Mwandishi wa habari za uchunguzi na watoto toka E-fm Radio Bw Livingstone Mkoi akimuhoji mama huyo na kuelezea jinsi tukio hilo lilivyomshtua kiasi cha presha yake kupanda hadi kulazwa Hosptal ya Mwananyamala
Hili ni dela ambalo msichna huyo mwenye umri wa mika 14 alikuwa amelizaa siku ya tukio kabla ya kubakwa, na hizo ni damu zilizotokana kubakwa.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAJIKI " Wanawake Katika Jitihada za Maendelea" Janeth Mawinza akizungumza na Mwandishi Livingstone haonekani pichani, ambapo taasisi hiyo imelani vikal tukio hilo na kuliomba Jeshi la Polisi ikibidi Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr John Pombe Magufuli kusaidia suala hili.
Baba mkubwa wa binti huyo akionesha dela hilo lilivyotapakaa damu
Mwanafunzi wa kitado cha tatu, Jina lake na shule anayosoma vinahifadhiwa kwa ajili ya maadili, akizungumza na mwandishi Livingstone Mkoi pembeni na kueleza jinsi alivyochungulia kifo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar Kamanda
Simon Sirro ameombwa na wananchi kuunda timu maalum kwa ajiri ya kuchunguza tukio hilo la kubakwa mwanafunzi huyo, huku mtuhumiwa akiwa na vitambulisho viwili vya kupigia kura, huku mtuhumiwa huyo akidaiwa kujihusisha na mambo ya kiharifu sehemu mbalimbali ikiwemo Mombasa nchini Kenya.
Rais Mgufuli, wananchi wameomba kutia mkono wake kwenye sakata hilo la mtuhumiwa huyo kukutwa na shahada mbili za kupigia kura.
RC Makonda
Hizi ndiyo shahada 2. za kupigia kura zilizokutwa chumbani kwa mtuhumiwa maeneo ya Mwananyamala Mchangani Jijini Dar hivi karibuni
Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Katika hali ya kushtua mwanafunzi wa kidato cha tatu kwenye shule moja iliyopo Temeke Jijini Dar jina linahifadhiwa amenusa umauti baada ya kubakwa na kuchanwa vibaya na kumsababishia maumivu makali.
Tukio hilo lililotoke maeneo ya Mwananyamla Mchangani Jijini Dar na kulipotiwa kituo cha Polisi CCM Mwinyijuma na kupewa kumbukumbu hizi MW/RB/148/2016, na kuwaacha wananchi midomo wazi na majonzi baada ya mtuhumiwa huyo pia kukutwa na shahada mbili za kupigia kura zenye jina lake moja.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni, ambapo kwa mujibu wa wanafamilia wa mwanafunzi huyo walisema kuwa kijana huyo ambae alikuwa anajihusisha biashara ya duka na kutoa na kuweka pesa, ambapo alianza kumdanganya binti huyo kwa kumnunulia chipsi kuku pamoja na kumpa pesa zaidi ya zile alizokuwa anapewa na wazazi wake.
Hali hiyo ya jemba hilo kumuhadahaa binti ilidumu kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kumshawishi bint huyo kwenda chumbani kwake maeneo hayo hayo ya Mwananyamala Mchangani.
Akiongea na mwandishi wa maskanibongotz binti mwenyewe alisema kuwa siku ya tukio kijana huyo alimwambie aende chumbani kwake usiku kwani ana mazungumzo muhimu sana ndipo alipokwenda na kumkuta ya kumkuta.
Msichana huyo akiongea kwa uchungu mara baada ya kutoka Hospital alikolazwa zaidi ya wiki moja.
Msichana huyo alisema" Mara baada ya kufika chumbani kwake alianza kunibaka kwa nguvu licha ya kupiga kelele lakini sikupata msaada na dakika chache baadae nilianza kusikia maumivu makali pamoja na damu nyingi kunitoka na nilijitizama vizuri kumbe nilikuwa nimeshachanika upande wa chini na juu wa maumbile yangu" Alisema msichana huyo huku machozi yakimtoka
Baada ya kuona hali mbaya za binti huyo ambae sasa wakati huo alikuwa anatoka mapande ya damu kama yanavyoonekana pichani alimruhusu aondoke kwa vile nyumbani kwao hapakuwa mbali lakini cha kusikitisha njia nzima damu ilikuwa ikimmwagika.
Hata hivyo alipofika nyumbani binti alizidiwa na kudondoka wazazi wake walipomkaugua ndipo walipogundua kama mtoto wao amebakwa na haraka walikwenda kituo cha polisi CCM Mwinyijuma na kutoa taarifa juu ya tukio hilo na alipewa pf3 na kukimbizwa Hospital huku askari wengine wakienda nyumbani kwa mtuhumiwa lakini kwa bahati mbaya walimkuta amekimbia na kuacha kila kitu chumbani kwake vikiwemo vitambulisho viwili vya kupigia kura vyenye jina lake.
Sakata hili la kubakwa mwanafunzi huyu linakwenda kwa kusua sua sana kiasi cha familia ya msichana huyo kumuomba Rais John Pombe Mgufuli au Waziri Mkuu kuwasaidia kwa kile walichodai Polisi kuna mambo mengi sana isitoshe Mama wa mtuhumiwa amefunga safari toka Mombasa na kufika kituo cha Polisi Osterbay na kudaiwa kuweka mipango sawa.
Aidha wananchi wameliomba Jeshi la Polisi Kanda Maalum kulichukulia kwa usiliasi hili jambo lwa mtuhumiwa huyu kukutwa na shahada mbili za kupigia Kura je alizipataje na kisha litoa majibu kwa wananchi.
Maskanibongotz ilifanya mawasiliano na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni na kutaka kufahamu kama taarifa za tukio hili zipo mezani kwake tayari ama laa, kwa bahati mbaya simu yake iliita bila kupokelewa.
Credit: maskanibongotz