TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Sunday, September 29, 2013

MAJAMBAZI WAFANYA UMAFIA BENKI DAR, WAPORA ZAIDI YA TSH 150, WALIINGIA WAKIWA NA SARE ZA POLISI KUWAZUGA WAFANYAKAZI!




Majambazi saba akiwemo mmoja ambaye amevalia sare za polisi wameiteka benki ya I&M  jijini Dar es Salaam na kuchukuwa fedha zinazohisiwa  kuwa  ni zaidi ya shilingi milioni 150 na kutokemea kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea katika benki hiyo iliyoopo katika makutano ya mtaa wa Indira Gandi na Mosque ambapo baadhi ya mashuhuda wameelezea tukio hilo lilivyokuwa.
 
Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoa wa Ilala kamanda Marieta Minagi amesema bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio lenyewe ingawa  mpaka sasa ni kama milioni zaidi  150 zinahisiwa kuibiwa.
 
Naye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiki akiwa katika eneo hilo amesema  matukio ya Kuiba fedha katika benki yanazidi kushamiri na hivyo kuna haja ya taasisi husika kujipanga  upya.
  Hata hivyo ITV ilishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakipandishwa katika gari la polisi lenye namba za usajili  T220 AMV na kuondoka  nao kwa ajili ya mahojiano  zaidi

JAMANI WAUME WA WATU NI SUMU ACHANENI NAO KABISA, ONENI DADA HUYU ALIVYOPIGWA NYEMBE KWENYE SHAVU BAADA YA KUFUMANIWA NA MUME WA SHOSTI WAKE!



Hawa  ni  mabinti  wawili  ambao  walikuwa  ni  marafiki wa  damu.Urafiki wao uliingia  dosari  baada  ya  mabinti  hao  kusalitiana  na  kuchukuliana  wapenzi....

Anayevuja  damu  usoni ni  binti  ambaye  amechanwa   nyembe  na Magreth  ( rafiki yake ) akimtuhumu  kutembea  na  mpenzi wake.


MAJAMBAZI WALIOMVAMIA FEZA KESSY KUMBE WALITUMWA NA MAADAU WAKE KUMFANYIA KITU MBAYA!




  Siku ya jana mitandao kadhaa ya kijamii ilitaarifa habari ya kusikitisha ya aliyekuwa mshiriki wa Big Brother da Chase Feza Kessy baada ya kuvuamiwa na majambazi wenye silaha nzito, hivyo wasomeji wengi walielezea tukio hilo huenda ni la utengeneza na wabaya wake waliokuwa na nia ya kummalizi.
Feza Kessy  alipatwa na matatizo ya kuvamiwa na majambazi wenye silaha siku mbili zilizopita. Feza Kessy amesema kwamba tangu avamiwe na majambazi hao hajisikii kuwa na amani kabisa. Feza Kessy anaendelea kuwashangaa hao majambazi kwamba silaha walizobeba zilikuwa za nini?, au walidhani kwamba anapesa wakati hakushinda Big brother na alikuwa hana kazi kwa muda miezi mitatu iliyopita. Pole sana Feza Kessy na hizi ni tweet zake akielezea tukio hilo

MASKANI SERIKALI YAYAFUNGIA MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA KUTOCHAPISHA HABARI ZAKE TENA!


Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.
Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013. Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali (Government Notice ) Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.
Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani, mfano tarehe 17 Julai, 2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini. Aidha, katika toleo la Jumamosi, tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI” habari hiyo ilikolezwa na picha ya Mbwa mkali mwenye hasira. Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam. Jambo ambalo halikuwa la ukweli. Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti.
Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake hakiwezi kupitisaha au kuingiza Mbwa katika maeneo ya ibada. Hivyo basi, kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.
Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi. Gazeti hili limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za fani ya Habari.
Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano; Katika toleo na 7262 la 20 Machi, 2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”, tarehe 12 Juni, 2013, toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”. Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika. Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga walioumizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishutumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi. Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa haviwasaidii.
Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania kutochapishwa kwa muda wa siku tisini (90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332 (Government Notice No.332) la tarehe 27 Septemba, 2013,. Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini, kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.
Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma, kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu. Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia. Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani nchini.
Imetolewa na;
MKURUGENZI IDARA YA HABARI WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO 28 SEPTEMBA, 2013

Friday, September 27, 2013

RAY C AHAIDI KUMPA URODA WA BURE KWA MTOTO WA WAZIRI AMBAE ALISAIDIA KUOKOA WATU WENGI WAKATI WA MASHAMBULIZI YA KIGAIDI WESTGATE KENYA, HUENDA AKAENDA KWA AJIRI YA KUTIMIZA AZMA YAKE HIYO!





