TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Wednesday, February 12, 2014

TAHADHARI KUBWA DAR: WAZUNGU WAINGIZA MAMILIONI YA EURO FAKE KUWAPIGA WANANCHI WAMESAMBAA SANA KWENYE VIBANDA VYA ATM, POLISI WATANGAZA HALI YA HATARI KWA WAKAZI JIJINI..!


 Hizi ni EURO Halisi

KAMISHINA WA POLISI KANDA YA MAALUM DAR, SULEMAIN KOVA
 Hii ni EURO feki kama inavyoonekana

Na Mwandishi wa Xdeejayz
Jeshi la Polisi Kanda ya Kinondoni limeanza msako mkali wa kuwasaka raia mmoja wa kigeni ambae ni mzungu na hajafahamika uraia wake kufuatia kuongoza genge la utapeli kwa wananchi kisha kwa kuwapatia pesa fake za kigeni.

Habari za kuaminika toka ndani ya kituo cha Polisi Oysterbay kilisema kuwa mzungu huyo mwanaume ambae anashirikiana na wakidada wawili raia wa Cameroon na Nigeria akiwemo mtanzania mmoja na tayari watu kadhaa wameshatapeliwa hela nyingi akiwemo mwandishi wa blog hii ambae wiki mapema wiki hii nae alitapeliwa kiasi cha shilingi laki mbili za kitanzania huku akiambuliwa kuepwa Euro mia moja ambazo ni feki.
Akiongea na Xdeejayz mwandishi wetu aliyeingizwa mjini na mzungu huyo alisema" Ilikuwa siku ya Jumatatu saa tatu za usiku nilienda kuchukuwa pesa kwenye ATM mashine na mara baada ya kufika pale nilichukuwa laki mbili keshi kwenye mashini wakati natoka chumba cha ATM nikakutana na mzungu huyo aliyekuwa amevalia suti nyeusi"
Alisema mwandishi wetu
Aidha mwandishi wetu aliongeza kusema kuwa baada ua kukutana mzungu huyo alimwambia kuwa anashinda sana kwani alikuwa anasafiri usiku ule kuelekea mwanza hivyo sehemu za kuchenji hela nyingi zilikuwa zimefungwa hivyo asaidiwe kupatiwa pesa shilingi laki mbili kisha atampatia pesa hizo za ikigeni euro mia moja.
Hata hivyo kutokana na muonekano wa mzgungu huyo ambae aivaa suti nyeusi ambae wakati wa kutoa hiyo pesa alitoa burungutu la noti hizo na kuchomoa noti mbili tu za hamsani hamsini euro na kumpatia mwandishi wetu ambazo baadae ziligundulika kuwa ni feki.
Baada ya tukio hilo mwandishi wetu alifungua taarifa kituo cha Polisi Oysterbay na kupewa kumbukumbu OB/RB/2971/14
KUTOA EURO FEKI/KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU. 
Hata hivyo kutokana na matukio inadaiwa mzungu guyo amewahi kukimbia gari yake kituo cha Polisi Kituo cha Kawe na isitoshe wananchi wametakiwa kuwa makini kutokana na kwamba wazungu hao wana pesa nyingi sana za kigeni ambazo wamepanga kuwatapeli wananchi na mara nyingi wamekuwa wakitembelea maeneo yote ya miji mikubwa kama Arusha, Dodoma, Mwanza na Dar huku wakizungukia maeneo ya kwenye ATM.
Hadi habari hii inaruka Kamanda wa Polisi Kanda Kinondoni hakuweza kupatikana ili kuzungumzia ishu hiyo ambayo ni hatari sana kwa wananchi kutokana na watanzania wengi huwaamini wazungu kuwa hawezi kuwa matapeli kama watanzania.
"DODOMA KUWAKA MOTO IJUMAA HII HAIJAWAHI TOKEA NI VALENTINE"

No comments:

Post a Comment