Kumetokea Mlipuko katika mgodi wa makaa ya mawe magharibi mwa Uturuki ambao umesababisha vifo vya zaidi ya wachimbaji migodi 200 na kujeruhi wengine wengi kujeruhiwa kwa mujibu wa maafisa nchini humo.
Sehemu ambayo inasemekana ulianzia mlipuko huo ni kitengo cha kusambazia umeme katika mgodi huo ambao una zaidi ya wafanyakazi 780 kwa sasa waokoaji wanajaribu kila mbinu kuwafikia mamia ya wachimba migodi.
Ingawa hadi sasa inahofiwa kuwa wachimbaji mgodi wengine ambao idadi yao inatajwa kuwa kubwa bado wamefukiwa chini ya mgodi huo,japo inaaminika wengi waliweza kukimbia kuhofia usalama wao .
Mgodi huo ambao uko katika mji wa Soma,mkoani Manisa,takriban kilomita 250 kusini mwa Istanbul kwa sasa ripoti iliyotangazwa ya watu waliofariki ni 157 ndugu wa wachimbaji migodi hao wamekusanyika katika makundi karibu na mgodi huo ambao unamilikiwa na wawekezaji wa kibinafsi huku wengi wao wakilia hadharani na kububujikwa na machozi.
Chanzo cha moto huo kinasemekana ni kutokana na hitilafu ya umeme.
Imeandikwa na Bbc.
No comments:
Post a Comment