TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, September 30, 2013

BONDIA WA KIMATAIFA FRANCIS MIYEYUSHO ASHAURIWA KUACHANA NA MAPAMBANO YA USWAHILINI KWANI YANASHUSHA HADHI YAKE!

Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Miyeyusho wakati wa mpambano wao usiokuwa wa ubingwa uliofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa  Friends Coner  Manzese Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa pointi.
Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Miyeyusho wakati wa mpambano wao usiokuwa wa ubingwa uliofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa  Friends Coner  Manzese Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa pointi.
refarii Sako Mtlya akimnyoosha mkono juu bondia  Fransic Miyeyusho baada ya kumgalagaza Bondia Sadiki Momba wakati wa mpambano uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Friend Conner Manzese.

SOMA KISA CHA MAMA ALIYEZITAFUNA NYETI ZA MWANAE KISHA KUZIMEZA!

  MKAZI wa Kijiji cha Mlongazila, wilayani Kisarawe, Pwani, Moshi Hamad anatuhumiwa kumng’ata mwanaye, Khadija Hamad (6) sehemu za siri kwa madai ya kujisaidia haja kubwa na ndogo hovyo.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima juzi wilayani Kisarawe, wakazi hao walisema mama huyo amekuwa na tabia ya kumfungia ndani mtoto wake huyo na kumchapa kwa zaidi ya nusu saa, akitumia nyaya za simu na kumng’ata sehemu mbalimbali za mwili zikiwamo za siri na kumsababishia maumivu makali.
  Wakazi hao walisema waliamua kutoa taarifa kwenye dawati la haki za binadamu baada ya kuchoshwa na vitendo hivyo, na sasa wamelitaka Jeshi la Polisi kumkamata mama huyo na kumchukulia hatua.
  Stella Musa, alisema sehemu za siri za mtoto huyo zimeharibiwa kutokana na kung’atwa na meno, huku zikiwa na vidonda vinavyodaiwa vimetokana na kuchomwa na kitu chenye ncha kali. “Wazazi wa mtoto huyo ni wanangu, siku moja mama huyo alimuumiza mkono. Nilimchukua na kukaa naye nyumbani kwangu kwa mwezi mmoja nikimuhudumia kwa kumkanda kwa maji ya moto,” alisema Stella.
  Mwalimu wa Shule ya Msingi Mlongazila, Paulo Idana ambaye pia ni katibu wa dawati la kutetea haki za binadamu, alisema suala hilo limewafikia, hivyo wanachukua hatua za kisheria huku mtoto huyo amewekwa chini yao kwa matibabu zaidi.
  “Tulimfuata mama huyo Septemba 20 mwaka huu na tulifanya nae mahojiano mbele ya ofisa mtendaji wa kijiji na alikiri akisema alifanya hivyo kwa sababu ya hasira. Tunafanya utaratibu ili tumfikishe kwenye vyombo vya sheria,” alisema Idana.
  Akieleza mkasa huo, mtoto huyo alisema wakati mwingine mama yake alikuwa akimwita ili amfundishe kusoma na aliposhindwa aling’atwa mgongoni, mapajani na sehemu za siri huku akisema atamfanyia hivyo hadi ajue kusoma.
  Mama wa mtoto huyo, Moshi, alisema alikuwa akitoa adhabu kwa mwanaye huyo kutokana na kujisaidia haja ndogo na kubwa hovyo wakati akirudi shule.
  “Nafanya hivi kutokana na hasira siwezi nikamuona mtoto wangu anajisaidia haja kubwa na ndogo kwenye nguo nikamwacha tu, lazima nimwadhibu… jana alitapika kwenye sahani. Je, mtoto kama huyu nitamwacha?” alihoji Moshi. Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Khadija Samizi alikiri kuwepo kwa tukio hilo.

NI KWELI NILIKAMATWA CHINA KWA SKENDO HII YA SASA, LAKINI NAMSHUKURU MUNGU NIMEYAMALIZA MWENYEWE WATANZANIA WA




                                      Rehema Fabian.

