Ni time ya kufahamu kuhusu tuzo ambazo hutolewa kwa Wanamuziki/Wasanii mbalimbali wa Tanzania zikiwa zimeanzishwa mwaka 1999 ambapo za mwaka huu 2014 zimezinduliwa leo February 17.
George Kavishe kutoka TBL ambao ndio Wadhamini wa tuzo hizi amesema
>>> ‘Maboresho makubwa ambayo tumefanya mwaka huu ni tofauti na
mara zote ambazo tumekua tukihusisha Watanzania dakika za kupiga kura
tu hivyo wanakosa nafasi ya kupendekeza nani aingie kwenye category
gani, mwaka huu tumebadilisha kutokana na matakwa ya soko hivyo
Watanzania ndio watapendekeza nani aingizwe kwenye category gani’
‘Kupitia Magazeti, website ya Kilimanjaro na vipeperushi kuanzia
kesho February 18 2014 kutaonyeshwa category zote za mwaka huu za
kupigiwa kura na Wananchi, Watanzania watatuma kura zao kupitia simu ya
mkononi kupitia 15440, unapendekeza msanii, kikundi au producer gani
aingie kwenye kipengele’ – Kavishe
‘Kwa hiyo Mwaka huu Watanzania watapiga kura mara mbili ambapo ya
kwanza ni nani aingie kwenye category alafu tutarudi tena kupiga kura
nani awe mshindi wa kwanza, yani mwaka huu ile timu ya watu 100 ya
Waandishi, Watangazaji na wadau wa muziki kuchagua nani na nani aingie
kwenye category haitofanya hivyo bali itakutana kuhakikisha tu kama
wimbo uliopendekezwa na Wananchi ni wa mwaka husika, uko sehemu husika
na pia kama umekidhi vigezo vya kuingia KTMA’ – Kavishe
MABADILIKO: Kwa mujibu wa Baraza
la sanaa la Taifa (BASATA), mabadiliko yaliyofanywa kwenye tuzo za
mwaka huu wa 2014 ni kutokana na maoni na mapendekezo ya wadau wa tasnia
ya muziki kutoa sababu mbalimbali.
Mwaka huu KTMA itakua na category 36 ambapo category 34 ni za kuchaguliwa na mbili zilizobaki ni zile maalum za kuteuliwa.
Mwaka 2013 kulikua na category 37 ambapo Mwaka huu imeondolewa moja
kutokana na maoni mbalimbali ya wadau wa muziki ambapo category yenyewe
ni Mtayarishaji chipukizi wa mwaka.
Category zilizobadilishwa majina mwaka huu 2014 ni Mtumbuizaji bora
wa kike wa muziki badala ya msanii bora wa kike ilivyokua mwaka jana,
mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki badala ya msanii bora wa kiume mwaka
jana, mwimbaji bora wa kiume Taarab ambayo mwaka jana ilikua msanii
bora wa kiume Taarab.
Mwimbaji bora wa kiume bongofleva badala ya mwaka jana Msanii bora wa
kiume bongofleva, mwimbaji bora kiume band ambayo mwaka jana ilikua
msanii bora wa kiume band, mwimbaji bora wa kike bongofleva badala ya
mwaka jana msanii bora wa kike bongofleva.
Mwimbaji bora wa kike Taarab badala ya mwaka jana msanii bora wa kike
Taarab, mwimbaji bora wa kike band badala ya msanii bora wa kike band.
BASATA wanasema ‘kwa nini kumekua na mabadiliko haya? ukiangalia
maana halisi ya neno Msanii linasadifu au linaleta maana za kuingia
zaidi ya kitu kimoja, kunaweza kuwepo na msanii wa uchongaji, msanii wa
Uchoraji n.k kwa sababu wanafanya kazi ya sanaa ndio maana tunatumia
majina ya kimuziki kwa sababu huku tuko kwenye muziki’
MENGINE
BASATA wanasema >>> ‘mwaka
huu tutakua na video bora ya muziki ya mwaka badala ya video bora ya
wimbo, neno muziki lina uwanja mpana kuliko wimbo…….. pia tutakua na wimbo
bora wa Afropop badala ya wimbo bora wa bongopop, kutakua na wimbo bora
wenye vionjo vya asili ya kitanzania badala ya wimbo bora wenye vionjo
vya asili’
‘Jingine ni Msanii bora chipukizi anaeibukia badala ya msanii bora
anaechipukia…. wapo wasanii wengi sana chipukizi huko mtaani na miziki
yao haijasikika, inawezekana amekaa miaka mingi akifanya kazi zake
lakini akaibuka na ameonekana’ – BASATA
"GAZETI LA MASKANI BONGO LIKO MTAANI KILA JUMTANO FATILIA KUONA MENGI JUU YA TUZO HIZI"
No comments:
Post a Comment