa mtangazo ya simu pale Moroco na kusema ndiyo maana anaroho mbaya.
Majibizano hayo yalidumu kwa muda mrefu sana huku Jb akiwa kimya kwani stevu alionekana kuumizwa na jambo hilo kwani inadaiwa zile picha za Jb kwenye mabango ya mtandao huo wa simu mchongo alipewa na steve lakini baadae Jb alimgeuka na kwenda kupiga mchongo kimaya kimya na kumuacha Steve akishangaa.
Hata hivyo Steve aliendelea kusasambua Jb mbele ya watu hali hiyo ilimfanya Jb kunyanyuka na kuanza kufokea nae huku akimtahadharisha kama atamfinyangafinya na ufupi wake ndipo steve nyerere aliyekuwa ameshika chupa ya kilaji aliruka kichwa kimoja kilichompiga Jb kifuani na kupepesuka.
Wakati watu akijianda kwenda kuamulia basi Steve ambae aliwahi kucheza ngumi miaka ya nyuma alimshindilia Jb ngumi kama tisa za harakaharaka sehemu ya tumbo iliyomfanya Jb kudondoka chini na kushindwa kupumua kwa  dakika tano  kisha alinyanyuka na kukalia kiti.
 Maskanibongtz iliwasiliana na wasanii hao ili kupata ukweli wa mambo lakini kwa bahati mbaya simu zao hazikupekelewa na bado tunawatafuta.
Source: Maskanibongotz.

Thursday, May 22, 2014

MSANII HUYU ATOA MPYA, ASEMA ANAPENDA KUMLA DENDA MPENZI WAKE KABLA HAJAPIGA MSWAKI ASUBUHI SANA, ADAI ANAPENDA RADHA YA UCHACHU MMH HII KALI TIZAMA MWENYEWE UJIONEE..!


Msanii wa kizazi kipya anayejulikana kwa jina la Jaco Beats A.K.A Kilaza na pia ni Msanii wa kwanza ktk Mkoa wa Dodoma anayefanya  vizuri kwa wimbo wake mpya wa ''WALIONUNA'' ambaye Video ya wimbo huo ukiwa unakaribia kutoka hivi karibuni.Pia msanii Super nyota aliyewakilisha mkoa wa Dodoma katika tamasha la fiesta 2013 kwa wimbo wake wa ''KILIAZA'' Ambapo kwa sasa anafanya poa sana kwenye Game:
Masanii huyu siku ya leo amepost Picha kwenye Ukurasa wake wa Facebook akiwa na Msichana ambaye inasadikika na Mpenzi wake.... Baadhi ya watu wake wa karibu walifunguka na kudai msaniii huyo kwa sasa hajiwezi kwa manzi huyo yani mapenzi yao ni kama ya Dj Hunter na Snura yani wanamaanisha Mahaba Niuwe nipeteze kama Ndege ya Maleysia





ANGALIA TUKIO LA NAIBU WAZIRI WA MITAA ALIVYOJINYONGA NYUMBANI KWAKE, KISA KINASIKITISHA TIZAMA HABARI HII ..!








Aliyekuwa waziri wa serikali za mitaa Malawi amejiua baada ya kupata taarifa za kushindwa uchaguzi mkuu.Kifo chake kimetokana na kujipiga risasi akiwa nyumbani kwake.


A Malawian minister has killed himself, police say, as results are still awaited from Tuesday's general elections.
Outgoing deputy Local Government Minister Godfrey Kamanya shot himself in his home, according to police.
His spokesman denied reports that his suicide was linked to him apparently losing his parliamentary seat.
Official results have not yet been declared in what was expected to be a tight presidential race.
The BBC's Raphael Tenthani in Malawi says the electronic counting system has broken down in some areas and votes are being collated manually in these places.
Mr Kamanya left a suicide note at his home in the capital, Lilongwe, asking President Joyce Banda to take care of his daughter and provide for her education, our reporter says.
Eleven candidates ran against Mrs Banda, but her main challenger is Peter Mutharika, the brother of former President Bingu wa Mutharika.
The Malawi Election Commission (MEC) will announce
results when 30% of votes have been counted, its chairman Maxon Mbendera said on Wednesday.
The MEC was "not anywhere in the neighbourhood" of that figure, he added.
Counting was being done manually because the electronic system was "refusing to take the information from the ground where our data clerks are stationed to send the results," chief elections officer Willie Kalonga told the AFP news 
My take: 2015 tutegemee mengi kwa mawaziri na manaibu waziri kujinyonga baada ya matokeo kuwa tofauti na mategemeo yao.
Source: BBC Swahili, Habari Zilizotufikia hivi punde