WAKATI msanii Agness Gerald ‘Masogange’ akisubiriwa kutua Dar baada kumaliza msala wake huko Afrika Kusini, skendo ya baadhi ya wasanii Bongo kuhusishwa na usafirishaji wa madawa ya kulevya ‘unga’, lingine limeibuka ambapo Video Queen Rehema Fabian amekiri kukamatwa nchini China kwa ishu hiyo.
Madawa ya kulevya.
Wiki mbili zilizopita kulizagaa habari kutoka kwa marafiki wa karibu wa Rehema ambao walidai kuwa mshiriki huyo wa Miss Kiswahili 2009 alikamatiwa huko Shaghai baada ya kukutwa na mwanaume aliyekuwa na unga.
Baadhi ya Watanzania waishio China walitofautiana ambapo wakati wengine wakidai kuwa alikamatwa na wapo waliosema kukamatwa kwake kulitokana na kupitiliza muda wa kuishi nchini humo tofauti na viza yake inavyoeleza.
Katika kipindi hicho chote, Ijumaa Wikienda limekuwa likimsaka ambapo wikiendi iliyopita lilifanikiwa kuchati naye ili kupata ukweli wa ‘niuz’ hizo.
Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Rehema?

Rehema: Mambo poa tu. Nani mwenzangu?
Ijumaa Wikienda: Unachati na gazeti la Ijumaa Wikienda. Kuna taarifa zimezagaa Bongo kuwa umekamatwa na unga China. Hizi habari zina ukweli?
Rehema: Ni kweli nilikuwa mahabusu. Mateso ya huko wee acha tu. Nilipata kesi lakini si yangu ila namshukuru Mungu nimetoka salama.
Ijumaa Wikienda: Kesi inahusu nini na kama ilikuwa haikuhusu kwa nini ulikamatwa?
Rehema: Nilikamatwa na mtu (hakutaka kumtaja na ni nani kwake) alikuwa na unga, nimekaa mahabusu wiki mbili na siku mbili. Uzuri huyo mtu alikataa mbele ya polisi kuwa hanifahamu na sihusiki ndipo nikaachiwa.

WASIWASI WATANDA MSANII RAY KUSOMEWA ALALBADIR KUVIMBISHWA “BUSHA” KISA MKE WA MTU, ATAKIWA KUMUOMBA RADHI RAFIKI YAKE FRANK MTAO KUHUSU MKEWE, CHUCHU HANS APIGWA TARAKA!

 Frank Mtao ambae amedaiwa kumpa taraka mkewe Chuchu Hans kisa  rafiki yake Ray
 Msanii Ray akiwa kwenye majukumu ya kuigiza
  Chuhu Hans





 Moja ya Layout ya gazeti pendwa liliripoti habari ya fumanizi la Ray na Chuchu Hans.

