Ray na Chuchu wakijiachia.
Chanzo chetu makini kilieleza kuwa mastaa hao wamekuwa wakionekana
pamoja mara nyingi na hivi sasa inadaiwa kuwa wanaishi pamoja huku
wakiwa na mtoto wa Chuchu aitwaye Danzel.Mpashaji wetu huyo alizidi kudai kuwa kutokana na mapenzi hayo kukolea siku hadi siku, juzikati baadhi ya ndugu wa mastaa hao walianza vikao vya chini kwa chini ili kuhakikisha mwaka huu wasanii hao wanafunga ndoa lakini haijajulikana kama watafungia kanisani au msikitini kwa kuwa wana dini tofauti.
“Yaani sasa hivi hakuna siri hata chembe, ni fulu kujiachia. Mara nyingi wapo pamoja kila sehemu yaani kama njiwa,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kujazwa ‘info’ hizo na kumwagiwa picha za mastaa hao, gazeti hili lilimtafuta Chuchu kisha kumuuliza kuhusiana na penzi lake na Ray kuwa ‘shatashata’ ambapo alifunguka kuwa kama kuna mtu anawaona wakiwa pamoja ni kwa sababu hivi sasa eti wanaandaa ‘sinema’ yao wawili.
Alipotafutwa Ray ili kuulizwa kuhusiana na ishu hiyo, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa kwa muda wa nusu saa.
"VALENTINE DAY YA KIHISTORIA NDANI YA CLUB MAISHA WAPENDANAO KUPEWA MAUA YA UPENDO MLANGONI, DVJ MAJEY, ZUNGU MNYAMA KUWAPA ZWADI WAPENDAO NI IJUMAA YA WIKI HII USIKOSE KUSIMULIWA"
No comments:
Post a Comment