TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Wednesday, February 5, 2014

NJAA KALI NDIYO ILIYOWAPELEKA BONGO MOVIE CCM WASANII WENGI WAMEPOTEZA UMAARUFU NA WATAENDA KUWA MIZIGO KWENYE CHAMA,-MANAIKI SANGA "THE DON"..!








Na Mwandishi Wetu-Iringa
Mwanamuziki na msanii wa filamu nchini Manaiki Sanga maarufu kama The Don amewachana live wasanii wenzake wa Bongo Movie kuwa njaa kali na kupoteza muelekeo kwenye tasinia hiyo ndiyo imewafanya waiingie kwenye Siasa.
Akiongea kwa njia ya simu toka Iringa Manaiki alisema" Hii njaa ni noma hawa wasanii wa bongo movie wamepotea sana kujiunga na CCM kwani na ni dhahiri kuwa wamefanya hivyo kwa ajili ya ukata "njaa" ili wapewe tenda za kuuza nyago kwenye msimu wa kampeni mwakani" Alisema Manaiki ambae nae ni msanii wa kundi hilo
Aidha katika hatua nyingine Manaiki aliongeza kusema kuwa bahati mbaya wasanii wote waliojiunga na chama hicho kwa sasa hawana mvuto kwenye jamii tofauti na mwanzo hivyo huenda wataenda kukididimiza chama " Pale hakuna hata mtu ambae chama kinaweza kumsimamisha na kugombea ubunge ama cheo chochote mfano Jb kwa sasa amepoteza muelekeo kabisa kwenye jamii, Amanda hakuna hata anaemjua, Irene nae majanga matupu hawa wengine ndo kabisa, Richie nae hamna kitu" Alisema Manaiki Sanga
Hata hivyo juhudi za kuwatafuta wanabongo muvi hao ziligonga mwamba hadi habari hii ia nakwenda mitamboni.
"GAZETI LA MASKANI BONGO LIKO MTAANI KILA SIKU YA JUMATANO PATA KOPI YAKO|"  

No comments:

Post a Comment