 Chuchu Hans akiwa na mtoto wake


Na Mwandishi Wetu
Ni kipindi kirefu sasa kumekuwa na madai ya kashfa ya msanii Vicent Kigosi “Ray “ kudaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi  na mke wa mtu ambae pia ni msanii wa bongo muvi Chuchu Hans huku vyombo mbalimbali vya habari hasa magazeti pendwa yakiripoti kwa kina tukio hilo.
Habari za ziada zilizonaswa na Xdeejayz toka kwa mtu wa karibu na familia ya Frank Mtao zilisema kuwa taarifa za Ray kutembea na Chuchu Hans zinaukweli kubwa sana kwani hata tukio la hivi karibuni la Ray kufumaniwa na akiwa na Chuchu Hans wanazichukulia kama ni za ukweli kwani Johari ambae ndiye mchumba harisi wa Ray aliwahi kukutana na mmoja wa wanafamilia wa Frank Mtao na kuwaeleza kila kitu.
Hata hivyo  Ray  inadaiwa amesababisha ndoa ya Frank Mtao kuvunjika kwani hivi karibuni Frank Mtao ambae anaishi nchini Austaralia baada ya tukio la kufumaniwa mkewe na Johari akiwa na Ray nyumbani kwa Chuchu mtangazaji huyo amemtwanga taraka Chuchu Hansa ambae sasa hivi maisha yanamwendea kombo baada ya kushindwa kulipia pango ya nyumba maeneo ya Msasani na kuhamia Mwananyamala kwa Mama Zacharia uswahili.
Aidha  katika hali isiyokuwa ya kawaida Ray anadaiwa amekuwa akimng’ong’a Frank Mtao kwa kujifanya kuwa ni rafiki yake wa karibu  na mara nyingi amekuwa akimpigia simu Frank Mtao na kumuweka roud speak wakati akiwa na Chuchu Hans.
Chanzo hicho kiliendelea kueleza “ Kwa kweli inasikitisha kuna siku Ray alikuwa na Chuchu Hans alimpigia simu Frank Mtao na kuanza kutaniana nae na baadae alimuuliza kama huko hana demu  na Frank alimjibu kuwa anae wa kuzugia na Ray alihitaji Frank amtumie picha yake na Frank alifanya hivyo na picha hiyo aliiona Chuchu Hans na baadae palizuka mtiti mzito” Alisema dada huyo ambae alisema yeye ni binamu wa familia ya Frank.
Aidha watu mbalimbali wameonesha wasiwasi wao kuwa huenda Frank Mtao akalipa vibaya kwa kumsomea alalbadir msanii Ray na kama kweli tuhuma anazotuhumiwa zitakuwa za kweli msanii huyo atakuwa amejipatia matatizo makubwa kutokana na dua hiyo jinsi inavyofanya kazi kama tukio lina ukweli na huenda akashushwa “busha” na baadae atalazimika kutembea na mkwangwaju.

MSICHANA MREMBO KULIKO WANAWAKE WOTE DUNIANI ACHUKUA TAJI LA UREMBO WA DUNIA, JARIBIO LA WAISLAM WENYE ITIKADI KALI WASHINDWA KUVURUGA ONESHO!


Mrembo wa Duinia 2013, Megan Young wa Philippines baada ya kutwaa taji hilo.
Mrembo wa Duinia 2013, Megan Young  (katikati) wa Philippines akiwa na mshindi wa pili Marine Lorphelin (kushoto) wa Ufaransa, na mshindi wa tatu Carranzar Naa Okailey Shooter (kulia) kutoka Ghana.
Warembo mbalimbali walioshiriki shindano hilo.

MREMBO wa Philippines alivishwa taji la binti mzuri zaidi duniani mwaka huu (2013) jana huko mjini Bali, Indonesia, ambapo kulikuwa na wasiwasi kwamba Waislam wenye msimamo mkali walikuwa wamedhamiria kulivuruga tukio hilo.
Mlimbwende huyo, Megan Young, mwenye umri wa miaka 23, aliyezaliwa Marekani, ambaye anachukua mafunzo ya upigaji wa filamu, alipokea taji la mashindano hayo kutoka kwa mshindi wa mwaka jana, Wenxia Yu wa China, na akaahidi kuwa “mlimbwende bora zaidi duniani ambaye hajawahi kutokea".
Maelfu ya Waislam wa chama cha Islam Defenders Front waliingia mitaani tangu mwezi uliopita wakipinga kufanyika kwa mashindano hayo nchini Indonesia, nchi ambayo ina Waislam wengi zaidi duniani, wakiyaita mashindano hayo kuwa ni “maonyesho ya ngono”.
Upinzani huo uliwalazimisha waandaji kulihamisha tukio hilo kutoka Jakarta kwenda Nusa Dua, kusini mwa Bali.
Katika kulifahamu hilo mapema, balozi za Marekani, Uingereza na Australia zilitoa vibali vya kwenda kwenye shindano hilo kwa kuwaonya wenye kusafiri kwamba tukio hilo la mashindano ya urembo lilikuwa limepangwa kuvurugwa. Hata hivyo, polisi wa Indonesia walisema hapakuwepo na vurugu zozote siku ya Jumamosi.
Marine Lorphelin, mwenye umri wa miaka 20 kutoka Ufaransa, alishika nafasi ya pili na Carranzar Naa Okailey Shooter (23) kutoka Ghana alikuwa wa tatu.