Abdul Haji ni miongoni mwa mashujaa ambao hawatasahaulika nchini Kenya kutokana na kuamua kuhatarisha maisha yao ili kuokoa watu waliokuwa wamekwama ndani ya jengo la Westagate baada ya kushambuliwa na Al-Shabaab Jumamosi iliyopita.
Tangu asimulie namna alivyopambana na magaidi hao, Haji ametokea kuwa kipenzi cha watu wengi hasa wasichana na mmoja wa watu aliowagusa ni Rehema Chalamila ambaye amesema anatamani mwanaume mjasiri kama yeye ambaye watazaa naye watoto.
“In love with ths Soldier!i want a soldier like him to marry me,” ameandika Ray C kwenye picha ya gazeti aliyoipost kwenye Instagram ikimuonesha Abdul Haji.
“I love You Abdul Haji,You are my Heroooooooo,” aliandika Ray C kwenye picha nyingine.
Kwenye picha nyingine Ray C aliongeza, “My soldier,My Prince,My Love….Love You Abdul Haji.”
Kijana huyo ni mtoto wa waziri wa zamani wa ulinzi nchini Kenya ambaye alienda kwenye mall hiyo baada ya kupata ujumbe kutoka kwa rafiki yake kuwa kaka yake alikuwa ndani ya Westgate wakati watu hao wenye silaha walipovamia.
Akiongea na NTV, Haji ambaye sio mwanajeshi, alisema alifundishwa kutumia bunduki na baba yake ili kulinda mifugo yao isiibiwe na wezi.
Ujuzi huo ulimsaidia Jumamosi hiyo kuwasaidia wafanyakazi wa Red Cross wafanye kazi yao kwa usalama kwa saa tatu na kusaidia kuokolewa kwa watu wafikao 1,000 nje ya mall hiyo

POLISI WALIYEMPIGA SHOGA NA KUMDHALILISHA WAZUSHA BALAA, MASHOGA WAANDA MAANDAMAMO MAKUBWA WAKIWEMO TANZANI!


Na Xdeejayz kwa msaada wa mtandao.
Shoga  moja  nchini  Nigeria  limejikuta  likiangukia  mikononi  mwa  polisi  wa  nchini  hiyo  baada  ya  kujifanya  ni  DEMU...
Shoga  hilo  lilikuwa  na  mazoea  ya  kuvaa  nguo  za  kike  na  urembo  mwingine  wa  kike  ikiwa  ni  pamoja  na  keseti  nywele  zake  ili  kuwarubini  wanaume....
Kwa  kifupi  ni  kwamba, ukiliona  ni lazima  ULIMEZEE  MATE...Likivaa  nguo  za  kike,...linapendeza  kuliko  hata  wanawake...
Nyuma  limefungasha  kiaina  ( choo kipo )  na  kifuani  huweka  matiti ya  bandia...Ukilitongoza  ujue  utapewa KABANG ( kiboga )  , maana  ni  dume  hilo.
Wanaume  ambao  si  wadau  wa  KABANG, waliamua  kulilipoti  polisi  ambapo  lilikamatwa ...
Mateso  aliyopewa  huyu  shoga, nadhani  hatakaa  ayasahau  maishani  mwake..
Hata hivyo tukio limeonekana kuwa kera mashoga wote duniani wakiwemo wa hapa nchini Tanzania hivyo wametishia kufanya maandamano makubwa.
Kwa mujibu wa mtandao mmoja nchini humo. 

FILAMU YA UFUSKA YA MSANII MANAIKI SANGA YAVUNJA REKODI SASA YAFIKIA ODA KOPI ELFU 38 NCHI NZIM, KAMPUNI YA USAMBAZAJI YA STEPS YAVUJISHA SIRI NZITO!!

Na Mwandishi Wetu.
Katika hali ya kushtua kuna taarifa kuwa filamu ya msanii kina kwa ufuska kwenye kiwanda cha bongo movie Manaiki Sanga "The Don" ameweka rekodi mpya nchini kufuatia filamu yake kufikisha kopi nyingi ambazo huenda kiasi hicho hakijawahi kufikiwa na msanii yeyote.

Habari za uhakika toka kwa mtu wa karibu na kampuni ya Steps ambae aligoma kutaja jina lake kwa madi kuwa yeye si msemaji wa kampuni hiyo alisema " Kwa kweli hii ni kali unajua hadi sasa hapa ofisini tunapokea maelfu ya filamu wakihitaji kupata nakala ya filamu ya msanii huyo" Alisema kijana huyo wa kihindi

Aidha kijana huyo aliongeza kusema kuwa kitu kikubwa kinachofanya watu kuisubiri kwa hamu filamu ni kutaka kuona msanii huyo aliyejizolea umaarufu nchini na dunia nzima kutokana na picha za utupu za mabint zaidi ya 400 ambao baadae hao mabint  wote kuwafanyisha filamu hiyo inayoitwa Ngema huku pia mastaa mbalimbali wakishirikishwa.
Kijana huyo alimaliza kusema kampuni ya Steps imeichukua filamu hiyo na tayari wako kwenye makubaliano ya mwisho na Manaiki na huenda ikapewa nafasi ya kuachiwa haraka mtaani kutokana na wananchi wengi nchini Tanzania na Kenya, Kongo na Uganda kutaka filamu hiyo kuwafikia ili kuona nini kilichopo ndani yake.