MH.MBOWE APATA PIGO KUBWA DADAAKE ALIYEHAMIA CCM TOKA CHADEMA AFARIKI GHAFRA NJIANI!

 
DADA wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amefariki papo hapo baada ya gari alilokuwa akiendesha kupasuka tairi ya mbele na kuingia chini ya daraja baada ya kupinduka na kusababisha watu wawili kufa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya.

Dada huyo, Grace Aikaeli Mbowe,  anayesadikiwa kuwa na umri kati ya miaka 47 hadi 50, alikuwa akiendesha gari yenye namba T 277 CAJ aina ya Toyota Cresta akiwa na mumewe  aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Lukindo (52), wakitokea Jijini Tanga, walipata ajali hiyo eneo la Kabuku wilayani Handeni.


Kamanda wa polisi mkoani Tanga (ACP) Costatine Massawe alisema kupitia Ofisa wake wa upelelezi mkoani Tanga, Bw Aziz Kimata, kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:30 asubuhi jana  katika eneo hilo baada ya gari hilo kupasuka tairi ya mbele kulia na kisha kuingia chini ya daraja lililokuwepo eneo hilo.

"Ni kweli kuna ajali ilitokea eneo la Kabuku gari aina ya Cresta lililokuwa likiendeshwa na ndugu inavyosemekana wa Bw Freeman Mbowe, limepata ajali baada ya kupasuka tairi la mbele na kuacha barabara na kuingia chini ya daraja .


"Dereva anayeitwa Grace Aikael Mbowe na mtu anayesemekana ni mumewe anayeitwa Ibrahim Lukindo, wamefariki na watu watatu waliowachukua wamejeruhiwa," alisema RCO Kimata.

Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Bw Ridhiwani Bakari (29) aliyekuwa na mkewe Zeddy Nzuke (29) raia wa Kenya aliyekuwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili na miezi minne aliyefahamika kwa jina la Mariam Ridhiwan ambao kwa sasa wamelazwa katika hospitali ya Magunga wilayani Korogwe.

 
RCO Kimata aliyezungumza kwa niaba ya kamanda huyo wa polisi alisema chanzo cha ajali hiyo inasemekana kimetokana na kupasuka kwa mpira huo na mwendo kasi wa kawaida na kwamba majeruhi na maiti zimehifadhiwa kwenye hospitali hiyo.
 
Mwandishi wa habari hizi, aliyefika kwenye hospitali hiyo na kuzungumza na Ridhiwani pamja na mkewe ambaye amelazwa wodi namba mbili ya wanawake katika hospitali hiyo, alisema kwamba ndoto zake za kufanya kazi Dar es salaam zimezimika ghafla kutokana na kwamba alikuwa aende kupamba kazi ya uofisa ugavi katika taasisi moja ya fedha ya marehemu Mbowe Jijini Dar es salaam.
 
"Nilikuwa naenda kupewa kazi na mama Mbowe katika Institution yake ya Micro-Financial Jijini Dar es salaam, mimi ni procurement (Mgavi-manunuzi) na ni Mkenya kwetu ni Eastern Province Kang'undo na nimeolewa na bwana Mtizedi...Lakini sasa ndoto zangu za kufanya kazi Dar es salaam zimezimika ghafla," alisema Zeddy akiwa kitandani amelala na mwanwe ambaye alikuwa haongei tangu amefika katika hospitalini hapo.
 
Mumewe na mwanamke huyo akizungumzia ajali hiyo alisema kuwa hakuwa akijua kwani alikuwa amelala dakika tatu kabla ya kutokea ajali hiyo ambapo alishtukia yeye, mkewe na mwanawe wametupwa chini kwenye majani wakiwa hawajijui na walikimbizwa katika hospitali hiyo ya Korogwe
 
Ridhin ambaye ni mkazi wa Nguvumali Jijini Tanga, alisema safari yao hiyo ilikuwa ifanyike Jumamosi mchana lakini kutokana na na kuchelewa kwa wenyeji wao hao, waliondoka Tanga kwenye hoteli ya Doliphin walikolala majira ya saa 11:00 alifajiri kwa ajili ya kwenda Jijini Dar es salaam.
 
Muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo Bi Nayela Missingo alikiri kuwapokea wagonjwa hao ambapo alisema wanafanya jitihada za kuwahamishia katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam mtoto Mariam ambaye amepata majeraha katika kichwa chake na kwamba tangu afikishe hospilaini hapo hakuwa katika hali nzuri, haongei walakunyonya.


 
  Bi Zeddy Nzuke  na mtoto wake wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Magunga wilayani Korogwe baada ya kupata majeraha katika ajali hiyo

WANANCHI WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA ALIYEWAPIGIA MAGOTI WANANCHI WAKE KUONESHA UNYENYEKEVU, VIONGOZI WENGINE WATAKIWA KUIGA TABIA HIYO!

 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8dysIPBzfJjyDfTAIhGw0Jwu8x41xUZNhGMHrEEq7YVCF3ESNZZOj0ZvJPtCE5jxXSktDofI_V0-y9tZ-K8VYaGGcqhx2716Dcfoxj_ieyQhR1R7SojrG2Z3VN2hHEmKreTUtmRF5fklA/s1600/dc.jpg
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya akiwa amewapigia wananchi magoti kwa maana ya kuonyesha unyenyekevu
Mbulu. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya, amesema kuwa aliwapigia magoti wananchi wa Kijiji cha Hydom, ili kuonyesha unyenyekevu kwa wananchi hao aliodai walionekana kujazwa maneno ya uchochezi na wanasiasa ili wavuruge amani .

Alisema kutokana fujo zilizofanywa na baadhi ya wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika majuzi, kwa nafasi yake angeweza kuagiza hata Jeshi la Polisi kuwadhibiti watu, lakini misingi ya dini yake haimruhusu kumdhuru mtu zaidi ya kumwonyesha unyenyekevu.
 
 

Alisema hali hiyo ndiyo iliyomfanya kuamua kupiga magoti na kumshtakia Mungu.

“Mimi ni mkristo, unyenyekevu ndiyo nguzo pekee ya kuonyesha upendo na kudumisha amani. Ningeweza kuagiza polisi wawadhibiti, lakini sioni sababu kwa kuwa hiyo siyo misingi ya utawala. Ndiyo maana nikaona bora nitumie njia nyingine ya kumshirikisha Mungu mbele yao,”alisema Choya na kuongeza:

“Wanasiasa wamekuwa wakipandikiza chuki kwa wananchi kwa makusudi kwa lengo la kuvuruga amani lakini kwa kumweka Mungu mbele nina imani tutafanikiwa ili siku moja tusije tukaingia kwenye mkumbo wa Syria na Misri”

Choya alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na Mwananchi Jumapili, siku chache baada ya kitendo chake cha kupiga magoti mbeye ya wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Haydom.

Mkuu huyo wa wilaya alidaiwa pia kuwalaani baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Haydom kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kumdharau na kutofuata maagizo yake, wakati yeye amewasaidia katika kutatua migogoro mbalimbali waliyokuwa nayo.

Tukio hilo la kusikitisha lilijitokeza baada ya wananchi wa kijiji hicho kupinga agizo la Choya, lililowataka kufanya uchaguzi wa kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho, kabla ya kufanya uchaguzi mdogo, ambapo walipinga kwa kudai kuwa hakuna sheria hiyo.

Mmoja wa wananchi hao alilumbana na mkuu huyo wa wilaya mbapo Choya alijibu; “Nami nitarudi kwetu." Naye Tikin akasema tena: “Unasema utarudi kwenu Biharamulo wakati hawakutaki kwani ulifukuzwa ubunge?”
Maneno hayo yalionyesha kumkwaza Choya ambapo alipiga magoti huku machozi yakimlenga na kumwomba Mungu afanye jambo kwa watu wa Haydom kwani wanamdharau kabla ya kujitokeza wazee watatu wa Haydom na kumwomba msamaha mkuu huyo wa wilaya